Sijui anataka kurudi kwani ndiye aliyeniumiza

Sijui anataka kurudi kwani ndiye aliyeniumiza

Shmy

Senior Member
Joined
Aug 3, 2012
Posts
148
Reaction score
55
Tuliachana muda wa miaka miwili. Sasa naona jamaa anataka kurudisha mawasiliano baada ya kusikia nachat sana na rafiki yake wa kiume.

Nikimuuliza mbona hivi anadai nimsamehe anasema ulikuwa utoto. Na anataka kufika kwangu wakati zamani alikuwa hataki kuja anaweka visingizio namkataza anasema basi niende kwake.

Kwa sasa nimemaliza shahada yangu ya pili na ninatafuta kazi. Sasa nipo njia panda au ananipima tu.
 
Moyo wako una Amani Naye? Kama Amani ipo, Tena Amani Ya Mungu Kama Ipo tele Moyoni Mwako.. rudiana naye...lakini si kwa kurupuka endelea kumsoma taratibuu kwa huwezi jua kajirudi kweli au kuna kitu kakiona toka kwako kinamfanya arudi...
 
Ww moyo wako unatakaje?. We nenda tu kampe raha jamaa
 
KWanini usimuulize muhusika kama anakupima au anakufanyaje
 
Mtu anapoomba ushauri co kwamba muhusika anakuwa hana maamuzi ya kufanya . Lakin kuna watu wana experience ya mambo hayo wanaweza kukuongezea maharifa au kukupa tahadhari. Kusoma co kigezo kuweza kumaliza matatizo peke yako. Ndo maana hata kipengele hk katika jamii forum kipo. Mara nyingi moyo unaweza taman kitu bila kujua undan wa mtu. Reference ni muhmu jaman kwa wale wapondaji.
 
Shahada za siku iz bhana. Ukizingatia la kutafta kazi itakuwa poa sana
 
Appuch mbona una-like kila comment inayoshauri huyu dada arudi?? ni wewe muhusika??
halafu jina lako ni kama mtoto mdogo akiambiwa sema 'papuchi' atasema apuch au ukivuruga hizo herufi utapata pappuch!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom