Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Uganda wamezindua mabasi yanayotumia umeme wa jua (solar energy). Shirika la utangazaji la BBC limeeleza kuwa kampuni ya magari ya Kiira Motors ya nchini humo imeunda mfumo maalumu wa umeme wa jua unaotumika kuendesha mabasi hayo badala ya kutumia nishati ya mafuta.
Kenya wamezindua kiwanda cha kutengeneza magari ya kisasa ya Mobius. Kampuni ya Mobius Motors ya mjini Nairobi wiki jana ilizindua toleo la pili la magari yake (Mobius II) ambayo ni muundo wa SUV maalumu kwa ajili ya barabara za Afrika. Mobius II imeboreshwa zaidi na inavutia kulinganisha na Mobius I iliyozinduliwa mwaka 2013.
Tanzania na sisi hatupo nyuma, jana tumezindua passport mpya. Halafu tukitoka hapo tunaenda kubomoa jengo la TANESCO kwa milioni 700, then tunarudia uchaguzi kwa bilion 2 (Siha na Kinondoni). Ama kweli kupanga ni kuchagua.!!