Wanasherehekea maisha, kwamba wameweza kuishi na hawajafa, kwamba wamefanya mambo fulani na fulani.
Si lazima kusheherekea, ila hata ukiamua kutojiua tu ushasheherekea maisha, maana umeyapenda maisha kuliko kifo.
Kwa hiyo, kila siku ambayo hujaamua kujiua unasherehekea maisha bila kujijua.
Si lazima siku ya birthday.
Ukila chakula kizuri na kusema "chakulahiki kizuri kweli", hapo umesheherekea maisha.Kwenye kifo kadiri ya tunavyojua, huwezi kupata ladha ya chakula kizuri. Unapofurahia chochote, unasheherekea maisha. Hata unapopata mabaya, maadam unaishi, unasheherekea maisha, kwa sababu una nafasi bado ya kubadilisha hayo mabaya kuwa mazuri.
Kwa hiyo hata wewe kuja hapa JF kujumuika na waja wenzako ni kusheherekea maisha, ukifariki hutaweza kujibizana nami hapa JF.
Kwa hivyo, maisha yanasherehekewa kila siku, iwe ya birthday au si ya birthday.
Inawezekana ulikuwa hujui kwa sababu umeangalia kusheherekea kwa mtazamo finyu.
Mimi hapa kuanza kukuelezea habari hizi nasherehekea maisha, maana habari ya mimi kukaa mbali na wewe halafu tukabadilishana mawazo bila kuonana ni neema ya maisha, so far ninavyojua wafu hawawezi kubadilishana mawazo nasi hapa JF.