Sifa gani zilizomfanya Dr Shein awe bora kati ya wenzake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifa gani zilizomfanya Dr Shein awe bora kati ya wenzake?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngekewa, Jul 11, 2010.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Haya tena wanajamii CCM imetowa uamuzi utakaogusa mustakbali wa nchi kwa kumteua Dr. Shein kuwa mgombea wa urais wa sehemu moja ya Muungano (Zanzibar)

  Tulisikia mengi kutoka kwa wana CCM wenyewe kuhusu nafasi hiyo ilo ikigombaniwa na watu 11. Katika hatuwa ya mwisho majina matatu yalipigiwa kura na matokeo Dr. Shein kuwashinda Dr. Bilali na Shamsi Nahodha. Nimekuwa najiuliza wakubwa wa CCM walitumia vigezo gani vya kuwanufaisha Wazanzibari kwa uamuzi wao?

  Ama kwa mimi naona hawa watatu hawana tofauti kati yao kwa maslaha ya Wazanzibari. Naomba ukumbi unisaidie kuiondowa hofu yangu hiyo!
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Swali lina kuwa gumu kwa sababu una uliza mwanasiasa huyu ana sifa zipi zinazo mfanya aonekane kiongozi bora. Ubaya ni kwamba kwenye siasa mtu hashindi kwa kuwa kiongozi bora bali ana shinda kwa kuwa mwanasiasa bora. Ndiyo maana tunaona wimbi la watu wanaoweza siasa lakini si viongozi wakipanda vyeo na wale wanaojua uongozi lakini si wazuri kwenye siasa wakikosa nyadhifa. Ni vigumu sana kukutana na mtu ambae ni mwanasiasa mzuri na kiongozi mzuri kwa wakati mmoja na mara nyingi kama tunavyo ona kwetu mambo hayo mawili hayaendani.
   
 3. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Swali zuri sana na kama WaTZ wenzangu wote tungekuwa tunajiuliza hivi kabla ya kupiga kura bila shaka tungeondokana ana adha tunayoipata sasa. Kwa kifupi Shein hana la maana alilolifanya kwa taifa kiasi cha kupewa uongozi kama huu. His academic qualifications are very impressive, but those did not translate to a leader who produce.
  Tujenge desturi ya kuhoji wagombea kwamba Ulifanya nini kinachostahili kura yangu?
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa bahati mbaya ushindi wa Shein haukuja kwa uanasiasa bora bali ni uchaguzi tu wa CCM ulioangalia masilahi ya Chama chao na wala sio walengwa (Wazanzibari). Amekuwa kwenye madaraka ya juu karibu miaka saba sasa na hajafanya lolote linaloweza kuonekana limesaidia Wazanzibari.Hali hii pia iko kwa wagombea wenzake, walishakaa kama mawaziri Viongozi kwa vipindi vya miaka kumi kumi na hawana la kuonyesha juu ya maendeleo ya visiwa hivyo, nao pia walipewa nafasi kubwa na CCM jambo linalothibitisha kuwa walifanya kazi nzuri kwa chama chao na sio kwa Wazanzibari. Wazanzibari walihitaji wagombea wengine zaidi ya hawa watatu ambao walishapata nafasi na hawakuleta maendeleo!
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ngekewa

  Kama alivyosema MwanaFalsafa1 kuwa ni vigumu sana kumpata mwanasiasa bora at the sametime awe kiongozi bora, ubaya wa Shein hana sifa hizo zote mbali ya merits yeye si mwanasiasa kabisa.

  Kushinda kwake si kuwa kumetokana na ubora wake katika siasa bali kumetokana na maslahi ya waliomzunguka na chama chao, kuna watu wamefanya kazi hiyo on behalf hata kama angelala nyumbani wiki nzima na kuibukia ukumbini still angeshinda tu. Kwa hiyo huwezi kusema mtu wa aina hiyo ni mwanasiasa au mwanasiasa bora.

  Kwa mawazo yangu nafikiri waliomzunguka(viongozi) wamefanya hivyo kwa maslahi ya chama na wazanzibari. Wameangalia mtu ambaye anaweza kumaliza makundi yaliyoanza kujitokeza ya siasa za kihafidhina za upemba na uunguja, wametafuta mtu aliye moderate mvumilivu asiye na makundi kama walivyo baadhi ya wagombea wengine 11.

  Tumeshuhudia baadhi ya wagombea na wapambe wao walivyokuwa wakifanya kampeni chafu wakitumi maneno ya vitisho 'asipochaguliwa mgombea wetu hapatakalika' wengine wakiwagawa wazanzibari kwa upemba na uunguja kitu ambacho viongozi wa juu hakikuwafurahisha.

  Inavyoonekana uongozi wa juu ulikuwa hauna mpango kabisa wa kuweka mtu wao hata Shein amekuja kushtukizwa dakika za mwisho mwisho baada ya viongozi wa juu kutoridhishwa na majigambo ya wagombea wengine, kama wasingeendesha kampeni za chuki nafikiri hata Shein asingewekwa kugombea.
   
 6. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Si kwamba kila atakae pitishwa na CCM ndiyo lazima achaguliwe, hili litabaki swali kwa Wanzinzibari kuwa Shein aliwanyia nini since 2001 alipokua makamu na wanategemea awafanyie nini kama watamchagua awe rais wa Zanzibar kwa miaka Mitano ijayo au Kumi ijayo kama itikadi ya kuachana vipindi viwili haitakoma.

  Ukweli kwamba Shein pale kawekwa upo wazi, hakuipigania nafasi yake kuna watu wanaomtaka awe pale hata katika hotuba yake alisema atalinda Muungano na Sera ya CCM ndo itakua muongozo wake. So hizi sera zipo tangu siasa zimeanza na Muungano upo tangu mwaka 64 ila maendeleo yana hali gani??? hali ya uchumi wa Zanzibar na wa Wazanzibari upo vp?? Hajasema nini mipango yake kwa wazanzibari.

  Kwa ufupi ni jukumu la Wazanzibari kuwaonyesha wale waliomuweka Shein pale sio wenye sauti ya Mwisho ndani ya Zanzibar ila Wazanzibari ndio wenye uamuzi wa mwisho. kama walivyomtaka Shein na wakampitisha kwenye chama chao nanyi mnaweza kutumia haki yenu ya Msingi kutomchagua then tuone watafanya nini.

  October 31 ndo itamuua.
   
 7. p

  p53 JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ni lini mgombea wa urais Zanzibar/Muungano aliyepitishwa na ccm hakushinda uchaguzi/hakuwa rais?Shein ndiye Rais wa Zanzibar,ukibisha bisha mpaka mishipa ya shingo ikutoke lakini habri ndiyo hiyoo!
   
 8. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 3,996
  Trophy Points: 280
  hana chokochoko za Kiunguja
   
 9. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Huu ni Mtihani mkubwa kwa CCM dhidi ya CUF maali Seif kwani hapa tumeona na tumesoma baadhi ya watu wamechangia ni kweli hana JIPYA sasa tuone mwisho wa siku.
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu you are entitled to your opinion. Naweza kukubaliana na wewe kuwa Shein hakufanya lolote la maana toka awe VP, and it will be same atakapokuwa rais wa Zanzibar. Lakini kwa upande mwingine lazima ukubali kuwekwa kwake kwenye U-VP kumeifanya ofisi ya VP iwe ni kama conduit pipe, haina lolote linaloonekana wazi kuwa inafanya. Lakini pia ujue kuwa aliwekwa pale kama symbol of unity, sio kwa kuwa mtendaji mzuri au ana mchango fulani kwa maendeleo ya taifa as person. Kazi kubwa aliyofanya ni kupunguza mivutano serikalini, kuonesha symbol ya unity na muhimu zaidi ni mtu muadilifu, hana makuu. Sikumbuki kama nimewahi kumsikia kwenye madudu ya ufisadi. Kwa upande fulani naona it was smart decision kumuweka pale kuwa VP, na hata kumpa urais wa Zanzibar is wiser. Na tushukuru mungu yeye ndio alikuwa running mate wa JK, kama angekuwa Lowassa ina maana pamoja na madudu yote yale ya Richmond angeendelea kuwa madarakani, simply kwa kuwa alichaguliwa na wananchi. So kwa maoni yangu Shein is a blessing in disguise.

  Kuwekwa kwake kugombea urais Zanzibar ni kazi ya dola, si kwa kuwa ana mvuto kwa wazanzibar au atafanya lolote jipya, do not even think. It will be so easy to control him by a remote control, ingekuwa shida sana kufanya hivyo kwa Bilalna hard liners wengine, na katika siku za mwisho za urais wake, Karume ameonesha kabisa kuwa yeye anaanza kuwa liability, so any of his allies wangekuwa liability as well.

  So piga ua, Zanzibar Rais atakuwa Shein, kuwafanya wapemba nao wajisikie kuwa wamewahi kuwa na urais wa Zanzibar. CUF wanaweza kushinda uchaguzi, lakini CCM wataongoza as has always been. Watapigwa mikwaju, watalia na kulalama, utakuja mwafaka mwingine and then watasubiri 2015. It looks like for a third time CUF wameingia mkenge... siasa so interesting hi hi hi.
   
 11. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Labla upole wake
   
 12. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Japokuwa kwangu hana mvuto wowote wa kisiasa Naona ninchaguo bora hasa kwa kipindi hiki ambacho Zanzibar ule unaoitwa uunguja na upemba umeimarika. Ni muda muafaka huyu bwana kugombea. Sababu kuu ni moja tu kwangu. Rais wa mwaka huu Zanzibar atatoka Pemba, either awe Seif au Shein. That is History. I beleive it!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280
  Hana sifa zozote zaidi ya kuwa ni "mtu wa watu." CCM iliizima debate kati ya wagombea wa nafasi ya urais kule Zenj. Hii ingesaidia kuona kwa kiasi kikubwa tofauti ya sera kati ya wagombea wale lakini kwa kuwa tayari kuna usanii wa hali ya juu katika kupata wagombea ndani ya chama hicho basi hawakuona umuhimu wa kuwa na mdahalo. Si ajabu kabisa CCM tayari ina majina ya nani ambao watastahili kumrithi Kikwete 2015 na nani ambao watastahili kupewa nafasi ya mgombea mwenza toka visiwani mwaka huo.
   
 14. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tata hii mkuu
  mix wuth yours
   
 15. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr shein ni mpole...mkimya...hana kiherehere.....akiwepo mahali ni ngumu kujua kama yupo unilesi umeambiwa yupo! hana mvuto wa kisiasa...sina hakika kama ni mtu mwenye misimamo au laah...sijui pia kama ana kigeugeu....sijui sifa za kiongozi bora kwa znz! ingekuwa wa hapa bongo ningeweza kum jaji....ila kwa rekodi yake ya umakamu WA RAIS NATHUBUTU KUSEMA ALIPWAYA SANA....SIJAWEZA KUJUA IMPACT YA UWEPO WAKE KATIKA KITI KILE ......sijui may be ndio nafasi ile inataka mtu ajikunyate vile

  Mix with yours
   
Loading...