Sielewi hii aina ya "Mbunge wa Viti Maalum Aliyefukuzwa na chama"

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Waandishi hebu kuweni Makini basi katika uandishi wenu.
Je, Bunge lina Aina ngapi za Wabunge?
Je, ktk Aina ya Wabunge Je Mbunge wa Viti Maalum Aliyefukuzwa Anapatikanaje?
Kama kuna Wabunge wa Viti Maalum Waliofukuzwa Chadema je Bado ni Wabunge licha ya Kufukuzwa na Chama chao? Hebu Andikeni kwa Usahihi badala ya kupotosha Wananchi.
 
Hapo unapigia Mbuzi Gitaaa
Unadeki bahari
Unatwanga maji kwenye kinu

Hii issue ni ya muhimu kuhoji lakini huwezi kusikilizwa, utapuuzwa tu!
 
a.k.a wabunge wa gereji
1612964684342.png
 
Nikusaidie kwa kuwa najua akili zako ni chache

Aina za wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

1.wabunge wa kuchaguliwa (wabunge wa majimbo)

2.wabunge wa viti maalumu vy wanawake

3.wabunge wawakilishi kutoka Zanzibar

4wabunge 10 wa kuteuliwa na rais

5.mwanasheria mkuu wa serkali.

Siku nyingine uje na posts za maana
 
Kama ulichokijibu kinaendana na wingi wa akili unazohisi unazo, basi huyo muuliza swali ana akili nyingi kukuzidi ingawa umedai anazo chache.
Nikusaidie kwa kuwa najua akili zako ni chache

Aina za wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania...
 
Wale akina mama nadhani bado wanajihesabu kuwa wanachama kwa kuwa rufaa zao hazijatolewa maamuzi.

Mkutano mkuu uje ukate mzizi wa fitina tu na mbivu na mbichi zijulikane
Unakata rufaa baada ya kufukuzwa... Rufaa ikisikilizwa ndiyo inaweza ikabaditilisha maamuzi ya kufukuzwa uanachama... KABLA YA KUSIKILIZWA, NI KWAMBA ULIYEKATA RUFAA, HUKUMU YA MWANZO INAENDELEA.... Vinginevyo huna sababu ya kukata rufaa.. COMMON SENSE IS NOT COMMON
 
. KABLA YA KUSIKILIZWA, NI KWAMBA ULIYEKATA RUFAA, HUKUMU YA MWANZO INAENDELEA....
Haya ni mawazo yako binafsi au ndivyo katiba ya CHADEMA inavyosema?

Kamati kuu ina mamlaka ya kufukuza au INAPENDEKEZA tu then Mkutano Mkuu unabariki au kukataa?

Wakati huu kabla Mkutano haujayapitia mapendekezo, ile dhana ya “innocent until proven guilty haiapply?

Linapokuja suala la kanuni, sheria na taratibu, Common sense might not be common to all..
 
Then kama yalikuwa mapendekezo tu, WAMEKATA RUFAA AGAINST MAPENDEKEZO? Nijuacho, maamuzi ndiyo hukatiwa rufaa.... Mapendekezo yanakatiwa rufaa tangu lini?
Labda wanakatia rufaa mapendekezo ili atleast story yao nayo isomwe pia na wenye mamlaka kabla kubariki/kukataa mapendekezo baada ya kusikia side moja tu.

Ni kama kwenye kandanda. Usipoonekana mchezoni, mpinzani wako anatwaa point 3 kutoka mezani😂

All in all, hili saga litaisha juu kwa kuu tu. It is just a matter of time. Watasameheana kwa kile kinachoitwa “maslahi mapana ya Chama na Taifa”
 
Nimebold neno ulilolitumia... LABDA....
KUKATA RUFAA MAANA YAKE HAWAKUBALIANI NA HUKUMU..... Hivyo basi kwa vile rufaa haijasikilizwa, WALE SIYO WABUNGE WA VITI MAALUMU WA CHADEMA... watafute namna nyingine ya kuwaita....

Labda nikupe hili, ili ujuwe kwa nini akina "Ndugai" wanawang'ang'ania hao wabunge...

Ni kwamba, kwenye kamati zihusuzo fedha, NI LAZIMA WABUNGE WA UPINZANI WAWEPO, TENA KWINGINE WANATAKIWA WAWE WANAONGOZA KAMATI HIZO..!! Sasa CCM hawakuipiga hesabu hiyo wakati wa uchaguzi, wakakomba viti vyote na kubakiza viwili tu (Mtwara vijijini (kulikokuwa kwa Hawa ghasia) na Nkazi kaskazini (kwa yule atake asitake lazima akubali, bwana Kesy, kama sijakosea). Hao wawili hawatoshi kuwekwa kwenye kamati zote zinazohitaji wapinzani..!!! HAPO NDO KIMBEMBE KINAPOANZIA KULAZIMISHA WALIOFUKUZWA KUENDELEA KWENDA BUNGENI
 
Nikusaidie kwa kuwa najua akili zako ni chache

Aina za wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

1.wabunge wa kuchaguliwa (wabunge wa majimbo)

2.wabunge wa viti maalumu vy wanawake

3.wabunge wawakilishi kutoka Zanzibar

4wabunge 10 wa kuteuliwa na rais

5.mwanasheria mkuu wa serkali.

Siku nyingine uje na posts za maana
KWA Akili zako Ndogo Mbunge Viti Maalum Aliyefukuzwa mbona hujaelezea?
 
Nikusaidie kwa kuwa najua akili zako ni chache

Aina za wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

1.wabunge wa kuchaguliwa (wabunge wa majimbo)

2.wabunge wa viti maalumu vy wanawake

3.wabunge wawakilishi kutoka Zanzibar

4wabunge 10 wa kuteuliwa na rais

5.mwanasheria mkuu wa serkali.

Siku nyingine uje na posts za maana
Hawa 19 ni wabunge wa nani mkuu?
 
Faida ya wizi wa kura! Kama uongozu wa nchi unaiba bila mahesabu ya kura je kwenye raslimali ya taifa vipi?)????
 
Back
Top Bottom