Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

Namba 3 noma kumhusisha Mungu (m kubwa) bora ungesema miungu/ mungu (m ndogo). Sifa nyingine, hakuna kuota kitambi kama mimba ya miezi tisa; physique ya nguvu i.e. kifua kipana na six pack zikichomoza.
 
But kuna mengine itakubidi ulie bro,mfano kama baba umeibiwa mtoto na mwanamke kisa mmeachana na hujui alipoenda huna namna kama mm kulia hua ni njia ya kunipunguzia hasira kwa haraka
 
Naomba niwape hongera wanaume wote wenye sifa nzuri zilizotajwa. Babu natumai utakuwa miongoni mwa wanaume wa kiafrika.

Ahsante sana Catherine,

Sina hakika....but I wish I were one of those...!!

Babu DC!!
 
Mzee DC leo usingizi umegoma? hahaha! Mana jana umenicheka kulala mapema... (sorry kwa kuchakachua lol):yawn:.
 
But kuna mengine itakubidi ulie bro,mfano kama baba umeibiwa mtoto na mwanamke kisa mmeachana na hujui alipoenda huna namna kama mm kulia hua ni njia ya kunipunguzia hasira kwa haraka

Hakuna aliyesema kuwa mwanamume ana kinga ya kutohisi huzuni na hivyo kuishia kulia. Hata hivyo, pale inapobidi anatakuwa kulia kidume dume bila kupiga ukunga (yowe) ambao unaweza kuwafanya watoto wakawehuka!!

Hiyo logic huioni?

Babu DC!!
 
Mzee DC leo usingizi umegoma? hahaha! Mana jana umenicheka kulala mapema... (sorry kwa kuchakachua lol):yawn:.

Daahhhhhhhhhhhhhh,

Leo nimebanwa mahali...mzigo wa bwana haujafika...Tuombe Mungu punda asife!!

Jana ulikuwa na usingizi au ndo mambo ya kiutu uzima......???? (Hope watoto hawajaelewa!!!)

hahaha! Mzee una akili wewe! Jana ilikuwa mambo ya kiutu uzima, Inshallah usiku ulikuwa ni mzuri namshukuru Mungu. (watoto wa siku hizi wewe acha tu!)

Pole na shughuli...
 
hahaha! Mzee una akili wewe! Jana ilikuwa mambo ya kiutu uzima, Inshallah usiku ulikuwa ni mzuri namshukuru Mungu. (watoto wa siku hizi wewe acha tu!)

Pole na shughuli...

Hahahahahhahhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh

Hongera kwa kazi Da Asha....lol!!

Ngoja nisalimie kitanda kwanza kisije kunishitaki kwa Bibi!!

Babu DC!!
 
Usiku mwema DC... Salamu kwa bibi with Love...

Ahsante Da Asha,

We ndo umeamka toka mida ile juzi?

Bibi nitamwona mida ya jioni....Salamu nitafikisha....Kwa sasa najiandaa kuhesabu nyota na kujikumbusha enzi zetu za mwaka 47 ili nitafute usingize wa kizazi chetu!!

Nitarudi kusalimie baadaye kidogo!

Babu DC!!
 
haswaaaa, na wakati wa sikukuu haleti maua bali jogoo na mchele.

Idd hiyo, wee nanii, nataka hivyo.

Hii nimeipenda!Sio mwanamke kila sikukuu unalalamika huletewi maua wakati unaletewa Jogoo, Mchele na Nguo mpya!Unataka mumeo nilete zawadi za kisharobaro!Kwa kweli post za leo zimenifurahisha saana!seriously
 
Jogoo na mchele ndo mpango mzima
Kama anataka kuleta maua bora aongeze fungu la spinach au mchicha.

Hii nimeipenda!Sio mwanamke kila sikukuu unalalamika huletewi maua wakati unaletewa Jogoo, Mchele na Nguo mpya!Unataka mumeo nilete zawadi za kisharobaro!Kwa kweli post za leo zimenifurahisha saana!seriously
 
Hii nimeipenda!Sio mwanamke kila sikukuu unalalamika huletewi maua wakati unaletewa Jogoo, Mchele na Nguo mpya!Unataka mumeo nilete zawadi za kisharobaro!Kwa kweli post za leo zimenifurahisha saana!seriously

Ndugu yangu ,

Unajua watu wengi wamepofushwa na mapenzi ya kwenye display...Yaani mtu anakufanyia vitu ambavyo hawezi kuvifanya kwa muda mrefu....

Sie wenzenu bado tunabeba vinavyoonekana na kuleta manufaa kwa familia...Ndiyo hiyo migunia ya mkaa, vibaba vya matunda, mikebe ya unga wa soya n.k!! Hayo maua, hata yakiwa ya plastic siwezi kubeba mikononi mwangu!!

Babu DC!!
 
Ndugu wadau, baada ya kuona na kushiriki mijadala mingi, nimeonelea nitoe mchango wangu ili ndugu, dada, binti na wajukuu zetu waweze kuelewa tunavyomfahamu mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika.
  1. Siku zote hujitahidi kwa kila njia kuonesha kuwa yeye ni mwanamume na siyo mvulana mkubwa (big boy) au mwanamke asiye kuwa na maziwa huku akiwa ndani ya suruali.
  2. Hufanya maamuzi pale pale inapotakiwa na husimama kidete kuhakikisha maamuzi yake muhimu (yale ya busara) yanatekelezwa tena kwa gharama yoyote. Mwanamume wa kweli hatoi kauli tata na kauli zake huwa ni aina fulani ya maelekezi (orders) ya jinsi ya kudeal na issues zote muhimu ndani nyumba!
  3. Huwa halii lii ovyo hata kama kafiwa. Hujitahidi kutowaambukiza weliomzunguka emotional break down. Kwa hiyo, inapobidi kulia, huficha sura yake. Mwanamume wa kweli hawezi kuangua kilio mbele za watu hata kama kafiwa na Mungu wake!!
  4. Hatelekezi familia hata siku moja bali uhakikisha ustawi wa familia yake unakuwa kipaumbele chake cha kwanza. Watoto watapata matunzo mazuri (bila ubaguzi) kwa kadri ya uwezo wa familia na mke wake atapewa kipaumbele cha kwanza katika matumizi ya rasrimali za familia (family resources)
  5. Hufanya kila njia mke wake awe na furaha na amani kwa kumpa haki zake zote za ndoa bila mzaha (she needs a full dose).
  6. Inapotokea akachepuka mara moja moja, hutengeneza mikakati ya kuhakikisha kuwa tahadhari kubwa imefanyika ili kumlinda mke wake na familia kwa ujumla…Ushauri wa The Boss hutumika katika mambo haya. CLICK HERE
  7. Husimama kwenye mstari ili kusimamia mambo ya msingi (principles) katika uendeshaji wa familia yake kama kiongozi imara. Na pale anapokosea, hutumia mbinu za kiutu uzima kuweka mambo sawa. Kamwe hatakubali shinikizo la mke wake katika kutatua matatizo ya kifamilia ndani ya nyumba yake!
  8. Mwanamume wa kweli hafanyi mambo ya mzaha mzaha na kuomba omba misamaha isiyo na kichwa wala miguu! Hata hivyo, anaweza kuomba msamaha kwa mke wake katika mambo ambayo hayagusi misingi na uwepo wa ndoa. Ila kamwe, hatakiwi kukiri kutoka nje ndoa. Hata pale anapokamatwa ugoni (labda akutwe bolt imefungwa na nut), atatumia mbinu zozote ikiwa ni pamoja na msaada wa wanaume wenzake (wakati mwingine hata wanawake) kutunza imani ya mke kwake. Hata siku moja, hatakiwi kumweleza mke wake (kwa kinywa chake) eti katembea nje ya ndoa.
  9. Siku zote atakuwa mwanamume na baba na hatafanya michezo ya kucheka cheka kipuuzi ama mbele ya watu au wanafamilia…Lazima kila kinywa kikiri kuwa kweli huyu ni baba ndani ya nyumba!!
  10. Hakimbii matatizo hata yakiwa makubwa kiasi gani…Atayakabili kwa mbinu zozote zile ili kulinda heshima ya uanaume na ubaba wake….Ndiyo maana, watoto wadogo wanaamini kuwa baba hashindwi na jambo lolote. Kuwaonesha watoto na hata mke kuwa baba ana vitu asivyoviweza ni kuwaharibu kisaikolojia!
  11. Ataonesha siku zote kwamba hasemi uongo. Hata pale atakaposema uongo mtakatifu (mfano, kumficha kitu mke wake ili kutomvunja moyo au kuharibu imani yake kwake), atalinda maneno yake kwa gharama zozote!!
  12. Atapigania himaya yake kwa nguvu na gharama zozote zile….Hawezi kukubali kudhalilishwa mbele ya mke na watoto wake! Bora afe kuliko kuona hayo yakifanyika machoni pake!

Nawatakia week njema,

Babu DC!!

Updates

[/LIST]

Babu DC wakati unatoa haya mambo nilikuwa nimetoka muda kidogo humu jf kutokana na shughuli nyeti nyeti kunikabili.
shukrani mkuu na aksante mungu nimeiona hii kitu.
snow white thumb up ,nimeikubali hiyo ya baba wa kiafrika.
ticha gfsonwin full respect kwa hizo inputs zako.........it takes a heart kwa wanawake wa sasa kukubali hayo uliyowakilisha wewe na snow white kuhusu mtizamo wa mwanaume wa ukweli........ Ndiyo maana mara nyingi walimu wa kike huvutia sana kuingia nao kwenye ndo kwakweli
 
Ahsante mkuu. Ni ukwel mtupu! Teacher gfsonwin nakupa zako heshima. Ujumbe wako uwafikie kina dada,mama, wanandoa n jamii nzima... Asiye la mkuu hufunjika guu!
 
Ahsante sana asakuta same.

Nimefurahi kwamba umepata muda kupitia maoni ya wadau. Pia nimefurahi kuona michango yako.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante mkuu. Ni ukwel mtupu! Teacher gfsonwin nakupa zako heshima. Ujumbe wako uwafikie kina dada,mama, wanandoa n jamii nzima... Asiye la mkuu hufunjika guu!

Ahsante kashili benjamini, maoni yako ni muhimu na changamoto kwetu sote.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom