Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,305
- 12,969
Baada ya kupita kwa awamu mbili za kwanza za Baba wa taifa marehemu Mwl Julius K. Nyerere na ile ya mzee Ally Hassani Mwinyi, marais waliofuata yaani wa awamu ya tatu Bwana Benjamini Mkapa na huyu aliyeondoka wa awamu ya nne Prof. Jakaya Kikwete walianzisha utaratibu mpya wa wake zao kuanzisha taasisi binafsi au NGO wakiwa ikulu.
Mke wa rais wa awamu ya tatu mama Anna Mkapa alianzisha taasisi au NGO yake aliyoiita EOTF na baaada ya kuondoka ikulu akaondoka nayo. Rais wa awamu ya nne mkewe mama Salma Kikwete alianzisha WAMA ambayo nayo atakwenda nayo. Sasa kama utaratibu huo utaendelea sijui mama Janeth Magufuli atakuja na NGO gani?
Labda tutegemee VIMA yaani Vijana na Maendeleo, au BAMA yaani Baba na Maendeleo au OA yaani Okoa Albino na pengine labda SAWA yaani Saidia Wazee.
Karibu sana ikulu mama Janeth Magufuli msaidie mzee kutimiza ahadi zake nyingi alizo ahidi. Mkumbushe asisahau kuanzisha mapema mahakama ya Mafisadi kama alivyosema akiingia tu hiyo itakuwa ni ajenda namba moja.
Nyingine ni kufuta ushuru wa biashara ndogo ndogo na mazao, kupunguza kodi za PAYE ba leseni za biashara, kufuta karo na michango yote shuleni ikiwa ni pamoja na ya mlinzi, mitihani, na madawati, kuunda baraza dogo la mawaziri linalowajibika na kujenga utaifa. Kila la kheri wanaikulu wapya!