SIFA/Kigezo cha kuowa

SOKETI

JF-Expert Member
Jul 24, 2010
206
50
Waswahili wanasema bora kukosea kujenga kuliko kukosea kuoa. Msemo huu unarihidhisha wazi kuwa swala la kuoa linahitaji busara na hekima ya hali ya juu. Ni kitu gani hasa kinachomwezesha mwanaume kutambua muda muafaka wa kuoa, Je ni fedha na hali ya kiuchumi, uzuri wa mwanamke unayetaka kumuoa, tabia yake, uhitaji wa kuwa na watoto, kutaka kuishi na mwanamke, shinikizo toka kwa wazazi na jamii nzima au swala la kuoa limekua ni fasheni(la kuiga).
 
kuowa ndo kiswahili gani na wewe? kuoa.................
sifa kubwa ni mapenzi tu................. ukiona moyo na mawazo yako muda wote yapo kwake, yaani unam-miss hata kama upo naye basi ujue ukikaa naye mambo yako yatakuwa mazuri
 
kuoa ni swala nyeti sana ni kweli kama unavyosema ukikosea kuoa uta suffer maisha yako yote, ni swala la magotini zaidi na sio kuiga wala kufanya kama fashion.
 
mimi sitakuja kuoa hadi nitimize ndoto zangu zote. may be nakosea?
Wale waleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
Ndoto hazikosi kati ya hizi.
1.Elimu (Professor may be)
2.Kazi "nzuri"
3.Nyumba "nzuri"
4.Gari "zuri"
5.Mke sorry,Mwanamke "Mzuri"
Jazia mwenyewe!
Labda na umri mzuri,hahahahaaaaaaaaaaaaa
 
Raha ya ndoa watoto, hivyo lengo kuu la Ndoa nyingi ni ma-kidz..........
 
ndoto zote nimeishatimiza ila sijisikii kuoa vile .. may be ni kwa sababu muda wangu wa kuoa umeishapita!
 
Wale waleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
Ndoto hazikosi kati ya hizi.
1.Elimu (Professor may be)
2.Kazi "nzuri"
3.Nyumba "nzuri"
4.Gari "zuri"

Jazia mwenyewe!
Labda na umri mzuri,hahahahaaaaaaaaaaaaa

zote hizo tayari bado moja nioe
 
- Kwa mali zao
- kwa uzuri wao
- kwa nasaba zao
- kwa dini zao (wacha Mungu).

Hivyo ni vigezo kwa wote, anaetaka kuoa na anaetaka kuolewa.
 
Back
Top Bottom