Sijawahi ona tabasamu la mpenzi hata siku moja

Sijawahi ona tabasamu la mpenzi hata siku moja

Duh unaish na mnyama au binadamu...nina rafiki yangu ni KOMANDOO tena mnaowaonaga kwenye t.v wakivunja mawe na kupigana na silaha za hatari lakini jamaa akiwa likizo % kubwa tukiwa na washkaji ana furaha anapenda kucheka na washkaji na ni mtu social sana ...sasa komandoo anayetembea usiku usiku maporini huko anatabasamu na kucheka ..sembuse huyo jamaa yako?!
Kifupi hafurahii mahusiano yenu so jipe jibu hapo kwamba ufanye nini
 
Aisee,mbona una madai ya ajabuajabu sana.Unataka achekecheke kama zuzu?
Mapenzi ni furaha.mnapokua wote ..mnanuna nuna tena uhusiano wa miezi hamna tabasamu hhamna, kwani mko polisi au unayeishi nae ni jambazi au nyinyi ni majambazi mnaenda kuua ...hata majambaz nadhani hua yanacheka
 
Achana nae. Huyo atakua na mwanamke mwingine ambae yuko moyoni mwake.

Mnaishi wote au kila mtu anaishi kwake? Kama hamuishi wote basi wewe ni mchepuko wake. Kama mnaishi pamoja basi hakupendi au amekuchoka.
Aiseeee.....[emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Muhimu kwako ni huduma Muhimu kama unazipata tabasamu ni sehemu ndogo ikikosekana haiathiri chochote vumilia tu
What if anakosa furaha, ilhali jamaa anampea huduma zote.... unamshauri afanye nini?
 
unacholilia kwake ni tabasamu tu mkuu ndo unaamua kumuacha ama kuna kingine!!!
Huyu binti amefikia kujiona anaanza kuikosa furaha kwasababu huyo mwanaume wake hajawahi kumpea tabasamu zaidi ya day 1 alipo anza kumtongoza
 
Habari zenu wadau,

Niende kwenye mada nina mpenzi wangu ambae sasa tunaenda takribani miaka miwili na kitu, ninampenda na nimewekeza mapenzi yangu yote kwake na yeye ameonyesha kuwa ananipenda, kifupi tupo kwenye mipango mingi nae.

Tatizo lililopo bwana huyu sijawahi ona tabasamu lake zaidi ya siku ya kwanza tuliokutana na kuanza kunitongoza mpaka leo hii, najaribu kumfurahisha kwa kila aina ya mapenzi ili nione labda ataonyesha kutabasamu na kunionyesha nami kuwa namridhisha kwa nimtendeayo lakini wapi.

Mpaka imefikia sasa napoteza kujiamini na kila nikimuuliza hunijibu kawaida tu hakuna tatizo. Nimewaza sana mimi uamuzi wangu ni wa kuachana nae.

Naombeni ushauri wenu labda kuna yaliwahi kumtokea na akarekebisha.
Mtie kidole atacheka
 
Huyo yuko kama Putin, rais wa Urusi. Yeye muda wote camuna tu. Hao wanaitwa cold face.
Hahaha,Putin sura ya kazi yule yapo yamchukizayo kama vile sura ya nyodo ya ahmed Nijad,na yeye inabidi atafute kimchukizacho.
 
Yani kisa yatoi tabasamu ndio uachane nae? Kweli kusoma kitabu cha wanawake itanichukua maisha yote.

Mtu anakupa unachotaka, anakupenda kama unavyosema, mipango yenu inaenda vizuri, unachotaka nini, tabasamu?

Dah!

unnamed.jpg
 
Pole mwaya..binafsi siwezi mweh..tabasamu lina raha yake jamani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom