Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dark City, Aug 17, 2012.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ndugu wadau, baada ya kuona na kushiriki mijadala mingi, nimeonelea nitoe mchango wangu ili ndugu, dada, binti na wajukuu zetu waweze kuelewa tunavyomfahamu mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika.
  1. Siku zote hujitahidi kwa kila njia kuonesha kuwa yeye ni mwanamume na siyo mvulana mkubwa (big boy) au mwanamke asiye kuwa na maziwa huku akiwa ndani ya suruali.
  2. Hufanya maamuzi pale pale inapotakiwa na husimama kidete kuhakikisha maamuzi yake muhimu (yale ya busara) yanatekelezwa tena kwa gharama yoyote. Mwanamume wa kweli hatoi kauli tata na kauli zake huwa ni aina fulani ya maelekezi (orders) ya jinsi ya kudeal na issues zote muhimu ndani nyumba!
  3. Huwa halii lii ovyo hata kama kafiwa. Hujitahidi kutowaambukiza weliomzunguka emotional break down. Kwa hiyo, inapobidi kulia, huficha sura yake. Mwanamume wa kweli hawezi kuangua kilio mbele za watu hata kama kafiwa na Mungu wake!!
  4. Hatelekezi familia hata siku moja bali uhakikisha ustawi wa familia yake unakuwa kipaumbele chake cha kwanza. Watoto watapata matunzo mazuri (bila ubaguzi) kwa kadri ya uwezo wa familia na mke wake atapewa kipaumbele cha kwanza katika matumizi ya rasrimali za familia (family resources)
  5. Hufanya kila njia mke wake awe na furaha na amani kwa kumpa haki zake zote za ndoa bila mzaha (she needs a full dose).
  6. Inapotokea akachepuka mara moja moja, hutengeneza mikakati ya kuhakikisha kuwa tahadhari kubwa imefanyika ili kumlinda mke wake na familia kwa ujumla…Ushauri wa The Boss hutumika katika mambo haya. CLICK HERE
  7. Husimama kwenye mstari ili kusimamia mambo ya msingi (principles) katika uendeshaji wa familia yake kama kiongozi imara. Na pale anapokosea, hutumia mbinu za kiutu uzima kuweka mambo sawa. Kamwe hatakubali shinikizo la mke wake katika kutatua matatizo ya kifamilia ndani ya nyumba yake!
  8. Mwanamume wa kweli hafanyi mambo ya mzaha mzaha na kuomba omba misamaha isiyo na kichwa wala miguu! Hata hivyo, anaweza kuomba msamaha kwa mke wake katika mambo ambayo hayagusi misingi na uwepo wa ndoa. Ila kamwe, hatakiwi kukiri kutoka nje ndoa. Hata pale anapokamatwa ugoni (labda akutwe bolt imefungwa na nut), atatumia mbinu zozote ikiwa ni pamoja na msaada wa wanaume wenzake (wakati mwingine hata wanawake) kutunza imani ya mke kwake. Hata siku moja, hatakiwi kumweleza mke wake (kwa kinywa chake) eti katembea nje ya ndoa.
  9. Siku zote atakuwa mwanamume na baba na hatafanya michezo ya kucheka cheka kipuuzi ama mbele ya watu au wanafamilia…Lazima kila kinywa kikiri kuwa kweli huyu ni baba ndani ya nyumba!!
  10. Hakimbii matatizo hata yakiwa makubwa kiasi gani…Atayakabili kwa mbinu zozote zile ili kulinda heshima ya uanaume na ubaba wake….Ndiyo maana, watoto wadogo wanaamini kuwa baba hashindwi na jambo lolote. Kuwaonesha watoto na hata mke kuwa baba ana vitu asivyoviweza ni kuwaharibu kisaikolojia!
  11. Ataonesha siku zote kwamba hasemi uongo. Hata pale atakaposema uongo mtakatifu (mfano, kumficha kitu mke wake ili kutomvunja moyo au kuharibu imani yake kwake), atalinda maneno yake kwa gharama zozote!!
  12. Atapigania himaya yake kwa nguvu na gharama zozote zile….Hawezi kukubali kudhalilishwa mbele ya mke na watoto wake! Bora afe kuliko kuona hayo yakifanyika machoni pake!

  Nawatakia week njema,

  Babu DC!!

  Updates
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  haswaaaa, na wakati wa sikukuu haleti maua bali jogoo na mchele.

  Idd hiyo, wee nanii, nataka hivyo.
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  yaani babu DC hapo namba 9, mie hoi.

  Sio baba anacheka cheka hadi vifungo vya shati vinafunguka mbele ya hausi gelo lol
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Dark City,
  Kuna wanaume siku hizi wanatelekeza watoto kwa hoja za kuacha mbachao kwa msala upitao. Ijumaa itakuwa njema umetukumbusha.
   
 5. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Haswaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Ahsante sana Kongosho......mbona sasa uzi wangu hujautendea haki.....au hicho ki-button kimefutwa??


  Sidhani kama kuna mtu (hata wanawake) anayemhusudisha baba anayecheka cheka kama taahira!!

  Umesahau lile tangazo la Kanumba la StarTimes lilivyokera watu??

  Babu DC!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwenye hili, misimamo ya wanaume wa kweli inajulikana,

  Hebu muulize [MENTION]The Boss [/MENTION]akukumbushe anavyopokelewaga matenga ya kuku, tena mitetea kiimba nyimbo za kuaga kwao!!

  Raha sana kumpekekea mama watoto zawadi za kweli ambazo siyo hizo zenu za kisanii!!

  Babu DC!!
   
 8. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Salute mkuu disii!
  Nakuunga mkono kwa asilimia kubwa isipokuwa hapo namba 3. Mkuu kufiwa kunauma ni balaa,mwaka jana nilifiwa na baba yangu,we acha tu,msiba hauna ushujaa. Kambarage na ubabe wake 1984 unakumbuka alivyomlilia Sokoine?
  Tuanze roll call ya wachangiaji ( interesting to know watasemaje):
  gfsonwin, Kaunga, Mamndenyi, cacico BADILI TABIA, Yummy FirstLady1, Zion Daughter and the gang.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  @ kongosho,una mme weye?
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh...wengine wamejaliwa kucheka cheka..watafanyaje sasa? Nyumba zao wanajenga kwa mizaha mizaha na siku zinaenda. Nyumba zinakuwa za kiswahili kama nyumba nyingine
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Bishanga, unalia ila sio kupiga kungwi maana utaleta tafrani kijijini.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  nani atupe ya mwanamke wa kiafrika?
   
 13. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Mkuu DC, Ukipata mwanaume anayejitambua kuwa yeye ni mwanaume, sio tu kwa kutamka bali kwa kutambua nafasi yake katika jamii kama kaka, baba, mtoto, mume na Kiongozi; AMINI nakuambia mengine yoote hufuata with flow. Sababu mwanaume anayejitambua (kwa vitendo na si maneno); atathamini yale yote ya msingi katika maisha na katika jamii. Iwe ni mwanamke, iwe kazi or iwe majukumu na wajibu wake. Akitambua hilo na kufanyia kazi huo utambuzi basi mengine yaliyo ya msingi na mema na yakumpandisha/kuonesha kuwa yeye ni mwanaume wa kweli yatafuata yenyewe...
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  nina kidumu na kimtetea, kiko so african hadi raha.

   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Bishanga, kulia si hoja but kiukweli baba bora akalilie chumbani.
  Akilia hadharani familia yote inataharuki hata kama ni msibani.

  Sijui kwa wengine, but nikiona baba yangu analia?! Nitachanganyikiwa sana kwa kweli.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Dark City Nimeipenda hii ''Lazima kila kinywa kikiri kuwa kweli huyu ni baba ndani ya nyumba!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  heko babu dc,naamini pia wewe ni moja ya wanaume wa kweli wa kiafrika.good analysis!....like!
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Asante asante mkuu
  nitarudi....
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  siku si nyingi hii itasambaa kwenye facebook na group zake.....

  ila namba 6 - ndo maanamaradhi hayaishi, mume moto mke moto....

  namba 7 - hivi wanaume wakikiri makosa yao wanachubukaga ngozi eeeh? maana tabia hiyo mnayo sana...

  ba namba 9 - hiyo nyumba itakua balaa, baba akirudi watoto wanajifungia chumbani, muda wa baba ku-bond na watoto upo kweli?

  namba 8 - i reserve my comments..loh!!!!!!
   
 20. James Jahazi

  James Jahazi Member

  #20
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa kabisa hakuna ubishi, nimeipenda gold digger wote piga chini.
   
Loading...