Sijamwelewa Waziri Mkuu ujue?

Kabisa Mkuu. Hii ni lugha gongana!
Kusema waendelee na shughuli zao, wakati kule ACCASIA wameambiwa wasiendelee na chochote mpaka wapate agizo jipya kutoka kwa rais..hapa ndio hapaeleweki.
Kusema waendelee na shughuli zao, wakati kule ACCASIA wameambiwa wasiendelee na chochote mpaka wapate agizo jipya kutoka kwa rais..hapa ndio hapaeleweki.
 
Hahaha,
Wajinga sana, Akili za Mchanga kubishana na Lissu? Yaani miaka yote wanaambiwa tunaibiwa wanabisha kwa dharau na Kebehi, eti Leo ndio wanajifanya wanauchungu na nchi yetu!! Shenztyp!!!

Eti Uzalendo!!! Dhahabu tani 7?? Yaani tani saba waibebe kwenye Lori? Hata kama ningekua mimi nisingebeba kwenye Lori hata siku moja!!

Zamani nilikua naamini wanasiasa ni magenious sana, kumbe hamna kitu kabisa, yaani kuna vitu kwa akili ya kawaida kabisa unaona kama ningekua mimi nisingefanya hivi ila wao ndo wanafanya tena MBELE YA MACHO YA DUNIA NZIMA, what a shame!!! Ndio maana hii ngozi nyeusi itaendelea kudharaulika mpaka siku Ulimwengu unafutika,. Sasa tusubiri kuwalipa fidia ya kupoteza zile bilion mbili zao za kila siku, fidia ya kuwachafulia jina na fidia ya kuporomosha hisa zao.

CCM Oyeeeeee

MAGUFULI Oyeeeeeeeq

Makonda Oyeeeeee

cocochanel Oyeeeeee

Babeli Oyeeeee

Troll JF oyeeeeee

Barbarosa Oyeeeeeeee

Simiyu Yetu Oyeeeeeeeee

Mudawote oyeeeeeeee

chinembe Oyeeeeeeee

Lizaboni Oyeeeeeee

MOTOCHINI oyeeeeeee

jingalao Oyeeeeeee

Subirini KARMA iwashughulikie, vita dhidi ya wanyonge hawajawahi kumuacha Mkandamizaji Salama hata siku moja.[/QUOTE
Hahaha, umeua mkuu! Hii itakuws ya kufungia uzi
 
Leo katika kipindi cha bunge cha maswali ya papo kwa hapo amesema kwamba serikali haijawachukulia hatua zozote kampuni yoyote ya madini au mwekezaji kutokana na ripoti ya makinikia.

Kwamba hatua zilizochukuliwa ni za ndani tu haxiwahusu hao wawekezaji. Hivyo wasiwe na wasiwasi na waendelee na shughuli zao kama kawaida. Lengo la serikali ni.kujiridhisha tu kilichopo kwenye makinikia na bado ripoti nyingine inasubiriwa.

Akasema baada ya ripoti hiyo kutoka wstashauriana nini cha kufanya kwa kuwashirikisha wadau wote na kwa haki. Na wala hakutakuwa na tatizo kwani kila kitu kitakwenda vizuri.



Hivyo watu waache kutishana na pia wawekezaji kwenye madini watulie. Jibu hili lilitokana na swali la mbunge wa Tabora mjini aliyetaka kujua kama serikali kwa kuxuia mchanga wa makinikia haioni kwamba inawaogopesha wawekezaji na tunaweza kujikuta tunaingia kwenye mgogoro na nchi wanazotoka wawekezaji hawa hasa endapo ikija kujulikana kwamba kilichosemwa na tume si kweli?

Kiukweli kabisa jibu la Waziri Mkuu limeniacha na kizunguzungu. Ukiacha kwanza kwamba jibu lake lake limeonekana kujaribu kupooza hali ya sintofahamu iliyopo na kwamba kuna uwezekano tume ikawa ilikosea, nimeshangazwa zaidi na aliposema eti hatua zilizochikuliwa ni za ndani tu na makampuni ya madini hayajachukuliwa hatua zozote mpaka sasa na eti waendelee na shughuli zao bila wasiwasi.

Hivi ni kweli WM hakusikia mapendekezo ya Tume ya Rais kwamba Acacia wamekuwa wanatuibia sana? Tena wakashauri makontena ya mchanga yaendelee kushikiliwa mpaka watakapotulipa kodi zetu kwa kile kilichopo kwenye mchanga?

Hakumsikia rais akisema ameyakubali mapendekezo yote ya Tume? Sasa atasemaje eti serikali haijachukulia kampuni yoyote hatua na waendelee tu na shughuli zao kama kawaida?

Je, hajawasikia Acacia wakilalamika kwamba wanapata hasara ya mabilioni kila siku kwa kitendo cha kushikilia mchanga ao muda mrefu?

My take: Nahisi serikali imeshachanganyikiwa kuhusu hili la makinikia ndio maana wanaanza kutoa kauli tata!

Tone ya WM leo na tone ya Magufuli kuhusu hili sakata siku ile ya kukabidhiwa ripoti ni vitu viwili tofauti kabisa.

Naona dalili kwamba somo ambalo limekuwa likitolewa na wadau kuhusu kutokurupuka katika hili limeanza kuwaingia serikali! Kudos kwa serikali kama mmeelewa somo.

Next time mtulize vichwa kwanza kabla ya kukurupuka na maamuzi yanayoweza kuliingiza taifa kwenye hasara kubwa. Tuwape madini, halafu tuwalipe tena fidia ya mabilioni?, No way. Sio kwa kodi zetu. Mngetoa hizo pesa mifukoni mwenu wallah!!

Kama bado kuna mashauriano yarakayoendelea ilikuwaje watimue waziri,wavunje bodi ya TMAA,wapeleke askari kuzunguka migodi?Kuna kitu hapa hakiko sawa kwa sauti ile ya PM nahisi dawa imeingia.
 
Kama bado kuna mashauriano yarakayoendelea ilikuwaje watimue waziri,wavunje bodi ya TMAA,wapeleke askari kuzunguka migodi?Kuna kitu hapa hakiko sawa kwa sauti ile ya PM nahisi dawa imeingia.
Naam, dawa imeingia kunako! Ingawa PM anaonekana ana busara mara 10 zaidi ya bosi wake!
 
Inasemekana wale maaskofu walipangwa kuuliza maswali,na maswali yenyewe mpaka leo hawajajibiwa,haiwezekani itokee coincidence eti wauliza maswali wote wawe maaskofu,

Asiwepo shehe hata mmoja
Huenda report ya pili watakaouliza maswali ni mashehe tuu
 
IMG-20170529-WA0003.jpg
 
Back
Top Bottom