Sibishi tena..Huyu Bwana anasomeka

kovai tamil taiga

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
1,415
2,005
Leo anazindua hili...

upload_2016-4-19_16-49-35.png

Juzi Aliweka jiwe la msingi huku..
upload_2016-4-19_16-50-48.png

Halafu ile Barabara Morocco Mwenge ndo wanamalizia hivyo..walalahoi tuanze kupeta ule muda wa kuwa ndani ya daladala na joto hili la Dar kupungua.Looh Mungu akupe maisha marefu we baba..!

upload_2016-4-19_16-55-44.png
 
Kimsingi kama hakuna upigaji, na watu wakifuata miiko ya kazi,basi hata mwanagu Andunje anaweza kuwa mkuu wa nchi, Tatizo Tanzania ya JK ilijaa mchwa wengi hadi ukwapuaji rasilimali ukawa ni tunu ya taifa!
 
Ubishi kwisha kabisa..wale ambao kila mara wanaimba' hasomeki' please yamkini yawezekana mna shida ya MACHO...!!ushauri kutoka moyoni mwangu wa dhati kabisa 'tafuteni haraka sana Daktari wa matatizo ya Macho ili muyaone haya..'
 
Miaka zaidi ya 50 ya uhuru,leo hii unasifia uzinduzi wa kidaraja cha kigamboni !!!!!! wakati fedha iliyotumika hapo ingeweza kujenga barabara ya kutoka Dar hadi moro kuwa 2 kwa 4.
 
Miaka zaidi ya 50 ya uhuru,leo hii unasifia uzinduzi wa kidaraja cha kigamboni !!!!!! wakati fedha iliyotumika hapo ingeweza kujenga barabara ya kutoka Dar hadi moro kuwa 2 kwa 4.

Unanikumbusha habari ile ya Baba aliyekuwa na uwezo wa kuipa familia yake pilau kila siku lakini yeye akawa anaipa ugali kwa maharage. Siku alipowapa wali kwa maharage kukawa na nderemo na vifijo vingi sana.......
 
Miaka zaidi ya 50 ya uhuru,leo hii unasifia uzinduzi wa kidaraja cha kigamboni !!!!!! wakati fedha iliyotumika hapo ingeweza kujenga barabara ya kutoka Dar hadi moro kuwa 2 kwa 4.
Ni daraja la aina yake kuwahi kujengwa eneo la Afrika ya mashariki na sio' kidaraja' - tafadhali muone daktari wa macho haraka iwezekanavyo nina imani utakuja ona vizuri!
 
Unanikumbusha habari ile ya Baba aliyekuwa na uwezo wa kuipa familia yake pilau kila siku lakini yeye akawa anaipa ugali kwa maharage. Siku alipowapa wali kwa maharage kukawa na nderemo na vifijo vingi sana.......
Kwa mwendo huu wa Magu safari hii utakumbuka vingi sana,hilo ni daraja tu la kigamboni. Barabara ya Morocco Mwenge umekukumbusha nini?
 
ilibidi tuwe zaidi ya hapa jamani, mapenzi yasitufanye tukauficha ukweli, bora uwadanganye wengine lakini ukifikia hatua ya kujidanganya mwenyewe ni tatizo hilo, sema fresh tu!
 
Ni daraja la aina yake kuwahi kujengwa eneo la Afrika ya mashariki na sio' kidaraja' - tafadhari muone daktari wa macho haraka iwezekanavyo nina imani utakuja ona vizuri!
Ungekuwa unaona kama ninavyoona mimi,usingesema ninatatizo la kuona.Hebu jenga picha ya barabara ya Dar to Morogoro kwa kiwango cha lami ikiwa imejengwa njia 2 kwa 4 ingesaidia kwa kiwango gani na hiki kichochoro kimesaidia kwa kiwango gani ???
 
Tanzania ni moja, Tayari morogoro imeshaunganishwa na mikoa mingi sasa kigamboni ilikuwa inafikika kwa tabu!Fursa nyingi za kiuchumi zitafunguka kwa kukamilika kwa hilo daraja kwa watu wa Dar na TZ kwa ujumla.Kichochoro kiko wapi?yaani hiyo picha ya daraja huioni kabisa?nachelea kukuita kipofu..!
 
Nawaza tu, kiwete amehangaika muda mrefu bila msaada wowote; ghafla akatokea wa kumpa magongo yale ya kumsaidia kutembea ingawaje yeye alitamani sana awe na kale kagari ka miguu mitatu! Hivi atasusia magongo kisa kiu yake ya kagari haijakidhiwa?! :confused:. Ngoja nikale samaki makange - Break point mie.
 
Aiyaaah...umenitia njaa mwenzio
 
mimi nilimkubali Magufuli since day one Dodoma walipomchagua....nilipata shida sana kupingana na wale nyumbu waliokua wamezagaa kila kona ya jiji bila direction maalum..niliteseka sana!!! asante Mungu kwa kutupa raisi uyu
 
Back
Top Bottom