Sijaelewa Tundu Lissu alipata wapi Ujasiri wa kumkosoa Magufuli hadharani akiwa hai. Sasa naona mbwa koko ndio Wanabweka

Hassani

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
370
500
Acha unafiki wewe.
Zitto ndiye aliyeongoza Jahazi la kumkosoa Magufuli kipindi Lissu yuko hospitali.

Zitto ndiye aliyemwambia Magufuli wazi kuwa awe makini maana akizuia uhuru wa watu kusema na kuibana demokrasia, watu wanaweza kutafuta njia ya kumtoa ikiwemo mapinduzi

Zitto ndiye aliyeongoza chambuzi nyingi za kukosoa mwenendo wa kiuchumi wa Magufuli, kumbuka chambuzi za ripoti za CAG

Zitto ndiye aliyeibua hoja ya Trillion 1.5, ishu iliyoiyumbisha sana serikali ya Magufuli

Zitto ndiye aliyeibua taarifa kuwa zaidi ya wananchi 400 wameuawa nadhani ni Kigoma au Kibiti

Zitto alifanya kazi nzuri sana ya kuushika mashati utawala wa Magufuli enzi hizo Lissu yuko hospitali
Uko sahihi kabisa mkuu,zito ni mmoja wa wanasiasa waliyemkosoa Magufuli waziwazi na bila uoga
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
13,162
2,000
Watu wengi wameshaamka ndio maana baada ya kuona box la kura linanajisiwa hawajitokezi tena kupiga kura. Hii idadi ndogo inayojitokeza kwenye vituo vya kura, ni baada ya wananchi kuichoka CCM, ila tume ya uchaguzi na vyombo vya dola vina ushirikiano wa kihalifu kwenye kuchakachua matakwa yao.
Ccm haijaanza jana wala juzi kuiba kura na kila mtu anajua ila bado watu mlikuwa mnaenda kupiga kura kila inapofika uchaguzi, sasa hapo kilichobadilika ni baada watu kuona hata hao mbadala wa ccm nao hawana tofauti na ccm.
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
13,162
2,000
Walimchukia kwa kulazimisha kuwatawala kwa shuruti.
Ccm imewatawala hadi leo na haitaki kuachia madaraka hata huyo Magufuli kapitia humo humo, hao watu wangekuwa na akili basi hasira zao wangezielekeza kwa ccm maana ndio chanzo cha yote ila sio huku ccm damudamu halafu et umejijaza chuki kwa Magufuli.
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
13,162
2,000
Waliokuwa sawa kisaikolojia ni walioagiza ashambuliwe kwa risasi? Yeye ana hasira kwa mwendakuzimu kuagiza ashambuliwe kwa risasi ili kumuua. Sasa ulitaka akae kimya bila kumshambulia aliyedhamiria kumuua?
Hao wawili wanafanana upande huo ni basi tu mmoja alikuwa na power na mwengine hana.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
30,407
2,000
Kiukweli nichukue fursa hii kukiri kuwa Tundu Antipas Lisu ni mwanasiasa mpambanaji wa viwango vya dunia.

Alithubutu kwa ujasiri mkubwa kumshauri na kumkosoa Rais Magufuli wakati wa uhai wake bila uwoga.

Hii ni tofauti na wanasiasa wengine wote wa upinzani ambao walimuogopa sana Magufuli akiwemo Zitto Kabwe ambaye aliogopa kutoka bungeni wakati wabunge wote wa upinzani walipotoka kuwaunga mkono CUF walioonyesha hasira zao kwa maalimu Seif kuporwa ushindi ( tuhuma).

Baada ya Magufuli kutwaliwa ndio Zitto kaanza kumsimanga.

Mwingine ni Nape Nnauye mtoto wa mwanajeshi lakini aliingia Ikulu huku analia na leso ya kujifutia puani mkononi akamshika miguu Rais Magufuli amsamehe kwa kosa la kumsengenya kwenye simu.

Maendeleo hayana vyama!
John, umetukana mbwakoko , futa hilo neno. Utatukanwa sana na utachukia. Futa mbwa Koko!
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,453
2,000
Ccm haijaanza jana wala juzi kuiba kura na kila mtu anajua ila bado watu mlikuwa mnaenda kupiga kura kila inapofika uchaguzi, sasa hapo kilichobadilika ni baada watu kuona hata hao mbadala wa ccm nao hawana tofauti na ccm.

Labda kama unadhani unaongea na mtu asiyejua tofauti ya chaguzi za wizi wa kura wa CCM, kabla ya Magufuli kuwa na rais, na chaguzi za kihayawani baada ya Magufuli kuwa rais. Kilichowafanya watu kuendelea kupiga kura kabla ya Magufuli kuwa ni rais pamoja na wizi wa CCM, bado wapinzani walikuwa wazidi kuongezeka kuongezeka, na trend ilivyokuwa ni kuwa CCM ilikuwa inaenda kukosa 2/3 bungeni ambayo imgewanyima kufanya maamuzi yoyote watakayo hata kama hayana maslahi kwa taifa. Lakini baada ya Magufuli kuwa rais, tulishuhidia changuzi za kikatili, kinyama, ma uhayawani wa wazi. Kibaya zaidi ushenzi huwa ulikuwa unaratibiwa na vyombo vya dola na kupewa baraka na tume isiyo huru ya uchaguzi. Hii ndio sababu ya wananchi kupuuza huo ushenzi uitwao uchaguzi.
 
Tewe

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
976
1,000
Kwahiyo hio barabara haikuwepo kipindi jembe liko Hai???. Haikuwai kutokea kiongozi mkubwa tz kufariki watu wengi wakafurahi mpaka kufanya vipati only ilitokea kwa Magufuli. Umejiuliza ni kwanini
Watu wa kada ipi kama sio wanufaika wa ufisadi?
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
30,407
2,000
Muroto alisema watakaoandamana watakutana na kipigo cha mbwa koko.

Makamanda mkaufyata!

Ni msamiati wa kawaida sana bwashee.
Kwa hiyo mtu akisema na mama yako na baba yako nao walimuogopa kumkosoa Magufuli nao sasa wanamkosoa na hivyo wanabweka kama mbwa Koko? Utakubali hilo? Chunga ulimi/maandishi yako. Lugha uliyotumia siyo stahili yako.

UMEKOSEA SANA TENA SANA
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
51,121
2,000
Kwa hiyo mtu akisema na mama yako na baba yako nao walimuogopa kumkosoa Magufuli nao sasa wanamkosoa na hivyo wanabweka kama mbwa Koko? Utakubali hilo? Chunga ulimi/maandishi yako. Lugha uliyotumia siyo stahili yako.

UMEKOSEA SANA TENA SANA
Mbwa koko ni jina la kiswahili sanifu bwashee.

Hata hospitali ya mifugo mbwa waoga hutambulishwa kama " koko"

Nadhani shida yako ni mimi kumfagilia Lisu ungetamani sana nimfagilie Lema!
 
Larry barrice

Senior Member
Sep 17, 2021
112
250
JPM alikuwa ni Rais bora ambaye kuna sehemu muhimu nchi ilimhitaji sana kuliko mapungufu yake ambayo yalisabishw na lack of controll maeneo fulani....

Binafsi nimefanya research juu ya mapenzi ya watu kwa huyu bwana, ukweli uliowazi JPM anaishi kwenye mioyo ya watu wengi saaana..

Ni leo tu usiku huu nimepita moja ya barabara maeneo fulani ambayo naamini ni feeder load, nikasema mbele za watu serikali inapaswa kujenga hii barabara, majibu ya raia ni "dah si kwa serikali hii angekuwepo jembe JPM angetia lami zote hizi"....hiyo ndio response ya raia

Hata serikali hii ikitaka iwe inaaminiwa basi iachane kabisa na kumsema sema yule jamaa aisee, upende na trust ya watu kwa JPM ilikuwa kubwa sana.....
Tumesema sana kuhusu sehemu ya jpm kwenye mioyo ya watz weng sana ni kubwa mno......watu wa serikali hawajui hili
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
15,235
2,000
Watu hao wengi hawafahamu kilicho nyuma ya pazia. Amemuachia mrithi wake mlima mkubwa wa madeni
Mnadhani kila mtu ni mjinga? Samia alikuwa sayari ya Mars wakati Magufuli anakopa? Uamuzi wa kukopa unatolewa na rais binafsi? Hapana wote walikuwa wanafanya kazi kwa pamoja? Ndiyo yale yale ya ujinga wa kusema utawala uliopita ulikataza wasifanyie mashine za umeme service wakati aliyeyoko kwenye urais ndiye alikuwa masaidizi mkuu wa Magufuli. Ujinga kama huu utaukuta Tanzania pekee.
 
KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,703
2,000
JPM alikuwa akimchukia sana Lissu kwa sababu hakuwa tayari kununuliwa wala hakuziogopa magereza,risasi 38 + watu wasiojulikana

Nitasimama nitatembea nitarudi Tanzania" alisikika Lissu akiwa kitandani hospitalini baada ya kushambuliwa na akina BASHITE
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
13,162
2,000
Labda kama unadhani unaongea na mtu asiyejua tofauti ya chaguzi za wizi wa kura wa CCM, kabla ya Magufuli kuwa na rais, na chaguzi za kihayawani baada ya Magufuli kuwa rais. Kilichowafanya watu kuendelea kupiga kura kabla ya Magufuli kuwa ni rais pamoja na wizi wa CCM, bado wapinzani walikuwa wazidi kuongezeka kuongezeka, na trend ilivyokuwa ni kuwa CCM ilikuwa inaenda kukosa 2/3 bungeni ambayo imgewanyima kufanya maamuzi yoyote watakayo hata kama hayana maslahi kwa taifa. Lakini baada ya Magufuli kuwa rais, tulishuhidia changuzi za kikatili, kinyama, ma uhayawani wa wazi. Kibaya zaidi ushenzi huwa ulikuwa unaratibiwa na vyombo vya dola na kupewa baraka na tume isiyo huru ya uchaguzi. Hii ndio sababu ya wananchi kupuuza huo ushenzi uitwao uchaguzi.
Labda kwa sababu na wewe ulikuwa unaendelea kupiga kura kwenye hizo chaguzi za vituko ila wengine kabla hata ya Magufuli tulishaonaga ni upumbavu kwenda kubariki ccm kuendelea kuwa madarakani halafu baadaye kuja kulalamika sijui uchaguzi haukuwa wa haki.

Kwahiyo kama uliweza kuvumilia hizo chaguzi za huko nyuma na ukawa unaenda kabisa kupanga foleni ili kupiga kura basi kweli mwenyewe unaweza kuona tofauti.
 
Board member

Member
Sep 24, 2021
8
45
Kiukweli nichukue fursa hii kukiri kuwa Tundu Antipas Lisu ni mwanasiasa mpambanaji wa viwango vya dunia.

Alithubutu kwa ujasiri mkubwa kumshauri na kumkosoa Rais Magufuli wakati wa uhai wake bila uwoga.

Hii ni tofauti na wanasiasa wengine wote wa upinzani ambao walimuogopa sana Magufuli akiwemo Zitto Kabwe ambaye aliogopa kutoka bungeni wakati wabunge wote wa upinzani walipotoka kuwaunga mkono CUF walioonyesha hasira zao kwa maalimu Seif kuporwa ushindi ( tuhuma).

Baada ya Magufuli kutwaliwa ndio Zitto kaanza kumsimanga.

Mwingine ni Nape Nnauye mtoto wa mwanajeshi lakini aliingia Ikulu huku analia na leso ya kujifutia puani mkononi akamshika miguu Rais Magufuli amsamehe kwa kosa la kumsengenya kwenye simu.

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu Tundu Lissu sio mwanasiasa kiasili Bali Lissu ni mwanaharakati aliyeingia kwenye siasa.
Hulka za Tundu Lissu ni za kiharakati. Nimefatilia historia yake tangu akiwa shule, jkt (kwa mujibu wa sheria) na hata akiwa kwenye chama cha wanasheria watetezi wa mazingira. Jamaa sio mwanasiasa naturally.
Mara nyingi wanaharakati sio watu wa kulegeza kamba au kurudi nyuma kwa wanayoyapigania bila kujali hatari zinazoweka kuwafika, tofauti na wanasiasa ambao kwao mapatano na maridhiano miongoni mwao ni Jambo la kawaida.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,453
2,000
Labda kwa sababu na wewe ulikuwa unaendelea kupiga kura kwenye hizo chaguzi za vituko ila wengine kabla hata ya Magufuli tulishaonaga ni upumbavu kwenda kubariki ccm kuendelea kuwa madarakani halafu baadaye kuja kulalamika sijui uchaguzi haukuwa wa haki.

Kwahiyo kama uliweza kuvumilia hizo chaguzi za huko nyuma na ukawa unaenda kabisa kupanga foleni ili kupiga kura basi kweli mwenyewe unaweza kuona tofauti.

Kuona tofauti sio lazima uwe ulikuwa unaenda kupiga kura, maana ni kitu kilikuwa kinaonyeshwa kwenye TV, na kutangazwa na media nyingine pia. Kwani ukiona wanafunzi wanaenda shuleni ni lazima na ww uwe mwanafunzi? Au umeishiwa hoja nini boss?
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
13,162
2,000
Kuona tofauti sio lazima uwe ulikuwa unaenda kupiga kura, maana ni kitu kilikuwa kinaonyeshwa kwenye TV, na kutangazwa na media nyingine pia. Kwani ukiona wanafunzi wanaenda shuleni ni lazima na ww uwe mwanafunzi? Au umeishiwa hoja nini boss?
Umezungumzia issue ya watu kupungua kwa sasa kwenda kupiga kura na ndio nakwambia kwamba sie wengine toka zamani tuliona hakuna uchaguzi ni ujinga ujinga tu ila nyie wenzetu bado mlikuwa mnaona kuna uchaguzi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom