John, umetukana mbwakoko , futa hilo neno. Utatukanwa sana na utachukia. Futa mbwa Koko!Kiukweli nichukue fursa hii kukiri kuwa Tundu Antipas Lisu ni mwanasiasa mpambanaji wa viwango vya dunia.
Alithubutu kwa ujasiri mkubwa kumshauri na kumkosoa Rais Magufuli wakati wa uhai wake bila uwoga.
Hii ni tofauti na wanasiasa wengine wote wa upinzani ambao walimuogopa sana Magufuli akiwemo Zitto Kabwe ambaye aliogopa kutoka bungeni wakati wabunge wote wa upinzani walipotoka kuwaunga mkono CUF walioonyesha hasira zao kwa maalimu Seif kuporwa ushindi ( tuhuma).
Baada ya Magufuli kutwaliwa ndio Zitto kaanza kumsimanga.
Mwingine ni Nape Nnauye mtoto wa mwanajeshi lakini aliingia Ikulu huku analia na leso ya kujifutia puani mkononi akamshika miguu Rais Magufuli amsamehe kwa kosa la kumsengenya kwenye simu.
Maendeleo hayana vyama!