kovai tamil taiga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 1,571
- 2,192
Miaka zaidi ya 50 ya uhuru,leo hii unasifia uzinduzi wa kidaraja cha kigamboni !!!!!! wakati fedha iliyotumika hapo ingeweza kujenga barabara ya kutoka Dar hadi moro kuwa 2 kwa 4.
Ni daraja la aina yake kuwahi kujengwa eneo la Afrika ya mashariki na sio' kidaraja' - tafadhali muone daktari wa macho haraka iwezekanavyo nina imani utakuja ona vizuri!Miaka zaidi ya 50 ya uhuru,leo hii unasifia uzinduzi wa kidaraja cha kigamboni !!!!!! wakati fedha iliyotumika hapo ingeweza kujenga barabara ya kutoka Dar hadi moro kuwa 2 kwa 4.
Kwa mwendo huu wa Magu safari hii utakumbuka vingi sana,hilo ni daraja tu la kigamboni. Barabara ya Morocco Mwenge umekukumbusha nini?Unanikumbusha habari ile ya Baba aliyekuwa na uwezo wa kuipa familia yake pilau kila siku lakini yeye akawa anaipa ugali kwa maharage. Siku alipowapa wali kwa maharage kukawa na nderemo na vifijo vingi sana.......
Ungekuwa unaona kama ninavyoona mimi,usingesema ninatatizo la kuona.Hebu jenga picha ya barabara ya Dar to Morogoro kwa kiwango cha lami ikiwa imejengwa njia 2 kwa 4 ingesaidia kwa kiwango gani na hiki kichochoro kimesaidia kwa kiwango gani ???Ni daraja la aina yake kuwahi kujengwa eneo la Afrika ya mashariki na sio' kidaraja' - tafadhari muone daktari wa macho haraka iwezekanavyo nina imani utakuja ona vizuri!
Tanzania ni moja, Tayari morogoro imeshaunganishwa na mikoa mingi sasa kigamboni ilikuwa inafikika kwa tabu!Fursa nyingi za kiuchumi zitafunguka kwa kukamilika kwa hilo daraja kwa watu wa Dar na TZ kwa ujumla.Kichochoro kiko wapi?yaani hiyo picha ya daraja huioni kabisa?nachelea kukuita kipofu..!Ungekuwa unaona kama ninavyoona mimi,usingesema ninatatizo la kuona.Hebu jenga picha ya barabara ya Dar to Morogoro kwa kiwango cha lami ikiwa imejengwa njia 2 kwa 4 ingesaidia kwa kiwango gani na hiki kichochoro kimesaidia kwa kiwango gani ???
Aiyaaah...umenitia njaa mwenzioNawaza tu, kiwete amehangaika muda mrefu bila msaada wowote; ghafla akatokea wa kumpa magongo yale ya kumsaidia kutembea ingawaje yeye alitamani sana awe na kale kagari ka miguu mitatu! Hivi atasusia magongo kisa kiu yake ya kagari haijakidhiwa?! 😕. Ngoja nikale samaki makange - Break point mie.
Ha ha ha Poooole! Ilibidi nikajilie maana baadhi ya comments zilinipa njaa ati!Aiyaaah...umenitia njaa mwenzio
Say Amen to development..!