Sijamwelewa Waziri Mkuu ujue?

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Leo katika kipindi cha bunge cha maswali ya papo kwa hapo amesema kwamba serikali haijawachukulia hatua zozote kampuni yoyote ya madini au mwekezaji kutokana na ripoti ya makinikia.

Kwamba hatua zilizochukuliwa ni za ndani tu haxiwahusu hao wawekezaji. Hivyo wasiwe na wasiwasi na waendelee na shughuli zao kama kawaida. Lengo la serikali ni.kujiridhisha tu kilichopo kwenye makinikia na bado ripoti nyingine inasubiriwa.

Akasema baada ya ripoti hiyo kutoka wstashauriana nini cha kufanya kwa kuwashirikisha wadau wote na kwa haki. Na wala hakutakuwa na tatizo kwani kila kitu kitakwenda vizuri.



Hivyo watu waache kutishana na pia wawekezaji kwenye madini watulie. Jibu hili lilitokana na swali la mbunge wa Tabora mjini aliyetaka kujua kama serikali kwa kuxuia mchanga wa makinikia haioni kwamba inawaogopesha wawekezaji na tunaweza kujikuta tunaingia kwenye mgogoro na nchi wanazotoka wawekezaji hawa hasa endapo ikija kujulikana kwamba kilichosemwa na tume si kweli?

Kiukweli kabisa jibu la Waziri Mkuu limeniacha na kizunguzungu. Ukiacha kwanza kwamba jibu lake lake limeonekana kujaribu kupooza hali ya sintofahamu iliyopo na kwamba kuna uwezekano tume ikawa ilikosea, nimeshangazwa zaidi na aliposema eti hatua zilizochikuliwa ni za ndani tu na makampuni ya madini hayajachukuliwa hatua zozote mpaka sasa na eti waendelee na shughuli zao bila wasiwasi.

Hivi ni kweli WM hakusikia mapendekezo ya Tume ya Rais kwamba Acacia wamekuwa wanatuibia sana? Tena wakashauri makontena ya mchanga yaendelee kushikiliwa mpaka watakapotulipa kodi zetu kwa kile kilichopo kwenye mchanga?

Hakumsikia rais akisema ameyakubali mapendekezo yote ya Tume? Sasa atasemaje eti serikali haijachukulia kampuni yoyote hatua na waendelee tu na shughuli zao kama kawaida?

Je, hajawasikia Acacia wakilalamika kwamba wanapata hasara ya mabilioni kila siku kwa kitendo cha kushikilia mchanga ao muda mrefu?

My take: Nahisi serikali imeshachanganyikiwa kuhusu hili la makinikia ndio maana wanaanza kutoa kauli tata!

Tone ya WM leo na tone ya Magufuli kuhusu hili sakata siku ile ya kukabidhiwa ripoti ni vitu viwili tofauti kabisa.

Naona dalili kwamba somo ambalo limekuwa likitolewa na wadau kuhusu kutokurupuka katika hili limeanza kuwaingia serikali! Kudos kwa serikali kama mmeelewa somo.

Next time mtulize vichwa kwanza kabla ya kukurupuka na maamuzi yanayoweza kuliingiza taifa kwenye hasara kubwa. Tuwape madini, halafu tuwalipe tena fidia ya mabilioni?, No way. Sio kwa kodi zetu. Mngetoa hizo pesa mifukoni mwenu wallah!!
 
chama cha kjana na njano kilibug sana kutuletea hil lijamaa, mbwembwe zote zile hamna lolote lilofanyka, pongez kbao toka kwa vjana wa chama kjan na njano, wazee wa dsm n.k leo PM anasema hiv. Aibu tupu miaka 5 itapta iv iv nawaambia
 
chama cha kjana na njano kilibug sana kutuletea hil lijamaa, mbwembwe zote zile hamna lolote lilofanyka, pongez kbao toka kwa vjana wa chama kjan na njano, wazee wa dsm n.k leo PM anasema hiv. Aibu tupu miaka 5 itapta iv iv nawaambia
To be honest, ccm walibugi step big time kutuletea mtu kama huyu! Nikikumbuka slivyoonesha hamaki siku ile ripoti inasomwa yaani rais anakosa utulivu kabisa! Mzuka ulimpanda vibaya mpaka akajikuta anatukana! Huyu sio kabisa!
 
Si n
Unasema watamnyoosha kama vile aikuhusu wewe wapuuzi kweli nyie labda kama nyie siyo watanzania kisa uchama wenu wa kipuuzi kabisa,ingekuwa ni amri yangu ningewafolenisha pale Taifa niwachape viboko nfufjqbveeiqb.
Si ndio maana tunapiga kelele ili serikali ishtuke? Unaonaje kwani? Hatutaki tuingie kwenye hizo gharama. Nimesema serikali ikiendekea kupuuza halsfu tukaja daiwa mafidia, Magu ajiandae kuzitoa mfukoni mwake!
 
Sasa huku mtaani wadanganyika wanavyopiga makelele kama ndege kwenye shamba la mpunga..
Ukiwaambia jamaa kachemka wala hawakusikilizi kwa makelele yao..!!

Tatizo nchi hii watu wengi utumia robo tu ya akili zao....

[HASHTAG]#Akili[/HASHTAG] za [HASHTAG]#Mchanga[/HASHTAG]
 
Kwani wale askari na mkuu wa mkoa kule bulyanhulu na buzwagi walifunga vitu gani mbona nahisi kizungu zungu saiv
 
Back
Top Bottom