Sifa za Mwanaume anayemchezea Mwanamke kwenye mahusiano

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
1. ANAKWEPA MAZUNGUMZO YA NDOA
Haonyeshi kufurahi unapoanzisha mazungumzo kuhusu suala la kufunga ndoa na wala hapendi kuzungumzia hilo. Wakati mwingine hata kukutambulisha kwa ndugu zake au rafiki inakuwa shida

2. ANAGHARAMIA ANASA KULIKO MAMBO MUHIMU
Anakuwa ni mtu wa kukununulia mapambo ya gharama na vitu vyote vya anasa, lakini hana mawazo ya kuzungumzia maisha yenu ya baadaye wala kukununulia vitu ambavyo vitakuwa na manufaa katika maisha ya mbeleni. Haangalii masuala ya elimu wala kukutafutia mtaji au kazi

3. HAJALI MACHOZI YAKO
Unaweza kugundua ni jinsi gani hana mpango mzuri na maisha yako, kwani hata anapokuudhi anakuwa hajali wala haumizwi na machozi yako, ni busara kuwa makini kwa sababu huyo atakuwa ni mtu wa kukupa maumivu wakati wote.

4 HAJITOKEZI HADHARANI
Mwanaume ambaye malengo yake ni kukuchezea huwa hataki mapenzi yenu yajulikane hadharani atakuwa mtu wa kutaka mambo yaende kwa siri. Hajitambulishi kwa rafiki wala kwa ndugu zako. Hatoi nafasi ya wewe kumtembelea nyumbani kwake wala kuwajua wale wa karibu yake na familia yake

5. HANA MPANGO NA WATU WAKO
Mwanamume anayekupenda atajishughulisha na mambo yanayohusiana na watu wako wa karibu, hususan ndugu, jamaa na marafiki zako. Utabaini kuwa mwanamume huyu haulizi swali lolote kuhusiana na familia yako au marafiki zako, basi tambua kuwa hana mpango wowote wa maana na wewe. Kumbuka mwanamume akikupenda hujaribu kuwafahamu na kuwapenda watu wako, maana amependa boga na sheria ni kwamba lazima upende na ua lake.

6. HAKUMBUKI LOLOTE LA MAANA
Ni wazi kuwa hujakaa sana na mwanamume huyu, lakini angalau kuna mambo muhimu umefanya naye ambayo anapaswa kuyakumbuka. Kama hawezi kukumbuka tarehe muhimu za uhusiano wenu, basi yamkini mwanamume huyu hana mpango wowote wa dhati wa kuendelea kuwa nawe.
 
We unajisumbua tu 50-65% ya Wasichana na wanawake nchini ni michepuko ya wanaume, na unaelewa sifa ya mchepuko
 
Je umeshawahi kupata mpenzi mchawi?
Nilipata mwanamke akawa anaamka usiku anaanza kuniombea laana, mabalaa, mikosi, eti nifukuzwe kazi, biashara zangu zianguke, nifilisike.
Nilipomuacha akaanza kusema nimemuharibia maisha
Sasa wewe umemuachisha kazi unategemeaje kwamfano? yan ulivo achananaye ni kama umemuachisha kazi ujue.
 
Je umeshawahi kupata mpenzi mchawi?
Nilipata mwanamke akawa anaamka usiku anaanza kuniombea laana, mabalaa, mikosi, eti nifukuzwe kazi, biashara zangu zianguke, nifilisike.
Nilipomuacha akaanza kusema nimemuharibia maisha
😂😂😂hii kweli mkuu?

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
1. ANAKWEPA MAZUNGUMZO YA NDOA
Haonyeshi kufurahi unapoanzisha mazungumzo kuhusu suala la kufunga ndoa na wala hapendi kuzungumzia hilo. Wakati mwingine hata kukutambulisha kwa ndugu zake au rafiki inakuwa shida

2. ANAGHARAMIA ANASA KULIKO MAMBO MUHIMU
Anakuwa ni mtu wa kukununulia mapambo ya gharama na vitu vyote vya anasa, lakini hana mawazo ya kuzungumzia maisha yenu ya baadaye wala kukununulia vitu ambavyo vitakuwa na manufaa katika maisha ya mbeleni. Haangalii masuala ya elimu wala kukutafutia mtaji au kazi

3. HAJALI MACHOZI YAKO
Unaweza kugundua ni jinsi gani hana mpango mzuri na maisha yako, kwani hata anapokuudhi anakuwa hajali wala haumizwi na machozi yako, ni busara kuwa makini kwa sababu huyo atakuwa ni mtu wa kukupa maumivu wakati wote.

4 HAJITOKEZI HADHARANI
Mwanaume ambaye malengo yake ni kukuchezea huwa hataki mapenzi yenu yajulikane hadharani atakuwa mtu wa kutaka mambo yaende kwa siri. Hajitambulishi kwa rafiki wala kwa ndugu zako. Hatoi nafasi ya wewe kumtembelea nyumbani kwake wala kuwajua wale wa karibu yake na familia yake

5. HANA MPANGO NA WATU WAKO
Mwanamume anayekupenda atajishughulisha na mambo yanayohusiana na watu wako wa karibu, hususan ndugu, jamaa na marafiki zako. Utabaini kuwa mwanamume huyu haulizi swali lolote kuhusiana na familia yako au marafiki zako, basi tambua kuwa hana mpango wowote wa maana na wewe. Kumbuka mwanamume akikupenda hujaribu kuwafahamu na kuwapenda watu wako, maana amependa boga na sheria ni kwamba lazima upende na ua lake.

6. HAKUMBUKI LOLOTE LA MAANA
Ni wazi kuwa hujakaa sana na mwanamume huyu, lakini angalau kuna mambo muhimu umefanya naye ambayo anapaswa kuyakumbuka. Kama hawezi kukumbuka tarehe muhimu za uhusiano wenu, basi yamkini mwanamume huyu hana mpango wowote wa dhati wa kuendelea kuwa nawe.
100 TRUE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom