jmchimbadhahabu
JF-Expert Member
- Sep 26, 2014
- 218
- 106
Nimejaribu kufuatilia kwa kina taarifa za kamati zote mbili za uchunhuzi wa mchanga wa madini yanayosafirishwa kwenda nje na kampuni ya ACACIA, Binafsi ninaona kama zina ukweli lakini napata shida sana pale ninapomsikiliza Mh.Tundu Lissu akipinga vikali taarifa hizo kwamba zimekuzwa mno na kwamba kiwango cha madini kilichotajwa kupatikana humo SI KWELI!
NO RESEARCH,NO RIGHT TO SPEAK;
Ninaomba nithibitishe kuwa kiwango cha madini(dhahabu tu) cha wastani wa kilo 28-47 katika kila kontena ni KWELI!
Nimekaa kwa muda mrefu sana katika kijiji cha KAKOLA ambacho kipo pembezoni tu mwa mgodi wa Bulyanhulu (1.5km),enzi za miaka ya 2005-2008 kuna deal zilizokuwa zikifanyika kati ya madereva waliokuwa wakisafirisha mchanga kwenye makontena na baadhi ya wakazi wa maeneo hayo ili kupata mchanga huo kwa njia za panya. Kiukweli watu walineemeka sana!
Baada ya kupata mkanganyiko qa taarifa za Mruma na msimamo wa Lissu ilinibidi nifanye UTAFITI mdogo ili kupata walau kujua kuwa ni nani MKWELI?
Ilinibidi nianze kuwatafta baadhi ya watu ambao walikua wanaupata mchanga huo na kuuprocess kwa njia za kienyeji kabisa.
Nilibahatika kuonana na vijana kama watano kwa muda tofauti tofauti amabao walikua wanashiriki na swali la msingi niliokua nawauliza ni JE KATIKA KILA MFUKO WA KILO 50 MLIPATA KIASI GANI CHA DHAHABU?
Majibu yao yalionekana kufanana sana ambapo walidai katika kila mfuko wa kilo 50 walipata wastani wa GRAMS 60-200 ya dhahabu.
Baada ya kujua hivyo ilinibidi kukokotoa ili nijue kontena zima lenye TANI 20 litatoa kiasi gano cha dhahabu?
Kwa kutumia wastani wa chini kabisa nilipata kila kontena GRAMS 24000 ambazo ni sawa na KILO 24, Ikbukwe kuwa hii ni local processing!
Sasa nikijaribu kilinganisha taarifa za Prof Mruma ambapo yeye anasema katika kila kontena la tani 20 lina wastani wa kilo 28-47 tofauti na taarifa za ACACIA zilizodai kuwa kila kontena lina wastani wa kil 3-5 ya dhahabu!
Mpaka hapo nashindwa kuelewa kwa nini baadhi ya viongozi kama Tundu Lissu anapinga taarifa za tume hizo