Sielewi kwanini watu husherekea siku ya kuzaliwa

Sielewi kwanini watu husherekea siku ya kuzaliwa

Uzi ilibidi ufungwe hapo uliposema "Katika maisha yangu....".
 
Hapana mkuu kwenye suala la kusherehekea maisha kila siku bado kila uchwao ni changamoto tu bora ya jana.
Nakwambia hivi, maadam unaishi, na hujafa,na hujajiua, unasherehekea maisha kila siku.

Kwa sababu kama hakuna cha kusheherekea, sasa unaendelea kuishi ili iweje?

Ukiamua kuishi, hata kama unaona ya leo bora jana, bado una matumaini kwamba keshoitakuwa afadhali, au hata kama si afadhaliutaweza kuimudu.

Ukishafikiri hivyo tu, ushasheherekea maisha.
 
sijawahi kufanya huo upuuzi....yani sasa hivi wamewakarirsha hadi watoto eti birthday yake leo kah na usipomfanyia au kumnunulia kitu kizuri kilio......enzi za wahenga hivi vitu havikuwepo kwa kiasi kikubwa hivi......
 
Mimi nakerwa na utaratibu wa kusherekea kumaliza shule au maosomo, yaani GRADUATION.... Jambo la ajabu kabisa hili
 
VIPI MNASHEREHEKEA UMRI UNAOZIDI KUPUNGUA KILA UCHWAO ? KAMA MWENYEZI MUNGU KAKUPANGIA KUISHI MIAKA 70 NDIO UTOKE DUNIANI HALAFU BAADA YA KUJITAMBUA UNAFIKISHA 30 UNASHREHEKEA . Imebaki 40. Ukifikisha 35 UNASHREHEKEA ! Inabaki 35 , ukifikisha 40 unasherehekea! Imebaki 30. Ukifikisha 50 . Unasherehekea imebaki 20. Siwaelewi !
 
Yaani huu upuuzi sijawahi kuufanya...yaani unafurahi kuelekea kaburini?....nilichogundua Ni ushamba ushamba flani Hivi kuiga uzungu Na maisha ya tamthilia za kifilipino,ila siamini kama wahusika wanafurahia kiukweli kutoka moyoni ila huwa wanatafuta sifa tu nao waonekane ulimwengu haijaeapita.
 
Uzi ilibidi ufungwe hapo uliposema "Katika maisha yangu....".
Hoja yangu tunaijadili kwani anaelalamika maisha mabovu ana maanisha hadi wakina mengi yanawahusu?
 
KILA SHEREHE INAMAANA KWA MUANDAAJI,KAMA HUJAONA MAANA USIFANYE SHEREHE...

PIA,


NI SIKU AMBAYO INAKUBIDI UTAFAKARI UMEZEEKA KWA MIAKA MINGAPI? UMEWAFAIDIA WANGAPI? UMETIMIZA MANGAPI? NA KAMA UKIFA LEO UTAKUMBUKWA KWA LIPI? NA UKIPATA ZIADA YA MWAKA MMOJA MBELE UTAFANYA NINI ZAIDI? NA JE,can yourself predict your destiny depend on lives you lived on this worldliness earth?......These are just some tips included after birthdayceremony.....

13-10-19s (Tomorrow z ma birthday[emoji23] [emoji6] [emoji322] Hbd priceless Soul IN ADVANCE.Haaaah)
 
Maadam tangu fertilization (conception) umekaa tumboni kwa miezi tisa ukiwa unamtegemea mama. Unapozaliwa unakua huru kujitegemea kama kula, kuvuta hewa kwa kutumia pua yako, na kujinyoosha unavyotaka. Hivyo unasherekea siku ulipokua huru, ndio maana ulilia kwani hukutamani huu ulimwengu lakini Mungu kakuambia tulia sasa upo huru. Kwa hiyo unasherekea siku ulipopata uhuru wa kuachana na tumbo la mama. Ukiambiwa utaje una miaka mingapi, ni siku ulipozaliwa ujumlishe na miezi tisa ukiwa mfungwa. Birthday ni siku nzuri ya ukumbusho
 
Sio lazima kufanya mawazo yawe sheria. kila binadamu anayo sababu ya kufanya analofanya; hata kama ni kwa vile kaiga kwa mzungu as long as ita has value kwake afanye tu ilimradi asivunje sheria.
Navyojua mie kukumbuka sherehe ya kuzaliwa ni ishara ya kushukuru kwa zawadi ya maisha. na ingawa tunaongezeka umri kila siku lakini check point za muhimu zipo. na kwa sisi washerekeaji wa birthday as new year clocks in ni lazima tuoneshe utofauti na siku zingine.

na hakuna kitu kizuri kama kushare furaha yako na wenzako.
 
Katika maisha yangu hili jambo naona la ajabu sana pale mtu anapoandaa sherehe kubwa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa maswali ninayojiuliza kuna umuhimu gani wa hii sherehe kwa yeye kuwepo hapa duniani ambayo inamfanya aifurahie ikiwa tunakufa?

Kama hukuzaliwa dunia inapata hasara gani? Kama hamna hasara basi hakuna umuhimu wa uwepo wako hapa duniani kwa kuwa sherehe yako ya kuzaliwa haina manufaa yoyote na ni batili ikizingatiwa aliekuzaa kapata maumivu makali sana kuna muda ananusurika hata kupoteza maisha yake, angalau wakina mama wao ndo wangefanya sherehe ya kukuleta duniani kwa kuwa kaokoka kifo wakati wa kujifungua hapo kidogo ingeleta maana.

Mimi huwa sihangaiki kumtumia mtu salamu ya eti hongera kwa siku yako ya kuzawaliwa au kumchangia mtu katika sherehe ambazo zinanikera basi ni hii ya siku ya kuzaliwa.
Binafsi huwa nasherehekea japo kimya kimya, sifanyi sherehe ila huna ni siku ya furaha kwangu.
Nimeanza kuiadhimisha hii siku miaka ya hivi karibuni baada ya kupitia matatizo fulani kiasi cha kuhisi kifo but kwa neema ya Mungu bado niko hai, hapo ndio ikawa kila birthday ikifika naona ni kama nimepiga hatua fulani ambayo wengi hawajafanikiwa kuifikia, .... so birthday together with mwaka mpya huwa ni muhimu kwangu, ila sifanyi sherehe
 
Nilichojifunza hapa kutokana na watu wanavyocomment nimegundua Umaskini wa kutokuwa na hela ni mbaya sana!

Binafsi naona rika sahihi la kufanya "Birthday Party" ni miaka 0 hadi 12, huyu ni mtoto na furaha yake kubwa ni kusherekea siku yake ya kuzaliwa sambamba na watoto wenzie maana hajui chochote.

Umri mwingine wa kusherekea siku ya kuzaliwa ni miaka 50 na kuendelea , hapa unakuwa kama unamshukuru Mungu wako kwa mabonde na milima uliyovuka mpaka kufikia hapo maana wanasema ukifikia huo umri akili inarudi tena kwenye utoto.

Kijana Wa miaka 20 hadi 40 ni ngumu sana kukumbuka siku zake za kuzaliwa hivyo huwa tunaona kama haina umuhimu na ni kweli sio ya muhimu.
 
Kila mtu nadhani anasherekea siku ya kuzaliwa....Ila tunatofautiana namna ya kusherekea, wengine wanashukuru Mungu tu inapita, wengine bila kumwagiwa maji bado haijawa nzuri....√√√
 
Nilichojifunza hapa kutokana na watu wanavyocomment nimegundua Umaskini wa kutokuwa na hela ni mbaya sana!

Binafsi naona rika sahihi la kufanya "Birthday Party" ni miaka 0 hadi 12, huyu ni mtoto na furaha yake kubwa ni kusherekea siku yake ya kuzaliwa sambamba na watoto wenzie maana hajui chochote.

Umri mwingine wa kusherekea siku ya kuzaliwa ni miaka 50 na kuendelea , hapa unakuwa kama unamshukuru Mungu wako kwa mabonde na milima uliyovuka mpaka kufikia hapo maana wanasema ukifikia huo umri akili inarudi tena kwenye utoto.

Kijana Wa miaka 20 hadi 40 ni ngumu sana kukumbuka siku zake za kuzaliwa hivyo huwa tunaona kama haina umuhimu na ni kweli sio ya muhimu.
Mkuu sio umasikini haina mantiki tu
 
Acheni watu wafurahie siku zao za kuzaliwa. Ni siku muhimu katika historia ya mtu binafsi. Mafanikio anayofikia mtu huanzia alipozaliwa. Na madanikio sio lazima yawe ya dunia, hata ya mtu binafsi
 
Back
Top Bottom