KWANINI JAJI MKUU ANASEMA HIVI?/MHE. MPANGO NI MAKAMU WA PILI AU NI MAKAMU WA RAIS JMT.?
View: https://m.youtube.com/watch?v=uEiA-G2LogA
Jaji Mkuu wa Tanzania mara kadhaa katika shughuli za kiserikali humtaja makamu wa rais kuwa ni makamu wa pili wa rais.
Wachambuzi wanahoji kauli hizi za mara kwa mara za jaji mkuu na kwa vile ni mmbobezi wa kutafsiri sheria na katiba, wachambuzi wanajiuliza huyu makamu wa kwanza wa rais wa jamhuri ya muungano ni nani ?
Mheshimiwa jaji mkuu amekuwa akisema hayo wakati Mh. Samia Suluhu Hassan akiwa makamu wa rais enzi za Rais John Magufuli na pia wakati huu rais akiwa no Mh. Samia Hassan jaji mkuu anamtaja Dr. Philip Mpango kama makamu wa pili.
Je huyo makama wa kwanza wa rais enzi za John Magufuli ni nani na pia kwa sasa ambapo rais ni Samia Hassan je makamu wa kwanza ni nani? Maana anatajwa yupo lakini hajulikani ni nani.