Siasa za Tanzania ni ngumu sana ila zitakuja kuwa na visasi!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Nasema siasa za Tanzania ngumu sana ila zinaonekana mwisho wasiku zitakuja kuwa za malipizo kama siasa za nigeria! Ukiangalia watu wanaomizwa na siasa iwe chama tawala au upinzani ni wengi na wanayaweka wakipata madaraka watalipiza bila shaka huu ndiyo utabiri wangu kwa leo.
 
Hiyo ndiyo itakuwa fundisho.
 
Nasema siasa za Tanzania ngumu sana ila zinaonekana mwisho wasiku zitakuja kuwa za malipizo kama siasa za nigeria! Ukiangalia watu wanaomizwa na siasa iwe chama tawala au upinzani ni wengi na wanayaweka wakipata madaraka watalipiza bila shaka huu ndiyo utabiri wangu kwa leo.
Hivyo hivyo visasi vinapaliliwa na wenyewe CCM
 
Lakini yote yanapaliliwa na awamu ya tano. Wanasiasa ni wavumilivu sana; kwa watu waliopo jikoni wanatambua na kuyaona mipango ovu yanayoandaliwa na kutekelezwa na awamu hii.
 
Kuna mtetezi mmoja wa jimbo juzi kapita mahala huku akiporomosha kejeli na matusi hadharani kumhusu mtia nia mpya.
Yule mtia nia mpya ameahidi kulipiza kisasi,sijajua ni njia ipia atatumia. Wote ni CCM.
Siku Magufuli akimaliza muda wake, jamaa watatoana roho na kuuana
 
Kuna mtetezi mmoja wa jimbo juzi kapita mahala huku akiporomosha kejeli na matusi hadharani kumhusu mtia nia mpya.
Yule mtia nia mpya ameahidi kulipiza kisasi,sijajua ni njia ipia atatumia. Wote ni CCM.
Mwezi uliopita nilikuwa Rukwa kwa kazi binafsi, nikakutana na kisa na Mbunge aliyemaliza muda wake kumchongea kwa polisi mpambe wake wa mwaka 2015 baada ya kumpigia debe mtia nia mpya. Baada ya kusota ndani siku NNE kwa kesi ya kuchonga, ametoka akiahidi liwe jua iwe mvua KISASI is inevitable!! Sijui atakachofanya ila tunajenga Taifa la wapiganaji, iwe kwa ngumi, visu, rungu, risasi au ndumba. Mleta mada una hoja ingawaje sidhani kama wasaka tonge watakuacha salama.
 
Nasema siasa za Tanzania ngumu sana ila zinaonekana mwisho wasiku zitakuja kuwa za malipizo kama siasa za nigeria! Ukiangalia watu wanaomizwa na siasa iwe chama tawala au upinzani ni wengi na wanayaweka wakipata madaraka watalipiza bila shaka huu ndiyo utabiri wangu kwa leo.
Nakubailiana sana na wewe. Bwana mkubwa ndio amefanya mambo kuwa mabaya na tena yatakuwa mabaya kweli kweli manake amewaonesha watu ukabila, visasi, propaganda, kufanya mambo hovyo hovyo, ukikteta na mengine. Kwa ujumla nchi imeharibika kabisa. Awamu ijayo ndio itakuwa hovyo kabisa.
 
Sio wote. Kuna ambao wako kama Mandela ambao watasamehe na wengine wako kama Mugabe watalipa kisasi.
 
Nasema siasa za Tanzania ngumu sana ila zinaonekana mwisho wasiku zitakuja kuwa za malipizo kama siasa za nigeria! Ukiangalia watu wanaomizwa na siasa iwe chama tawala au upinzani ni wengi na wanayaweka wakipata madaraka watalipiza bila shaka huu ndiyo utabiri wangu kwa leo.
hayo madaraka watayapata luni ilhali hakuna hiyo dalili
 
Unajua kama kuna sehemu ina siasa rahisi sana, yaani nyepesi basi ni tz, siasa yetu ni tumbo tu. Usione hata hawa wapinzani, issue kubwa ni tumbo. Mawaziri wengi walikuwepo toka awamu iliyo tangulia,ila sasa wanajida wako siriasi kuendana na mfumo, unafiki mtupu. Hata visasi unavyosema sio rahisi kwasababu ya njaa. Fulani aliambiwa kajinyea, njaa ilipokaza kaunga mkono juhudi!!!!!!!!!!! Hatuna agenda tuna njaa tuu
 
Kuna wengine unasikia wanasema uchaguzi huu lazima tutangazwe washindi make miaka yote huwa hatutangazwi hata tukishinda!! Hizi kauli sio nzuri huko tuendako
 
Back
Top Bottom