Sijamsikia kitambo Makamu wa Rais Philip Mpango. Je, yu wapi?

Sijamsikia kitambo Makamu wa Rais Philip Mpango. Je, yu wapi?

Ataibuka tu na kashfa za samaki au nyama. Safari hii
 
Wadau wa JF hamjamboni nyote?

Leo nimemkumbuka mno mtani sisi wa kanda ya ziwa na pia ni kiongozi wetu nambari 2 kitaifa kwani ni kitambo sijamsikia

Nauliza yu wapi mtani wetu huyu aliyechaguliwa kwa kura nyingi na Wabunge kuanzia March 31,2021?

View attachment 2384812
Wamemfunga breki aache kuropokaropoka juu ya samaki amekalishwa kikao kizito San had akatishia kuacha kazi za umakamu akambiwa ache kuropokaropoka
 
Philip Mpango angeomba tu kupumzika, majuma kadhaa yalopita nilikutana nae kwenye mkutano mfani wa shirika flan pale New York hakika niliona wazi jamaa bado hayuko sawa kuanzia kuzungumza hadi kutembea.

Nafkiri Samia alimteua kwa makusudi akijua fika jamaa hawezi mfunika. Ningekua mimi ni yeye ningepumzika.
"..., ni wazi jamaa bado hayuko sawa kuanzia kuzungumza hadi kutembea."?

Madhara ya UVIKO?

Hapana, kuteuliwa kwa Philip Mpango hakukutokana na hali mbovu aliyokuwa nayo, kwamba hawezi kumfunika mkuu wake.
Naamini kuteuliwa kwake kulitokana na utendaji kazi wake na wasifu aliokuwa nao huko siku za nyuma, na siyo kwa mwonekano mbovu uliomwona nao wewe.
Hata hivyo, sidhani kwamba Samia alikuwa na nafasi muhimu katika uteuzi wake.
 
Hapana,
Angalau akina Shein walikazana na mikasi na wakaonekana kuwa wapo.

Kuna jambo haliko sawa na huyu bwana.
Acha upuuzi,juzi hakuwa Marekani? Kabla ya kwenda America alikuwa Kigali.

Rais Samia akiwa VP ulishamuona na mikasi?
 
Itakuwa yupo mocwari anavizia wauza samaki wanaonunua maji yaliyo oshewa maiti.
 
Wote wako hivyo hata wa marekani nina siku nyingi nimemsikia,lkn Biden kila siku kuna news yake.
 
Aliwahi sapoti Tozo nikaona vijana wanamtolea uvivu toka hapo kakaa kimya kaona isiwe tabu..
 
Serikali iwe inatoa taarifa wakati viongozi wakuu wakiwa likizo, safari mikoani au nje ya nchi n.k Hii inaondoa maswali mengi.

Wakati wa Jakaya Kikwete hata alipokuwa nje kupata matibabu ya tezi dume, watanzania walitaarifiwa kuhusu wapi alipo.

Utamaduni wa ukimya ktk dunia hii ya utandawazi ambapo kila siku tunatupiwa habari kupitia vyanzo lukuki halafu ghafla kimya kingi cha muda kiongozi haonekani lazima maswali yataibuka.


View: https://m.youtube.com/watch?v=Ivse2f6Smsc
 
Serikali iwe inatoa taarifa wakati viongozi wakuu wakiwa likizo, safari mikoani au nje ya nchi n.k Hii inaondoa maswali mengi.

Wakati wa Jakaya Kikwete hata alipokuwa nje kupata matibabu ya tezi dume, watanzania walitaarifiwa kuhusu wapi alipo.

Utamaduni wa ukimya ktk dunia hii ya utandawazi ambapo kila siku tunatupiwa habari kupitia vyanzo lukuki halafu ghafla kimya kingi cha muda kiongozi haonekani lazima maswali yataibuka.


View: https://m.youtube.com/watch?v=Ivse2f6Smsc

Nyie watu vipi, mnamtaka VP wa nini nyie, hayuko Mzena wala nini, yeye yuko ofisini na anachapa kazi
 
Akaunti rasmi ya ofisi ya makamu wa rais posti ya mwisho ni hii ikionesha kwa kina mambo mengi kabla ya kuingia katika ukumbi wa UNGA New York

16 October 2023

MAKALA MAALUM YA ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MH. MPANGO NCHINI MAREKANI

View: https://m.youtube.com/watch?v=-yfiHgf69Mg
Makala haya maalum yanahusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, New York nchini Marekani. Pamoja na mambo mengine alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa yaani UNGA78.
Source : OFISI YA MAKAMU WA RAIS
 
Back
Top Bottom