Hawa watakuja kujuta kama Walibya tu.
Kwa tuliowahi kuishi Iran tunajua kule viongozi wao na wananchi wao wana msemo wao kwamba "Iran is made for Iranians".... huo msemo hutumika kulenga kwenye rasilimali zao kwamba zipo kwa ajili ya kunufaisha Wairan
Kule Iran mafisadi hukiona cha moto, wavunja sheria wanashughulikiwa haijalishi we ni bilionea au nani ukiwepa kodi au kutakatisha pesa au ukiibia nchi mapesa ukaenda ficha nje unakula kitanzi tena hadharani.
Vyakula ni bei rahisi sana, ukiwa na milioni moja ya Bongo pale Iran unasavaivu mwaka mzima, vyakula ni bei chee sana hususan mchele tena ule wa Basmat.
Kwa ambao ni wachanga nawakumbusha tu kuwa Ni wairan hao hao waliandamana kumtoa Shah wakitaka mfumo wa Kiislam, ni Wairan hawa hawa walipiga kura ya maoni kwa asilimia 95 wakitaka nchi yao iongozwe na mfumo wa kiislam kwa kiasi fulani....
Gesi, mafuta ni bei rahisi sana umeme ni masaa 24, huduma za afya zipo vizuri sana kule mtu kufa kwa kukosa dawa au matibabu ni nadra sana kitiba wapo vizur sana.
Watu wanapata vitu vya msingi karibia vyote ndo maana hawakimbii nchi yao.. Changamoto ambayo ipo ni vikwazo tu na suala la ajira lakini serikali inatoa fungu la kila mwezi kwa wasio na ajira.
Ukiangalia ndo nchi yenye wanasayansi wengi wanawake wa kule ni wasomi sana.
Wana viongozi wazalendo ambao hawauzi bandari zao kwa mikataba ya kibwege,hawauzi gesi na madini kwa kubadilishana na condom na vilainishi kama huku.Venezuela ni kama tz tu nchi ilikua inaendeshwa kihuni watu wanatekwa hali mbaya na ufisadi wa kutisha....
Sijui wanaandamania nini? Matatizo yao wanafahamu fika yanasababishwa na vikwazo.....Imagine Iran wasingekua na vikwazo wangekua level ya Japan...
Sisi ndo tunapaswa kuandamana maana hii nchi yetu imeoza kila pahali, ccm wameigeuza hii nchi kuwa mnada na chaka la upigaji, huu ujinga huwezi kuukuta Iran...Na mazuri yote wanajazwa upepo waandamane...
Libya,Iran, Qatar, Kuwait, UAE,Oman ndo nchi ambazo watu wake hawapaswi kuandamana kabisa maana viongozi wao ni wazalendo na wameleta maendeleo makubwa sana
My take:Wairan watajuta mara elfu zaidi ya walibya....Hawajui wanachoandamania....
Taarifa hii kuhusu Iran inaonyesha upande mmoja tu wa hali halisi na inahitaji kukosolewa kwa uwiano.
Kwanza, madai kwamba “mafiasadi hukiona cha moto” si sahihi kikamilifu; Iran imekumbwa mara nyingi na tuhuma za ufisadi wa kifisadi wa kisiasa na kiuchumi, na si kila mtu mwenye nguvu hushughulikiwa kwa usawa.
Pili, hoja kwamba gharama za maisha ni nafuu sana pia ni ya kupotosha. Ingawa mafuta na gesi ni bei nafuu, mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya sarafu ya Iran vimeathiri vibaya uwezo wa wananchi kununua bidhaa za msingi.
-Mfumuko wa bei Ulifikia 48.6% Oktoba 2025 na 42.2% Desemba 2025.
-Umasikini, Kati ya 27%–50% ya Wairan wanaishi chini ya mstari wa umasikini
-Lishe, 57% ya Wairan waliripotiwa kuwa na kiwango fulani cha utapiamlo (2024)
-Sarafu, thamani ya Rial imeshuka sana; dola moja ya Marekani ilivuka 100,000 tomans Machi 2025
-Ajira, ushiriki wa nguvu kazi uko chini licha ya kupungua kwa kiwango cha ukosefu
Tatu, huduma za afya na dawa si bora kwa kiwango kinachodaiwa; vikwazo vya kimataifa vimeathiri upatikanaji wa dawa na vifaa vya matibabu, na wananchi wengi wamelalamika kuhusu uhaba. Aidha, madai kwamba watu hawakimbii nchi si sahihi, kwani mamilioni ya Wairan wamehama kutokana na ukandamizaji wa kisiasa, ukosefu wa ajira na uhuru mdogo wa kiraia.
Kuhusu wanawake, ni kweli wako wasomi, lakini pia wanakabiliwa na vizuizi vikubwa vya kijamii na kisiasa.
Hatimaye, kusema kwamba wananchi hawapaswi kuandamana ni kupuuza ukweli kwamba maandamano mara nyingi hutokana na ukosefu wa uhuru, ukandamizaji wa haki za binadamu na matatizo ya kiuchumi. Iran si mfano wa ukamilifu bali taifa lenye changamoto kubwa zinazohitaji kutazamwa kwa uhalisia.