Sidhani Kama hii imekaa sawa

koba lee

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
964
1,552
Kwema wakuu,
Hii ishu nimekua nikikutana nayo sehemu nyingi lkn juzi imezidi,baada ya mihangaiko yng niliamua kwenda bar flan kwenda kupiga mbili Tatu,sasa kilichoniboa ni aina ya muziki walokua wanapiga pale,tangu nafika wanapiga nyimbo za dini tena na wale mabarmaid wanacheza kwa madoido kana kwamba wapo kanisani,sasa sijui wanaona wako sahihi au ni vp, (mpigaji na wachezaji),ifahamike sio kwamba mm sipend nyimbo za dini la hasha ila tuangalie na mazingira,hii ni Kama dhihaka kwa mungu,maana nadhan mlio wengi mnajua bar vinafanyika kitu gani ambavyo ni chukizo mbele ya Mungu lkn hawa wasiojielewa wanazidi kumwaga petrol katika moto unaowaka,sikupenda hiyo hali nikamuita muhudumu mmoja nikamuuliza vp jaman hamna nyimbo zinazoendana na mazingira ya hapa,akanijibu eti boss wao ndo kawapa maelekezo hayo,sikua na cha kusema,nikamaliza kinywaji changu nikaondoka maeneo hayo,
Sio hapo tu ni maeneo mengi nadhan wengi wenu mshashuhudia hali hii,
Japo nina miaka kama miwili sijaenda kanisani lkn Mungu aheshimiwe jaman sio kupiga nyimbo za dini bar afu ma_barmaid wanasasambua,
Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukristo unaruhusu yote hayo.

Wanasema, "dini yetu inadili na vya rohoni sio vya mwilini".
 
Yaani ili siku hiyo usije kukana kwamba "sijawahi sikia chochote kukuhusu Mungu".

Unafatwa mpaka katika urabu,guest kuna bible kabisaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom