MwanaDiwani
Hauna hoja. Kaa Mbali na siasa za Zanzibar kwani hata mwalimu nyerere alizikuta. Naomba niseme tu hayo kwa sasa, lakini Kama unataka mjadala wa "siasa za Zanzibar", niambie tuanze mjadala huo.
Ndugu Mchambuzi,
Unachokisema ndiyo kile kile nilichowashauri CHADEMA kama chama kwenye bandiko langu la
#1 ili waache kuzidandia siasa za Zanzibar wakiwa wamebeba bango la kisiasa lililoandikwa maneno yanayosema, ''My enemy's enemy is my friend'' wakati kwenye siasa za Zanzibar, the enemy of your enemy is not always your friend.
Suala la kusema sina hoja ni mtazamo wake na pia hakuna sehemu niliyosema Mwl. Nyerere hakuzikuta siasa za Zanzibar.
Soma vizuri bandiko langu
#1
Ya vimeo vya Sitta, tuachane nayo, kwani unatetea upuuzi; yeye ameshakiri kupitia vyanzo vya uhakika Kwamba vimetoka kwake; let's focus kwa yatakayojiri kufuatia uchakachuaji wa Dodoma; naandaa Uzi maalum kwa ajili ya Hilo, nitakualika katika mjadala:
viweke hapa vyanzo vyako vya uhakika vyenye maneno ya Mhe. Sitta akisema kuwa hivyo vimemo vyote viwili ulivyovileta ni vyake. Siasa za majitaka haziwezi kukupatia unachokitafuta.
Kwa akili na fikra yako unadhani Mhe. Sitta anaweza kuandikiana memo vya wazi au siri kwa Waziri Mkuu kuhusu suala la kutoa rushwa ndani ya bunge Maalum hata kama lipo(kitu ambacho hakipo) wakati huwa anawasiliana naye uso kwa uso muda wowote bungeni.
Jaribu kufikiri kwa mapana kama jina lako linavyokutambulisha, otherwise wewe siyo mchambuzi!
Kuhusu demokrasia nchini, Ndio Ipo, lakini it's top down democracy; mabadiliko yaja - bottom up;
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mabadiliko hayajaanza leo. Kila siku ni mabadiliko katika maisha siyo ya mwananchi pekee bali hata ya kitaifa kwa ujumla.
Neno mabadiliko yaja bottom up siyo geni kwa sababu wananchi wanayaishi kwa sasa.
Kuonyesha kama tuko kwenye bottom up democracy ndiyo maana kwa sasa tunaelekea kwenye kampeni za upigaji wa kura ya maoni kuhusu Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa ili wananchi waamue kupitia sanduku la kura kuhusu uharali wa mkataba wao na watawala.