Siioni tofauti ya Tundu Lissu na Shekh Ilunga Hassan Kapungu, TEC na BAKWATA wanamtumikia nani?

Mpangawangu

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
887
965
"Miaka Hamsini ya uhuru,watu mbalimbali wamekuwa wakikosoa namna muungano wetu ulivyokuwa na mapungufu mengi ya kisheria na kikatiba.

Lkn kwa bahati mbaya kila aliekuwa akihoji uhalali wa muungano alikwenda jela na hara kupoteza maisha yake"Tundu lisu asema.

Haya maneno si ya kwanza kusemwa hapo walipo yasema yalinasibishwa na udini.Shekh Ilunga Hassan Kapungu,na Mashekh wa uamsho walipo toa ufafanuzi juu ya udhaifu wa muungano na kudai kuwa muungano uliundwa kwa malengo maalum ,watu waliwaita majina mabaya na wengine kufikia kuwaita magaidi.

Serikali ikafika mbali,na kuwaweka kifungini bila kuwasomea mashtaka yao,kila walioomba kupelekwa mahakamani ili wakajitetee hawakupewa fursa hiyo.Mwisho tukaambiwa eti wamefutiwa mashtaka kwa sababu kesi yao haina msingi.

Baadae kule Mwanza nako tukasikia eti Ameshtakiwa kwa uchochezi,lkn kimsingi kosa la Ilunga lilikuwa kusema ukweli juu ya dhulma za muungano.

Leo walioziea kuishi kwa unafiki na kubambikiziana kesi ili kuwanyamanzisha wadai haki,leo wanaumbuliwa kwa hoja zile zile za Shekh Ilunga na Mashekh wa jumuia ya uamsho,Tundu Lissu,Ismali Jussa na Freeman Mbowe wamegingelea misumari ya motto kwenye utosi wa watawala,Ilunga alipo hoji hati ya Muungano ipo wapi aliitwa. Mchochezi ili wapenda dhulma wapate uhalali wa kumshughurikia.

Leo Lissu kahoji uhalali wa kisheria na kikatiba wa muungano na kudai kuwa,bila kuiona hati muungano utakuwa umekisa uhalali wa kisheria wa kujadiliwa na hivyo utakuwa haupo.

Watawala wamelegea na kuahidi siku mbili kuwa hati italetwa bungeni,ili waione nakala halisi (certified copy) na kujiridhisha maeneo tuliyoungana.

Wasira kakiri kuileta baada ya kichapo cha hoja nzito zilizokosa majibu.

Namuona Lissu akiwa sawa na Ilunga katika mitazamo yao juu ya muungano,lkn Ilunga aliitwa gaidi na leo Lissu ni shujaa.(umejifunza nini).

Niwakumbushe nyuma kidogo watanzania wenzangu,watawala wote duniani wanapenda sana kuwagawa watu wao ili kuwatawala kirahisi kama alivyowahi kusema mtaalamu Carl Max, Tunagawanywa kwa dini zetu,makabila yetu,ili tuendelee kutawaliwa.

Mbaya zaidi,anapopata matatizo Mtu wa dini flani,watu wa dini nyingine hushangilia na kupongeza uovu aliofanyiwa.

Wakati south Africa,wajipambana na Makaburu,Askofu Desmond Tuttu aliamua kuungana na weusi wenzake waliokuwa wakiteswa na Makaburu ndani ya nchi yao.

Maaskofu wenzake walimwita majina mabaya kwakuwa walikuwa wakitumiwa na Makaburu kuwakatisha tamaa waafrika wenzao,walimzodoa sana Dismond Tuttu lkn baadae akaibuka shujaa na sasa ni miongoni mwa waafrika wacheche waliotunukiwa tuzo ya NOBEL.

Waliombedha Ilunga leo watamkubali,na kama ulimbedha kwa kufuata mkumbo sasa niwakati wa kuzifuatilia CD zake,Tazama CD ya "Zijue dhulma za muungano" utaukubali ujumbe uliosheheni ushahidi ambao Leo Tundu Lissu Kautumia kuwanyosha ccm mpaka wakakubali kuleta hati ya muungano.

Uongo hupanda ghorofa kwa lift,lkn ukweli hupanda ngazi kwa ngazi.Cardinary pengo na Bakwata hawawezi tena kuokoa jahazi kama ilivyo kawaida yao kutumiwa na watawal,tumeshazijua hila zao,na sasa ndege kisha toka tunduni.
 
Mkuu nimekusoma na nimekukubali kwa takriban mangi mno ulosema!

Waongeze dose hawa vilaza/misukule ya Nyerere....tartib tu wataibuka toka kwenye comma yao nzito mno!? Daah!

Ahsanta sana.
 
Ujue wakati ni mwamuzo,enzi za ilunga hazikuwa za ukweli na uwazi leo chadema imeleta ukweli na uwazi.na ni wakati wa ukombozi kila anayethubutu ataitwa Shujaa.it is the matter of time.
 
Mi nafikiri kila kitu kina wakati wake.kama baba yako alibambikwa mimba na mama yako na baadae ukashtuka si baba yako unahitaji kutumia busara huwezi kumtusi mama yako au huyo mzee ila mama akishafariki unaweza kudai chako na kusepa kwa mdingi halali.
 
Ilunga hakuhamasisha kuchomwa makanisa? Hakuhamasishe kuua maaskofu?
Unaweza kufanya harakati ila za dini dhidi ya dini ni uchochezi na hatari sana.
Kama huamini hili rejea Seleka na antBalaka wa CRA
 
Ilunga ni gaidi tena usimlinganishe na Mwalimu wa Maprofessor Le profeseri incharge in Tanzania Mh Tundu Antipasi Lissu.
 
mkuu ungelisaidia jamvi kwa kuweka japo cd audio au video copy moja ya sheikh Ilunga, pia usimsahau na Sheikh ponda,asante mkuu.
 
umenena vyema sana. Haki sikuzote hudhihiri na batil hujitenga hatakama itachukua muda.

Tunapaswa kujifunza katika hili
 
Ilunga hakuhamasisha kuchomwa makanisa? Hakuhamasishe kuua maaskofu?
Unaweza kufanya harakati ila za dini dhidi ya dini ni uchochezi na hatari sana.
Kama huamini hili rejea Seleka na antBalaka wa CRA
Kumlinganisha Tundu na Ilunga ni sawa na kulinganisha usingizi na kifo!
 
Tundu Lisu ni SHETANI MKUU WA HAPA DUNIANI. TUTAFUNGA NA KUOMBA ILI ISRAEL AMCHUKUE MAPEMAAAA.
hapo unatutangazia kwamba Kikwete kawatuma mmumnyofoe kucha kama mulivyowafanya wengine mwambieni atakufa na kuzikwa akiwa amekaa
 
Hata Tundu Lissu mkamuita Osama bado alichosema ni Haki na ukweli uliopaswa kusemwa kitambo. Tuba dislike na kuukubali ukweli
 
Mpangawangu,

..wako watu pia hawakubaliani na hoja za Mch.Mtikila kwasababu ya udini.

..au wengine ambao wanampinga Dr.Slaa kwasababu tu wametofautiana naye kidini.

..kwa upande wangu nadhani Mashekhe/Wachungaji/Mapadre waji-confine kuwatumikia wananchi kiroho.

..pia Wachungaji/Mapadre/Mashekhe waache "kuchokonoa" au kujifanya wajuvi wa imani za watu wengine.

..ikiwa kuna Shekhe/Mchungaji/Padri analazimika kujihusisha na active politics basi ni vizuri akavaa "gwanda", "gamba" , etc etc,kwa maana nyingine ni bora akajiunga na chama cha siasa.

cc gombesugu, THE BIG SHOW
 
Last edited by a moderator:
kama leo Lisu anaongea kama llunga na Uamsho kwa nini yeye na chama chake hawakusema chochote juu ya mateso wayapatayo viongozi hao
 
Mpangawangu,

..wako watu pia hawakubaliani na hoja za Mch.Mtikila kwasababu ya udini.

..au wengine ambao wanampinga Dr.Slaa kwasababu tu wametofautiana naye kidini.

..kwa upande wangu nadhani Mashekhe/Wachungaji/Mapadre waji-confine kuwatumikia wananchi kiroho.

..pia Wachungaji/Mapadre/Mashekhe waache "kuchokonoa" au kujifanya wajuvi wa imani za watu wengine.

..ikiwa kuna Shekhe/Mchungaji/Padri analazimika kujihusisha na active politics basi ni vizuri akavaa "gwanda", "gamba" , etc etc,kwa maana nyingine ni bora akajiunga na chama cha siasa.

cc gombesugu, THE BIG SHOW

Sawa tuh

Me naona umeongea vema nakuunga mkono mkuu joka kuu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom