Sijui alipatwa na nini kilichopelekea kujiua!

Duuh ni roho za kipepo hakuna cha afya ya akili wala nini. Huyo aliemfanya akose ajira kwa miaka yote hyo eidha alijisahau au dawa ziliisha nguvu hatimae akapata ajira,kuona hivyo akamtupia jini kujiua likamfanya ajiue.... naandika huku naogopa
Mtu akishaazimia kujiua bhasi ujue hata apate nini bado yale mawazo yatamuwinda na ubaya wa watu wetu wa karibu si waaminifu, mtu anajua akiwaambia madhaifu yake anageuka topic

Kwa case ya jamaa pamoja na life kukaa upande lakini bado kuna vitu ndani yake hakuwa tayari kumuambia mtu ndio maana nafsi yake haikutulia akiamini kifo ni suluhisho bhasi hizo hisia haziwezi kupozwa kwa pesa au kazi, zinahitaji hisia kutoka kwa mtu mwingine ili zipotezwe. Tiba ya akili ni akili na tiba ya hisia ni hisia
 
uintrovert nauchukia, unamfanya mtu mambo mengi unakaa nayo rohoni. ila tumaini bado lipo, usipende kukaa mwenyewe Muda mwingi, penda kuimba, penda kusikiliza mziki wa taratibu usio na midundo, lia pale upatwapo na maswaibu, pia tafuta washauri wa saikolojia.

Mwisho Yesu ambaye ni tumaini letu anasema Philippians 4:6
"Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu" mpe nafasi katika moyo wako na hautajuta.
 
Sio mke tuu, na watoto wawili wadogo,
Hajamuonea huruma mama yake mjane mbichi aliyefiwa na mmewe miaka miwili iliyopita alafu mbaya zaidi yeye ni first born, very sad, kama kweli ni loneliness alikua mbinafsi.
Kama una mke anayeplay part yake Kwa usahihi na familia yenye upendo mawazo ya kujiua yanatoka wap
 
Kukata tamaa huenda alikuwa ana expectation kubwa sana wakati wa kusoma chuo maisha yakamkataa mambo yakaenda tofauti kabisa akalose hope kabisa
 
Back
Top Bottom