Sigara na bia

Sigara na bia

streat Anthem

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
395
Reaction score
476
Moshi unapanda juu,kifua kinawonder tuu
Kukohoa na kubanja tu makohozi na kuugua flu
Ila bado sijasanda tu mpaka kifua kikuu kinibariki sanda tu

Nashindana na mshindani niliye mpangisha ndani
Kodi nalipa mwenye nyumba na mpangaji ana kisirani
Kodi ikiisha ananibabaisha kwa majirani
Ili nilipie pango na mwenyewe aishi ndani

Siwezi sema ni nini kilichonisababisha mimi
Kuwapangisha bia na fegi waishi kwa Mimi
Bila hata discipline wanaleta ubebari na umwinyi
Umeme na maji vikikata kodi ninakatwa mimi

Kuwakaribisha mara moja wanafanya Mara zote
Wanafanya majanga mpaka majirani wananipaka matope
Wananiganda kama kope wanasema kama maji yakiisha na umeme nenda kaibe au ukaokote

Nilijaribu kuwafukuza hawakutoka kumbe sikufanya nilijaribu
Waliponitishia kuunguza nyumba nilipoogopa ndo nikaharibu
Sasa wametawala ndani ya Nyumba kila chumba wanaharibu

Kila Mpangaji akiulizia vyumba anakuta vimechakaa
Uchumi wangu unayumba bora wangevikuta vimejaa
Ubaya ni kuwachekee tu hawa jamaa
Ilimradi wakinuna wanalazimisha niwanunulie Furaha

Sasa sijui ni mapepo au nini
Maana huu mwaka wa ngapi bado wameganda mwilini
Sina amani na amani ikiondoka ina Mwana sina thamani
Na thamani ikiisha ina dhihirisha sina Maanani

Hivi ni kweli sina maanani?
Au sina akili za kuongeza akili kichwani
Maana sio siri wapangaji washaharibu hadi thamani za chumbani
Nimebaki kama moja iliyotangulia kabla ya kumi nadhani

Wanalala kitandani kwenye makochi na kuzagaa mezani
Wananiita mshindi kwa kuwalisha huku wakinivika Medani
Huku nikiwa nebeba mizigo yao kichwani
Hey sijui mimi ni nani




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pangilia vizuri kuna makosa ya kisarufi.
 
Back
Top Bottom