Sijalipenda hili jina

Sijalipenda hili jina

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,709
Reaction score
830,711
Nimetoka kwenye mihangaiko yangu nikaingia bar moja pande za sinza nipoze koo na kula japo kongolo. Baada ya mhudumu binti mkubwa tu kunihudumia nikamwomba aniitie mtu wa jikoni akapaza sauti akasema 'wee mangi huyu mbaba hapa anakuita'! Amenikera mno kwani kashindwa kutumia jina lingine?
 
hahaha!!.pole weh! may be unaonekana mbaba kama sio basi aliona wallet huyo.,kama unabisha weka picha tuone!
 
Kiongozi kama aliyeitwa hakuonyesha dalili za kukerwa au kukwazwa sioni tatizo, si unajua baa tena pengine anavuma(maarufu) kwa jina hilo

Hapo kwenye mbaba nafikiri amekupa heshima usijali kiongozi piga maji
 
Hai hai umbuje!!
Usichukie,ni ukumbusho kuwa unaelekea saa 12 jioni!!!
 
Nimetoka kwenye mihangaiko yangu nikaingia bar moja pande za sinza nipoze koo na kula japo kongolo. Baada ya mhudumu binti mkubwa tu kunihudumia nikamwomba aniitie mtu wa jikoni akapaza sauti akasema 'wee mangi huyu mbaba hapa anakuita'! Amenikera mno kwani kashindwa kutumia jina lingine?

pole mshana jr nakukumbuka sana kwa fb
 
Last edited by a moderator:
Tatizo hapo nini sasa we sio mbaba kwani? Au tukupeleke kwa "cameroon"
 
Utakua una angalau features mbili tatu za kuitwa mbaba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom