Siipendi CHADEMA

Siipendi CHADEMA

Ni mpela mpela tu hadi munywe sumu wote msioipenda chadema
 
Haya ndio matokeo ya kuchanganya kilevi cha kiroba na safari ya moto

Mkuu Mingoi vipi tena.!?? tukiipenda CHADEMA mnatuponda, tumeamua kuichukia tena mnaponda.. nipe ushauri tufanye nini sasa...
 
Last edited by a moderator:
CHADEMA haifai, imewafukuza uanachama watu muhimu MTEla na Juliana ambao kwenye chama chetu ndo wamekuwa tegemeo kuliko waliokuwepo ndani ya chama kabla...
 
Last edited by a moderator:
Narudia tena SIIPENDI CHADEMA na sitakuja kuipenda chadema kama haitajirekebisha.
Nasema hivyo kutokana na sababu zifuatazo.

1. Chadema imekua inaongoza nchi kinyume na taratibu. Tunajua kwamba kwenye uchaguzi mkuu uliopita CCM "ilishinda" uchaguzi huo na kua na "haki" ya kuongoza serikali na vyombo vyote vya usalama.

Lakini kwa masikitiko makubwa CHADEMA wamejitwalia jukumu hilo bila kufuata sheria na taratibu za nchi hii.

Mfano ni pale chadema inapotumia polisi kuwadhuru wananchi na kuwapiga mabomu wananchi kwa kutumia polisi.

2. Chadema kutumia mabavu kuliongoza BUNGE ambapo kisheria ilibidi bunge liongozwe na CCM yenye wabunge wengi, speaker,naibu speaker na wenyeviti wa bunge kutoka CCM.

Hii inajidhihirisha pale ambapo CHADEMA wamekua kimbelembele kutetea maslahi ya wananchi wakati hii kazi ilibidi ifanywe na CCM yenye wabunge wengi+serikali. Huu ni uporaji wa haki ya msingi unaofanywa na chadema kwa wabunge wa ccm.

3. Chadema kwa makusudi kabisa imekua ikiwachonganisha wananchi na serikali yao tukufu ya CCM.
Kitendo cha chadema kufichua maovu ya CCM na kuyaweka wazi kwa wananchi ni uchonganishi mkubwa na unawafanya wananchi kutoipenda serikali yao "halali" iliyopo madarakani.
Mfano mzuri ni list of shame, KAGODA, MEREMETA, DEEP GREEN e.t.c

4. Kitendo kiovu kinachofanywa na chadema kuilazimisha CCM kuacha sera zake na kutekeleza sera mbaya za chadema ni kitendo ambacho hakivumiliki na kinafaa kupingwa na wananchi wote. Wanancchi tumekiamini chama chetu tukufu ccm na tukakipa "kula" za kutosha ili kiingie madarakani na kutekeleza sera zake ilizokua inazinadi majukwaani. Matokeo yake chadema imefanya hila na michezo michafu ya kisiasa na kuilazimisha ccm kutekeleza sera za chadema.

5. Chadema imeiweka nchi rehani kwa kulazimisha USALAMA WA TAIFA kuripoti kwake badala ya kuripoti kwa serikali tukufu ya CCM.
Huu ni uhaini na wapenda haki wote inabidi tupaze sauti kukemea hili suala.
Haiwezekani wanausalama watiifu wafanye mauaji yanayofuata sheria halafu wale wanausalama wasiofuata maadili wakapeleka taarifa chadema. Hii sio sawa kabisa, kunaiweka nchi yetu kwenye hatari kubwa sana.

Naomba niishie hapa ila natoa rai kwa watu wote wenye uzalendo na nchi hii kuipiga vita CHADEMA kwa nguvu zote.

HIvi ndiyo CDM mmejipanga kuendeleza propaganda kwa wananchi ili nchini isitawalike? Eti CHADEMA wanatumia Polisi kuuwa wananchi? Wanausalama watiifu wanaua watu kwa kufuata sheria halali na wale wasiowatiifu kupeleka taarifa kwa chadema? CHADEMA wanatetea maslahi ya wananchi gani wakati wao ndo wako mstari wa mbele kwa kuwajenga hofu ili washiriki shuguli za maendeleo. Hata mjinga anajua kabisa unachotaka kupotosha hapa mkuu, hayo yote uliyoyabainjsha hapana shaka kabisa yanafanywa na CHADEMa Kwa tamaa zao za madaraka, mipango yao ya kutaka kuwafurahisha wafadhili wao na wala usihusishe serikali na vyombo vyake vya ulinzi, Haiwezekani mabomu yanalipuka leo , hata miili haijazikwa tayari wameshapanda majukwaani na kuomba huruma ya wanachi, huu ni mpango endelefu ambao CDM wamepanga kuutumia, bahati mbaya wananchi wameshawashtukia
 
Mkuu Mingoi vipi tena.!?? tukiipenda CHADEMA mnatuponda, tumeamua kuichukia tena mnaponda.. nipe ushauri tufanye nini sasa...
Mleta uzi ni mnafiki alichokiandika ni madongo kwa chama tawala.

 
Kafie porini kwanza kura yako ni 1/15,000,000 ambayo ni sawa na 0.0000015 kima hesabu ni sawa na zero
 
Kazi zenu mlizonazo chadema zinatosha ni mandamani,vurugu,tindikali nk mkiongeza zingine mnajiumiza wenyewe.
 
Back
Top Bottom