Kampuni ya China katika usafirishaji na ushauri wake kwa nchi za Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,008
1,032
Na Gianna Amani
1669088406624.png

Kampuni ya utengenezaji wa magari ya King Long iliyopo katika Mkoa wa Fujian imeeleza namna ilivyopenya katika soko la dunia na kuziambia nchi za Afrika juu ya magari wanayopaswa kuchagua hivi sasa.
Kampuni hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1988, mbali na kutengeneza magari tofauti tofauti, imejikita zaidi katika uzalishaji wa mabasi, na hadi sasa imezalisha mabasi 570,000 ambayo yameuzwa katika nchi zaidi ya 150 duniani nyingi zikiwa za Afrika.
Jin Shoulin ambaye ni Makamu mkuu wa kampuni hiyo anayeshughulikia biashara za kimataifa, alisema nchi nyingi za Afrika ikiwa ni pamoja na Tanzania, Kenya, DRC na Senegal ni soko lao kubwa na mabasi wanayouza huko ni yale ya masafa marefu lakini pia soko la mabasi kwa ajili ya usafiri wa mjini (City Buses) linakuwa kwa kasi. Alisema umuhimu na ukuaji wa soko hilo unatokana uhusiano mzuri wa kibiashara kati ya Afrika na China, pamoja na idadi kubwa ya watu katika bara la Afrika.
Alitolea mfano nchi kama Tanzania ambayo hivi sasa imepanua mtandao wake wa barabara za mabasi ya mwendo kasi katika jiji la Dar es Salaam, akisema mabasi yatahitajika kwa ajili ya kutoa huduma, na kampuni hiyo iko tayari kutoa magari hayo. Alisema kampuni yao inatengeneza mabasi ya aina tofauti na yanayotumia nishati tofauti ikiwamo mafuta, umeme na gesi asilia ambayo inapatikana katika nchi za Afrika.
Hata hivyo amesema changamoto iliyopo kwa mataifa mengi hususan ambayo yanatengemea fedha za mikopo kutoka taasisi za kimataifa kwa ajili ya kuboresha usafiri, sasa watoa fedha hupendelea zaidi miradi ya nishati safi jambo ambalo lina athari mchanganyiko.
“Gari litumialo mafuta bei yake ni rahisi zaidi, linalotumia gesi ni bei yake inaweza kuongezeka kwa asilimia 20 lakini linalotumia umeme bei yake ni mara 200 zaidi, muhimu ni kuangalia wewe kipi kitakuwa ufanisi zaidi,” alisema Shoulin.
Alisema vipuri vya gari itumiayo mafuta ni bei nafuu kuliko hayo mengine, lakini gesi na umeme bei yake ni nafuu zaidi kuliko mafuta, “Kabla ya kufanya uamuzi muhimu ni kufanya hesabu ya kina ya ulinganifu na mnyororo mzima wa manufaa”.
1669088426184.png

1669088439191.png
 
Back
Top Bottom