Sijui lengo lake nini

neema pita

Member
Apr 26, 2012
30
6
Nina miezi 3 tangu nimejifungua.

Mzazi mwenzangu tulipanga kuona baada ya ujauzito akaniambia nitoe nikakataa basi tukarumbana tukawa tumekosana.

Nimekaa nyumbani na ujauzito nyumbani nikaambiwa niende kwa alienipa huo ujauzito nikaenda kwa nguvu japo jamaa hakutaka alinipikea tumekaa.

Simu yake na yangu zinafanana zote ni tecno m3
Kuna siku nikashika yake kwa kutokujua nikadhani yangu.

Alinitukana sana na kuniambia hanipendi ana mtu anaempenda sio mimi nisimng'ang'anie hanitaki kabisa basi nikaamua kuondoka nikamweleza mama ukweli basi akasema huwezi mlazimisha mtu kama hakutaki.

Nilipokaribia kujifungua nikamuomba hela akaninyima.

Sikuchoka nilipojifungua nikamtaarifu nikamtumia na picha ya mtoto hata hongera hakunipa aliulizia jinsia tu nilivyomwambia kakaa kimya.

Sasa kilichonifanya nije kwenu.

Mtoto anamiezi 3 kipindi chote hatukua na mawasiliano cha ajabu wiki sasa ananiambia niende kwake nikamsalimie kaniuliza na mpenda nikajibu ndio.

Anataka niende sijui nia yake nini mama kasema kama anakutaka aje hapa nyumbani sababu alikutelekeza bila msaada wowote umezaa hajaja hata kumuoba mtoto iweje leo akuite uende? nimemwambia aje kakataa siwezi kuja huko kwenu wewe njoo.

Sielewi lengo lake nini je kwa nini akatae kuja nyumbani au anataka kuniumiza tena kwani nilishaanza kuzoea japo nampenda sana sijui nifanye nini? sijui nia yake nini juu yangu
 
Sikiliza maneno ya mzazi wako, huyo ni tapeli. Ataka uende ukampikie na kumfulia....tia akili dada, you can't be fooled twice. neema pita
 
Last edited by a moderator:
Huwezi kumkwepa maisha yako yote, ni mzazi mwenzako. Kama mama alivyosema, aje nyumbani ili ajibu hayo maswali. Kwa nini alikutelekeza? Kwa nini hakutaka kuja kumuona mtoto wake? Na kwa nini Leo aone ndio wakati wa wewe kuonana nae?

Nina wasiwasi jamaa anataka kuosha dushe hana lolote...!
 
Pole sana dada yangu naweza kuhisi ni jinsi gani unaumia.....kimsingi ni kwamba huyo jamaa hakupendi na amekufanya kama nguzo ya kuegemea wakati akiwa hana pa kuegemea lakini kiukweli hana mapenzi na wewe..hata chembe.....kipindi cha ujauzito ndio kipindi ambacho mwanamke anahitaji upendo kwa kiasi kikubwa sana kutoka kwa ampendae......kama aliweza kukukataa wakati wewe unamuhitaji iweje leo akuone wa maana...umebadilika nini...??..au umegeuka mrembo ghafla....?
Isitoshe mpaka alishakutamkia kuwa hakupendi na anaye ampendae kwa dhati bado tena unajiuliza mara mbili kuwa huyo bwana hana mapenzi na wewe...??
Ninachokushauri ni kuwa wakati huu akili yako yote na mawazo yako yote yawe juu ya mwanao...fikra zako ziwe juu ya future ya mwanao mpendwa...huyo mwanao ndio kila kitu kwako kwa sasa....angalia ulipojikwaa na usiyarudie makosa..tena jipange kwa ajili ya maisha yako na ya mwanao kuwa atasoma vipi....achana na huyo mpuuzi hakuwa chaguo lako kutoka kwa Mungu.....maisha bado yanaendelea na lazima yaendelee hata bila ya huyo mpu.uzi asiyejua thamani yako...bado una nafasi ya kuyafurahia maisha.....SONGA MBELE....
 
ndomana mijanaume mingi ikizeeka inakosa msaada kwa watoto wao sababu ya kuwatelekeza
 

hapa unasema umefeli form four na kila unachosoma unafeli sasa tuamini nini

wana JF wenzangu naombeni kuuliza mimi ninadiploma ya journalism je ninaweza nikapata kazi kwenye makampun ya mawasiliano kama airtel, voda, tigo...... na jinsi gani ninaweza kupata naombeni msaada na ushauri pia
wewe dada ni muongo sana hapa unasema una diploma in journalism

hapa unajitambulisha kama lesbian

sasa tutaaminije stori hii kama sio chai kama ajisemeavyo BADILI TABIA ??

 
Last edited by a moderator:

Aisee wewe utakuwa bonge la wiseman, huu ni ushauri muruwa kabisa, ila sasa, hawa akina dada akipenda huwa ni shida sana. Licha ya ushauri wote huu mnaompa, uatakuta anarudia yaleyale!
 

nisamehe tu ila ungekuwa mdogo wangu ningekuzaba kibao ivi mtu hakukujari na mateso yote eti unampenda sana ivi una akiri timamu?? uusiende na kwenu asikanyage. mtoto ataishi kwa uwezo wa mungu
 

Ahhhha i love u honey mabus mengimengi kwako umejua kumuumbua mtu kama Tyta
 
Last edited by a moderator:

Duh! Kumbe akilala akiamka analeta ndoto zake!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…