Sijaelewa Tundu Lissu alipata wapi Ujasiri wa kumkosoa Magufuli hadharani akiwa hai. Sasa naona mbwa koko ndio Wanabweka

Kiukweli nichukue fursa hii kukiri kuwa Tundu Antipas Lisu ni mwanasiasa mpambanaji wa viwango vya dunia.

Alithubutu kwa ujasiri mkubwa kumshauri na kumkosoa Rais Magufuli wakati wa uhai wake bila uwoga.

Hii ni tofauti na wanasiasa wengine wote wa upinzani ambao walimuogopa sana Magufuli akiwemo Zitto Kabwe ambaye aliogopa kutoka bungeni wakati wabunge wote wa upinzani walipotoka kuwaunga mkono CUF walioonyesha hasira zao kwa maalimu Seif kuporwa ushindi ( tuhuma).

Baada ya Magufuli kutwaliwa ndio Zitto kaanza kumsimanga.

Mwingine ni Nape Nnauye mtoto wa mwanajeshi lakini aliingia Ikulu huku analia na leso ya kujifutia puani mkononi akamshika miguu Rais Magufuli amsamehe kwa kosa la kumsengenya kwenye simu.

Maendeleo hayana vyama!
John, umetukana mbwakoko , futa hilo neno. Utatukanwa sana na utachukia. Futa mbwa Koko!
 
Ccm haijaanza jana wala juzi kuiba kura na kila mtu anajua ila bado watu mlikuwa mnaenda kupiga kura kila inapofika uchaguzi, sasa hapo kilichobadilika ni baada watu kuona hata hao mbadala wa ccm nao hawana tofauti na ccm.

Labda kama unadhani unaongea na mtu asiyejua tofauti ya chaguzi za wizi wa kura wa CCM, kabla ya Magufuli kuwa na rais, na chaguzi za kihayawani baada ya Magufuli kuwa rais. Kilichowafanya watu kuendelea kupiga kura kabla ya Magufuli kuwa ni rais pamoja na wizi wa CCM, bado wapinzani walikuwa wazidi kuongezeka kuongezeka, na trend ilivyokuwa ni kuwa CCM ilikuwa inaenda kukosa 2/3 bungeni ambayo imgewanyima kufanya maamuzi yoyote watakayo hata kama hayana maslahi kwa taifa. Lakini baada ya Magufuli kuwa rais, tulishuhidia changuzi za kikatili, kinyama, ma uhayawani wa wazi. Kibaya zaidi ushenzi huwa ulikuwa unaratibiwa na vyombo vya dola na kupewa baraka na tume isiyo huru ya uchaguzi. Hii ndio sababu ya wananchi kupuuza huo ushenzi uitwao uchaguzi.
 
Kwahiyo hio barabara haikuwepo kipindi jembe liko Hai???. Haikuwai kutokea kiongozi mkubwa tz kufariki watu wengi wakafurahi mpaka kufanya vipati only ilitokea kwa Magufuli. Umejiuliza ni kwanini
Watu wa kada ipi kama sio wanufaika wa ufisadi?
 
John, umetukana mbwakoko , futa hilo neno. Utatukanwa sana na utachukia. Futa mbwa Koko!
Muroto alisema watakaoandamana watakutana na kipigo cha mbwa koko.

Makamanda mkaufyata!

Ni msamiati wa kawaida sana bwashee.
 
JPM alikuwa ni Rais bora ambaye kuna sehemu muhimu nchi ilimhitaji sana kuliko mapungufu yake ambayo yalisabishw na lack of controll maeneo fulani....

Binafsi nimefanya research juu ya mapenzi ya watu kwa huyu bwana, ukweli uliowazi JPM anaishi kwenye mioyo ya watu wengi saaana..

Ni leo tu usiku huu nimepita moja ya barabara maeneo fulani ambayo naamini ni feeder load, nikasema mbele za watu serikali inapaswa kujenga hii barabara, majibu ya raia ni "dah si kwa serikali hii angekuwepo jembe JPM angetia lami zote hizi"....hiyo ndio response ya raia

Hata serikali hii ikitaka iwe inaaminiwa basi iachane kabisa na kumsema sema yule jamaa aisee, upende na trust ya watu kwa JPM ilikuwa kubwa sana.....
Tumesema sana kuhusu sehemu ya jpm kwenye mioyo ya watz weng sana ni kubwa mno......watu wa serikali hawajui hili
 
Watu hao wengi hawafahamu kilicho nyuma ya pazia. Amemuachia mrithi wake mlima mkubwa wa madeni
Mnadhani kila mtu ni mjinga? Samia alikuwa sayari ya Mars wakati Magufuli anakopa? Uamuzi wa kukopa unatolewa na rais binafsi? Hapana wote walikuwa wanafanya kazi kwa pamoja? Ndiyo yale yale ya ujinga wa kusema utawala uliopita ulikataza wasifanyie mashine za umeme service wakati aliyeyoko kwenye urais ndiye alikuwa masaidizi mkuu wa Magufuli. Ujinga kama huu utaukuta Tanzania pekee.
 
JPM alikuwa akimchukia sana Lissu kwa sababu hakuwa tayari kununuliwa wala hakuziogopa magereza,risasi 38 + watu wasiojulikana

Nitasimama nitatembea nitarudi Tanzania" alisikika Lissu akiwa kitandani hospitalini baada ya kushambuliwa na akina BASHITE
 
Labda kama unadhani unaongea na mtu asiyejua tofauti ya chaguzi za wizi wa kura wa CCM, kabla ya Magufuli kuwa na rais, na chaguzi za kihayawani baada ya Magufuli kuwa rais. Kilichowafanya watu kuendelea kupiga kura kabla ya Magufuli kuwa ni rais pamoja na wizi wa CCM, bado wapinzani walikuwa wazidi kuongezeka kuongezeka, na trend ilivyokuwa ni kuwa CCM ilikuwa inaenda kukosa 2/3 bungeni ambayo imgewanyima kufanya maamuzi yoyote watakayo hata kama hayana maslahi kwa taifa. Lakini baada ya Magufuli kuwa rais, tulishuhidia changuzi za kikatili, kinyama, ma uhayawani wa wazi. Kibaya zaidi ushenzi huwa ulikuwa unaratibiwa na vyombo vya dola na kupewa baraka na tume isiyo huru ya uchaguzi. Hii ndio sababu ya wananchi kupuuza huo ushenzi uitwao uchaguzi.
Labda kwa sababu na wewe ulikuwa unaendelea kupiga kura kwenye hizo chaguzi za vituko ila wengine kabla hata ya Magufuli tulishaonaga ni upumbavu kwenda kubariki ccm kuendelea kuwa madarakani halafu baadaye kuja kulalamika sijui uchaguzi haukuwa wa haki.

Kwahiyo kama uliweza kuvumilia hizo chaguzi za huko nyuma na ukawa unaenda kabisa kupanga foleni ili kupiga kura basi kweli mwenyewe unaweza kuona tofauti.
 
Kiukweli nichukue fursa hii kukiri kuwa Tundu Antipas Lisu ni mwanasiasa mpambanaji wa viwango vya dunia.

Alithubutu kwa ujasiri mkubwa kumshauri na kumkosoa Rais Magufuli wakati wa uhai wake bila uwoga.

Hii ni tofauti na wanasiasa wengine wote wa upinzani ambao walimuogopa sana Magufuli akiwemo Zitto Kabwe ambaye aliogopa kutoka bungeni wakati wabunge wote wa upinzani walipotoka kuwaunga mkono CUF walioonyesha hasira zao kwa maalimu Seif kuporwa ushindi ( tuhuma).

Baada ya Magufuli kutwaliwa ndio Zitto kaanza kumsimanga.

Mwingine ni Nape Nnauye mtoto wa mwanajeshi lakini aliingia Ikulu huku analia na leso ya kujifutia puani mkononi akamshika miguu Rais Magufuli amsamehe kwa kosa la kumsengenya kwenye simu.

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu Tundu Lissu sio mwanasiasa kiasili Bali Lissu ni mwanaharakati aliyeingia kwenye siasa.
Hulka za Tundu Lissu ni za kiharakati. Nimefatilia historia yake tangu akiwa shule, jkt (kwa mujibu wa sheria) na hata akiwa kwenye chama cha wanasheria watetezi wa mazingira. Jamaa sio mwanasiasa naturally.
Mara nyingi wanaharakati sio watu wa kulegeza kamba au kurudi nyuma kwa wanayoyapigania bila kujali hatari zinazoweka kuwafika, tofauti na wanasiasa ambao kwao mapatano na maridhiano miongoni mwao ni Jambo la kawaida.
 
Labda kwa sababu na wewe ulikuwa unaendelea kupiga kura kwenye hizo chaguzi za vituko ila wengine kabla hata ya Magufuli tulishaonaga ni upumbavu kwenda kubariki ccm kuendelea kuwa madarakani halafu baadaye kuja kulalamika sijui uchaguzi haukuwa wa haki.

Kwahiyo kama uliweza kuvumilia hizo chaguzi za huko nyuma na ukawa unaenda kabisa kupanga foleni ili kupiga kura basi kweli mwenyewe unaweza kuona tofauti.

Kuona tofauti sio lazima uwe ulikuwa unaenda kupiga kura, maana ni kitu kilikuwa kinaonyeshwa kwenye TV, na kutangazwa na media nyingine pia. Kwani ukiona wanafunzi wanaenda shuleni ni lazima na ww uwe mwanafunzi? Au umeishiwa hoja nini boss?
 
Umezungumzia issue ya watu kupungua kwa sasa kwenda kupiga kura na ndio nakwambia kwamba sie wengine toka zamani tuliona hakuna uchaguzi ni ujinga ujinga tu ila nyie wenzetu bado mlikuwa mnaona kuna uchaguzi.
 
Haukuwa bora kwa 100%, lakini ulikuwa wa kuridhisha, sio sawa na kipindi cha mwendakuzimu. Wakati huo hata idadi ya watu ilikuwa kubwa.
ezungumzia issue ya watu kupungua kwa sasa kwenda kupiga kura na ndio nakwambia kwamba sie wengine toka zamani tuliona hakuna uchaguzi ni ujinga ujinga tu ila nyie wenzetu bado mlikuwa mnaona kuna uchaguzi.
 
Nimesema mara nyingi kwamba ni Tundu Antipas Lissu peke yake aliyekuwa na uwezo wa kumkosoa Rais Magufuli akiwa madarakani kwa wale wa kambi ya upinzani.

Na Mwanaccm aliyekuwa na uwezo wa kumweleza ukweli Rais Magufuli alikuwa ni Benard Kamilius Membe.

RIP Magufuli!
 
Zitto ndiye aliyetufunulia kuwa kuna Upigaji wa Trillion 1.5

Na ndiye aliyetufunulia kuwa kuna Mauji ya raia zaidi ya 400 huko Kibiti

Kwa hiyo tulia Zitto atumie uhuru wake wa maoni, devide and conquer kuwagawa wapinzani haitofanya kazi.
 
Back
Top Bottom