Sijui ndo uzee....

Sijui ndo uzee....

rafiki yangu HorsePower asante sana kwa mchango wako, lakini mimi sina tatizo kabisa na usingizi.
yaani kati ya watu wanaopenda kulala nadhani ni mmoja wapo, na pia nikijilaza kitandani tu nalala, bila tatizo lolote.
hapa tatizo linalonikumba ni kuwashwa macho, yaani ninaposikia usingizi tu basi macho yananiwasha vibaya sana, kama umewahi ona watoto wachanga wanavyowashwa na macho wanapotaka kulala basi na mimi hunitokea hivyo

Kwenye hiyo makala, mojawapo ya symptoms za huo ugonjwa iliyotajwa ilikuwa "Difficulty falling asleep at night or getting back to sleep after waking during the night" Kwa hiyo hata tatizo la kuwashwa macho wakati una usingizi lingeweza kuwa ni tatizo hilo hilo. Hata hivyo, madaktari wa hosp huwa wanaaminika zaidi kuliko ushauri wa kitabibu tunaotoa hapa.
 
Sidhani kama hilo ni tatizo. Maana umekua na hali hiyo tangu utoto sasa ni vema ukajikubali tu kua wewe ndivyo ulivyo. Unajua zipo tabia nyingi za kitoto ambazo tunakuwa nazo na zingine tukiwa wtu wazima zinatuacha. Chukulia mfano tabia ya kulia, yaani mimi huwa inanitesa sana. Siipendi kabisa lkn nimejaribu kujizuia nimeshindwa nimeamua kujikubali tu.
pacha, hata mimi naona hii ni tabia ambayo imegoma kutoka mwilini mwangu maana sikumbuki lini macho yaliacha kuniwasha nikiwa na usingizi. basi ngoja nijikubali tu
 
Bibie.@Fixed Point Hujatuambia una umri wa miaka mingapi?umeolewa au hujaolewa? Matatizo yako yamekuanza lini? ulishawahi kwenda hospitali?
rafiki, mimi nina umri mkubwa sana, ila sijui kama ni kigezo maana hata nilipokuwa teen bado macho hayakuacha kuniwasha, yaani ninavyojukumbuka muda wote macho huwa yananiwasha ninapokuwa na usingizi.
Nimeolewa kitaambo...
nilishawahi kwenda hosp na nikapimwa macho hayakuonekana na tatizo lolote ila nikapewa drops ambazo nilitumia na wala hayakuacha
 
Kuna mtu hapa JF aliniambia tiba ya ugonjwa kama huo ni kutembelea lile Jukwaa la chini kabisa (Note that huwa mimi silitembelei asilani!!). For more clarification muone Madame B.

Kama hutapona kwa muda wa wiki moja jua uzee umeingia, na uzee si ugonjwa. Ila inaumaje kuwaona warembo wabichi wanakonyezwa barabarani lakini wewe hata sonyo hupati!
mtani si unitajie tu hilo jukwaa.... sasa mimi nitalijuaje?
kuhusu kukonyezwa barabarani :tape:
 
........Tena macho yakiwasha washa usingizi wake mtamuu...ilikua inanitokea nikiwa prepo kama nimechoka kusoma
ha haaa, ila sasa kujikuna nako ni kasheshe, maana unatamani hadi kulia, basi tu
 
Chezeya kutoboa weye!!!!...lazima macho yawashe ati!!!..Aisee mie siku mbili last week Alhamisi na Ijumaa nikajifanya kuangalia movie home kuanzia saa sita za usiku hadi saa zote na nikaamka mapema. Jmosi nikawa na wageni hivyo nikashindwa kulala mchana, pamoja na hayo si mpenzi wa kulala mchana, kisha siku hiyo nikajifanya kwenda movie iliyoanza saa nne za usiku basi nusu ya movie nilikuwa nimeuchapa 🙂🙂 acha njemba zinicharure 🙂🙂 lakini pamoja na yote hayo macho hayakuwasha hata chembe ila ile movie lazima niione tena 🙂🙂
rafiki ulikuwa unakoroma kwenye movie? kwa nini njemba zilikucharukia?
mimi ni bingwa wa kusinzia kwenye movie lakini sijawahi kucharukiwa, lol!
movie inaitwaje?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwenye hiyo makala, mojawapo ya symptoms za huo ugonjwa iliyotajwa ilikuwa "Difficulty falling asleep at night or getting back to sleep after waking during the night" Kwa hiyo hata tatizo la kuwashwa macho wakati una usingizi lingeweza kuwa ni tatizo hilo hilo. Hata hivyo, madaktari wa hosp huwa wanaaminika zaidi kuliko ushauri wa kitabibu tunaotoa hapa.
nitarudi tena kwa dr. ingawa sina shida kabisa ya kupata usingizi, yaani nikipanda kwa kitanda tu nimeshaangusha gogo
 
rafiki, mimi nina umri mkubwa sana, ila sijui kama ni kigezo maana hata nilipokuwa teen bado macho hayakuacha kuniwasha, yaani ninavyojukumbuka muda wote macho huwa yananiwasha ninapokuwa na usingizi.
Nimeolewa kitaambo...
nilishawahi kwenda hosp na nikapimwa macho hayakuonekana na tatizo lolote ila nikapewa drops ambazo nilitumia na wala hayakuacha
bibie Fixed Point Umri wako mkubwa kama Tembo vile? unakataa hata kusema umri wako? unamuogopa nani hapa Jamii Forums? mimi umri wangu miaka 60 sasa wewe una umri wa miaka mingapi?jibu swali langu usikwepe tafadhali.
 
Last edited by a moderator:

mmmhhhh! nilipoandika hivyo nilitaka kusema mimi mkubwa kwako..... kumbe umenipita miaka 3 tu, happy?
 
pacha, hata mimi naona hii ni tabia ambayo imegoma kutoka mwilini mwangu maana sikumbuki lini macho yaliacha kuniwasha nikiwa na usingizi. basi ngoja nijikubali tu
Bora ujikubali haiwezekani na ujana au uzee huo leo igeuke kua ugonjwa. Zipo hali hatuzipendi lkn hatuna control nazo
 
Hahahahahah lol! Mie huwa sikoromi banaaa 🙂🙂 nikilala kimyaaaa hata sauti ya fan ni kubwa sana...Walinicharura kwa sababu walijitahidi kuniamsha bila mafanikio na hawajawahi kuniona nauchapa kwenye movie hata tukiingia za saa nne za usiku....Chezeya siku mbili za kulala masaa machache weye!!!!... Movie hii hapa rafiki itafute ukaione, mie lazima niione tena safari hii na macho maangavu tangu mwanzo hadi mwisho 🙂🙂

rafiki ulikuwa unakoroma kwenye movie? kwa nini njemba zilikucharukia?
mimi ni bingwa wa kusinzia kwenye movie lakini sijawahi kucharukiwa, lol!
movie inaitwaje?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom