Sijui ni moyo au pressure, msaada wa haraka

Sijui ni moyo au pressure, msaada wa haraka

Boeing787-8

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2018
Posts
1,199
Reaction score
1,292
Wakuu napitia hali ngumu Sana.

Mwezi wa 11, nilikuja nkapata shida moja, yaani iliniperekea kupata stress, anxiety na totally ubnomal.

Sijakaa Sawa mwezi wa 12 nkafukuzwa kazi, aisee niliumia, nilikumbwa na stress sijawai pata,

Mwezi wa kwanza nkaachwa na mpenzi wangu niliyempenda kwa dhati.

Basi baada ya kufukuzwa kazi niliamua kujiajiri na kuanzisha bihashara, mungu anasaidia Hali sio mbaya.

Sasa kutokana na stress za kupoteza kazi, na stress za kuachwa, na stress za bihashara, yaani nkiwaza kidogo au kuwa na hasira, moyo unanidunda saaaaaaana, afu mtu akiniudhi kidogo moyo unanidunda saaaaana, yaaani mapigo ya moyo yanaenda mbio kinyama

Juzi nilipata mwanamke, wakati wa sex, during second ejaculation yaani niliishiwa pumzi nilidhani ntakufa au kuzimia.

Hospital sijaenda, Ila hii Hali ya mapigo ya moyo kwenda mbio Mara kwa Mara Ni magonjwa ya moyo au Ni pressure.

Wakuu ntawezaje kutibu hii hali, maana usiku naweza shikwa na mapigo ya moyo unaweza dhani moyo utachomoka, afu ukishapoa ntaskia maumivu kwa ndani badae.

Nifanyeje ndugu zangu, msaada tafadhali

Wasiwasi,stress, zitaniua
 
Wakuu napitia hali ngumu Sana.

Mwezi wa 11, nilikuja nkapata shida moja, yaani iliniperekea kupata stress, anxiety na totally ubnomal...
Tatua kwanza hizo stress then nenda hospitali
 
Dah! pole sana, jaribu kushabikia Simba. Kuna wengine ambao walikuwa na hali kama yako walipofanya maamuzi ya kuanza kushabikia Simba tu, hawana tena mambo ya pressure, wala BP, wala stress kila siku wao ni raha starehe.
 
1. Nenda hospitali.

2. Nenda kanisani kamuone Mchungaji mwelezee na kufanya maombi na upate mafundisho ya kusamehe na kuachilia na wewe kuwaomba msamaha ukowakosea.

3. Nenda kituo cha meditation cha wakorea.

4. Fanya mazoezi ya kutembea.

5. Kamuone Dokta wa psychiatrist.

6. Kama unauzito ulozidi jitahidi upungue.

Hayo yote yakfanyika sambamba utapona haraka sana.
 
1. Nenda hospitali
2. Nenda kanisani kamuone Mchungaji mwelezee na kufanya maombi na upate mafundisho ya kusamehe na kuachilia na wewe kuwaomba msamaha ukowakosea...
Shukran, kutembea natembea, uzito ni 60kg
 
Wakuu napitia hali ngumu Sana.

Mwezi wa 11, nilikuja nkapata shida moja, yaani iliniperekea kupata stress, anxiety na totally ubnomal...

Pole ndugu,
Kuna uwezekano wa uliyopitia kuwa msingi au sehemu ya unavyojisikia.

Pia, matumizi ya vinywaji kama kahawa, pombe kwa wingi na energy drinks.

Kutokupumzika kiasi cha kutosha.

Fika hospitali pamoja na mambo mengine ni mhimu kufanya vital signs:
Mfano:
1: Bp/presha yako
2: Pulse rate/mapigo ya moyo
3: Oxygen

Pia fanya baseline investigations kama:
1: Sukari
2: Damu/Fbp
3: ECG

Angalia uwezekano wa kukutana pia na Psychologist kama sehemu ya matibabu yako.
 
Back
Top Bottom