Sijui maisha ni bahati?

ndunajr

Senior Member
Apr 28, 2015
174
191
Maisha kweli yana siri kubwa sana, wakati huu wa Magufuli vilio vingi vimesikika kwa watanzania kwamba maisha ni magumu na pesa imepotea sana, ajira hakuna, vitu vinapanda bei sana na kadhalika na kadhalika.

Sisi wengine kelele hizi zimetupa maswali mengi sana hivi tatizo liko wapi kweli maisha ndo kama hivyo yanavyosemwa katika nyakati hizi za awamu ya tano? lakini kama ndivyo mbona toka napata akili ya ki utu uzima serikali ya Mwinyi wako watu walikuwa na kilio hiki hiki mpaka kwa Mkapa kilio hicho hicho kikwete pia na sasa Magufuli bado.

Ni nini hasa? ndipo nikagundua maisha hayataki kufuata mkumbo inabidi kusimama wewe kama wewe nami nikasimama na kuanza kufikiri sana. Of course nina kazi yangu ya udereva nikasema sitaki kusikia kelele za watu nataka nifanye kitu.

Nikakodi fremu ya duka kwa pesa ya mahangaiko sana; kukopa, kuwa mkarimu kwa mabosi wanakutoa kidogo kihela nikawa nikitumwa kazi yoyote halali sikuwa mbishi;kila kijisenti kwangu ilikuwa ni faida kubwa sana.

Baada ya kupata kafedha ka kukodi frem sikuwa na biashara ya kufanya nikachekwa ndani ya mwezi mzima. Mke wangu akawa anashangaa vipi mbona umechukua frem afu huna biashara?

Baada ya mwezi mmoja nikakopa tena kahela ka kununua mchele kilo 50 mara mbili wa bei tofauti, maharage kilo 25 mara mbili ya bei tofauti (njano na soya) tarehe 01/07/2016 nikafungua kiduka changu nikamwambia mke wangu kaa hapa tuuze mimi nikachukua likizo ya wiki moja tukaendelea

Leo ninavyozungumza kwa kujituma sana na ukarimu mwingi wa kitumwa niliouonyesha kwa watu na kunipa elfu kumi elfu tano nina duka la nafaka limejaa michele, ulezi, ngano nzima, maharagwe, mtama, mahindi,choroko,karanga yani in short duka ni tamu, (si kwamba sitamani bia au kuvaa vizuri natamani sana)

Baada ya muda kidogo wateja wakaanza kusema si uweke na soda...nikahangaika nikapata fridge nikanunua kreti moja la pepsi moja la koka kwa shilingi 1,9400/= tu.

Mzuka ukanipanda nikaongeza kretii tupu na kufikia kumi, nikajiona naweza kufanya kitu kingine nikachukua frem nyingine na kununua kreti 10 za soda aina ya pepsi kwa sababu niliamini ndio talk of the town

Nikaanza kuuza soda jumla muda kidogo kuna kama laki moja ya hisani ikapotea njia nikanunua maji ya jumla katoni kadhaa heee baaadae kidogo hela nyingine hiyo nikaweka na juice katoni 20 Mo Passion na Mo Chungwa baadae kidogo mtoto wa mjini nikatia Azam Embe na Azam Energy duka la vinywaji nalo hilo la jumla.

Kwa hiyo katika serikali ya awamu ya tano hii hii ambayo watu wanaipigia kelele nimefungua maduka mawili na kodi TRA nalipa duka moja mke wangu na jingine mdogo wa mke wangu yani shemeji.

Mungu si athuman bwana, katika kazi yangu ya udereva sikutaka kuhangaika sana kutafuta nikaridhika na hii hii.

Hee siku mara nikapigiwa simu kumbe ukiwa na heshima na ukarimu watu wanakujadili bila wewe kujua, mnamo mwezi wa kumi mwaka huu nikapokea simu ya kuniomba nikawe dereva kwenye shirika moja hivi kisa tu eti walisikia kuna kijana flani atawasaidia kwa sababu ni mchapa kazi.

Mungu anasaidia sana (kwa wanao amini) sijaenda VETA wala NIT lakini nikaitwa kwenye usaili bila kushandanishwa na mtu yoyote na tarehe 01/11/2017 nikaanza kazi jana tarhe 27/11/2017 nimelipwa mshara wangu wa Tsh 913000/= nimepigwa na butwaa kwa sababu ni mara tatu na zaidi ya mshahara wangu wa awali asa hebu niambie maduka yangu yatajaaje!!!.

Tunajifunza nini; tuongee na Mungu, tumuulize maswali Mungu, tukae na nafsi zetu, tupunguze anasa, tuwe na uthubutu, tuwe na heshima na ukarimu mbele za watu, tuache ushabiki wa kisiasa usio na tija.

TUNAWEZA kwa sababu hata raisi awe mzuri vipi hutoletewa pesa nyumbani.

MUNGU AWABARIKI SANA
 
Itabidi ukope tena ununue mchele kilo 50! Huyu jamaa bwana
Ewaaa... nadhani hii ndio ujanja wa kufanikisha maisha katika serikali ya awamu ya tano...

Mungu si Athumani mambo yakishaninyookea nami ntaitwa kwenye intavyuu bila kuapply...
 
Bigup sana mungu akubaliki, mpenda kazi atalipwa na kazi, mpenda papuchu atalipwa na papuchu, mpenda gegedo atalipwa na gegedo yan ni hvyo hvyo mpaka mwisho yan hata bahat utaipata kwenye kile unacho kiendekeza haiwezekan unapenda kazi upate bahati ya papuchu/gegedo wewe bahati zako zipo kwenye papuchu mzee hata usihangaike kwingne, kazana unaweza hata umpate Grace wa Gucci. Ndo mana hata mwizi anaweza apange aibe akifanikiwa atashukuruu "daa ninabahati kila nikiiba sikamatwi" usihofu mzee, halaf kumbuka msemo wa "za mwizi ni 40" hao ni wahenga tu unaweza uishie hata ya kwanza.

PIGA KAZ MKUU, UTATOBOA ZAID YA HAPO. NAKUOMBA TU USIJE UKABADILISHA GIA ANGANI, BAHATI ZITAHAMIA KWENYE GIA MPYA.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom