#COVID19 Siasa za nchi yetu na wingi wa vifo mitaani

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
6,270
12,310
Habari wadau wa JF

Kuna vurugu za maneno zinaendelea huko Kati ya wanasiasa katiba mpya na wengine chanjo ya covid19.

Tukiangalia mtaani vifo vimekuwa vingi lakini hatujui chanzo chake nini.

Tunaambiwa kuwa covid19 wagonjwa wapo lakini hawafiki hata 1000 maana last time Gwajima kuongelea hilo alitaja watu Kama 628 na tokea hapo hamna update hivyo hamna visa zaidi vya covid19.

Hali mtaani ipoje?
Kwa mwaka huu mzima toka January kumekuwa na vifo vingi ambapo tumeshindwa kujua nini chanzo chake maaana hata ndugu hawataki kusema.

Mwezi wa 7 na huu August hali ndio imekuwa mbaya zaidi mathalani wiki iliopita nilihuzuria misiba zaidi ya 9 iliyokuwa inanihusu kabisa yani ya ndugu wa karibu na bado imekuwa kawaida mjumbe wa serikali ya mtaa anapitia mchango wa rambirambi kila kawaida.

SIASA ZETU NA HILI TATIZO
siasa zetu ni kama hawaoni watu wakipuputika wao wanaendelea kujadili vitu visivyo vya muhimu maana afya na uhai ndio ya kwanza.

Namshangaa Dkt. Gwajima Kama Waziri wa Afya asilitolee ufafanuzi hili.

Au ndio nchi haijali maisha wanayopitia wananchi wakee?
 
Serikali inafeli kwenye issue ya Corona kwasababu wameshindwa kuwa wakweli, mfano, huwa wanatoa taarifa za idadi ya waliopata chanjo lakini hawasemi wagonjwa wa Corona ni wangapi, na vifo ni vingapi, they are too selective.

Hapo kwenye idadi ya vifo inawezekana wanaogopa kuwatisha wananchi, lakini ni bora uwaambie ukweli wajue kuliko kuendelea kukaa kimya ndio maana hata chanjo wengi hawaitaki, ni kwasababu bado hawajajua full extent ya damage inayosababishwa na Corona kwenye jamii yetu.
 
Serikali inafeli kwenye issue ya Corona kwasababu wameshindwa kuwa wakweli, mfano, huwa wanatoa taarifa za idadi ya waliopata chanjo lakini hawasemi wagonjwa wa Corona ni wangapi, na vifo ni vingapi, they are too selective...
Hao mnaotaka muwaambie kuwa watu wanakufa ni wengi wao kwani wapo dunia gani ambayo hawaoni hivyo vifo vingi mnavyovitangaza!?

Corona kwa tz ilishafeli kitambo. Watanzania ni watu wakujuliana hari,kama kuna jirani anaumwa basi majirani karibia ya wote wanajua nini shida ya mgonjwa, inapotokea yule mgonjwa kafa wanajua kilichomuua ni nini.

Na ndo hao hao watakaokuwepo kwenye msiba. sasa itokee mgonjwa alikuwa ana cancer ya muda mrefu inamsumbua na wao wanajua kilichomuondoa ni cancer alafu nyie mje mseme ni corona hapo ndo hawawezi kukueleweni kamwe na ndo maana mpaka leo kwenye madaladala watu wanajazana na bar zinatema.
 
Hao mnaotaka muwaambie kuwa watu wanakufa ni wengi wao kwani wapo dunia gani ambayo hawaoni hivyo vifo vingi mnavyovitangaza!?

Corona kwa tz ilishafeli kitambo. Watanzania ni watu wakujuliana hari,kama kuna jirani anaumwa basi majirani karibia ya wote wanajua nini shida ya mgonjwa, inapotokea yule mgonjwa kafa wanajua kilichomuua ni nini...
Hujalazimishwa kuamini, kama unadhani mleta mada anatania kwasababu bar zinajaa na hiace zinatema, stay as u are.
 
Serikali inafeli kwenye issue ya Corona kwasababu wameshindwa kuwa wakweli, mfano, huwa wanatoa taarifa za idadi ya waliopata chanjo lakini hawasemi wagonjwa wa Corona ni wangapi, na vifo ni vingapi, they are too selective...
Kweli aisee maana wananchi hawaelewi chochote
 
Hao mnaotaka muwaambie kuwa watu wanakufa ni wengi wao kwani wapo dunia gani ambayo hawaoni hivyo vifo vingi mnavyovitangaza!?

Corona kwa tz ilishafeli kitambo. Watanzania ni watu wakujuliana hari,kama kuna jirani anaumwa basi majirani karibia ya wote wanajua nini shida ya mgonjwa, inapotokea yule mgonjwa kafa wanajua kilichomuua ni nini...
Tukubaliane kwanza mwaka huu kumekuwa na vifoo vingi zaidi ya miaka yote,je nini chanzo Cha vifoo hivyo?
 
Yani kama vifo vyenye ni hadi serikali itangaze watu ndio watu waweze kujua kuwa kuna vifo vingi basi nadhani kuna haja pia ya kutangaziwa takwimu za vifo vya malaria, maana ukiangalia takwimu tunaambiwa watu wanakufa sana na malaria hata mimi mwaka juzi nimefiwa na mtu wa karibu kabisa kwa sababu ya malaria ila cha ajabu ukimwambia hicho kifo kuwa sababu ni malaria mtu anashangaa ni vp mtu aumwe malaria hadi anakufa.

Kwahiyo maoni yangu ni kwamba kama tumeona kuna faida kwa wananchi kujulishwa takwimu za vifo vya corona basi pia kuna faida kuna faida kujulishwa vifo vya maradhi mengine ikiwepo malaria nadhani watu wataweza kujua tatizo lililopo na kuweza kuchukua hatua.
 
Yani kama vifo vyenye ni hadi serikali itangaze watu ndio watu waweze kujua kuwa kuna vifo vingi basi nadhani kuna haja pia ya kutangaziwa takwimu za vifo vya malaria, maana ukiangalia takwimu tunaambiwa watu wanakufa sana na malaria hata mimi mwaka juzi nimefiwa na mtu wa karibu kabisa kwa sababu ya malaria ila cha ajabu ukimwambia hicho kifo kuwa sababu ni malaria mtu anashangaa ni vp mtu aumwe malaria hadi anakufa. Kwahiyo maoni yangu ni kwamba kama tumeona kuna faida kwa wananchi kujulishwa takwimu za vifo vya corona basi pia kuna faida kuna faida kujulishwa vifo vya maradhi mengine ikiwepo malaria nadhani watu wataweza kujua tatizo lililopo na kuweza kuchukua hatua.
Mimi nimeongelea vifoo in general this year vimekuwa vingi Sana , imagine toka na kua sijawahi kuona kijijini nilipozaliwa pakiwa na misiba angalau mitano kwa mwezi lakini last week nimeenda kuzika wa 9 wa ukoo moja
 
Serikali haina hela ya kupambana na Covid ipasavyo. Wakifanya lockdown watu watakufa njaa, uchumi utaporomoka na hali ya amani inaweza kupotea, wakiwapa takwimu za kweli za jinsi ya huu ugonjwa ulivyosambaa chanjo zilizotolewa msaada hazitatosha maana wengi watazitaka na hela za kununua chanjo hakuna. Matibabu ya wagonjwa wa Covid ni gharama sana, hospitali zinaelemewa. Ndiyo maana unaona yanayoendelea sasa hivi.
 
Watanza wakawaida kamabisa,muuza maandazi,mkaanga chips,wanabishana na madoctor
 
Mimi nimeongelea vifoo in general this year vimekuwa vingi Sana , imagine toka na kua sijawahi kuona kijijini nilipozaliwa pakiwa na misiba angalau mitano kwa mwezi lakini last week nimeenda kuzika wa 9 wa ukoo moja
Ukoo wenu mtakuwa wachawi mnalogana Sana msisingizie Corona

Hivyo Vingi viko kwenu Mimi mtaani kwangu hakuna kifo chochote toka tuzike mtu.wa mwisho kibaka mwaka juzi
 
Mimi nimeongelea vifoo in general this year vimekuwa vingi Sana , imagine toka na kua sijawahi kuona kijijini nilipozaliwa pakiwa na misiba angalau mitano kwa mwezi lakini last week nimeenda kuzika wa 9 wa ukoo moja
Jibu rahisi hapo ni kwamba hivyo vifo vimekuwa vingi kwa sababu ya corona, kwa sababu huko nyuma hakukuwa vikionekana vifo vingi labda mpaka uangalie takwimu.

Ila tatizo sasa sio wote ambao huona kama unavyoona wewe ndio maana hata humu bado kuna mabishano na ndio maana wengine humu wanasema bora serikali iweke wazi takwimu za corona.
 
Habari wadau wa JF

Kuna vurugu za maneno zinaendelea huko Kati ya wanasiasa katiba mpya na wengine chanjo ya covid19.

Tukiangalia mtaani vifo vimekuwa vingi lakini hatujui chanzo chake nini...

Tatizo kubwa ni janga kufanyiwa siasa:

1. Nimeshuhudia uzinduzi wa chanjo kulipodaiwa bila aibu chanjo ni kwa hisani ya SSH na CCM.
2. Kwenye uzinduzi vibwagizo vya SSH na CCM hoyeee kuwa rasmi.
3. Chanjo haizingatii masharti wala vigezo vya mtengeneza chanjo.

#COVID19 - Chanjo isiwe Siasa, Vigezo na Masharti vizingatiwe

4. Serikali kutokutambua wananchi tuko kwenye janga kwa kuongeza kodi, tozo tukiwa ndani ya janga.
5. Hazipo nafuu zozote tokea kwa serikali kuhusiana na ugonjwa huu maana hata kwa matibabu gharama ni juu ya waathirika wenyewe.
6. Takwimu sahihi za ugonjwa hazitolewi ili kuupa nafasi upotoshaji.
7. Mikusanyiko isiyokuwa na tahadhari kama mbio za mwenge, makanisani, misibani, magulioni, masokoni nk inaendelea.
8. Wale walioubeza ugonjwa wakaupotosha vilivyo na mambo ya nyungu leo ndiyo machampioni wa kuupiga vita kisayansi.

IMG_20210725_012351_122.jpg

9. Nk

Serikali haina mpango wala nia ya kuyahami maisha ya watu yanayoendelea kupotea kizembe.
 
Hao mnaotaka muwaambie kuwa watu wanakufa ni wengi wao kwani wapo dunia gani ambayo hawaoni hivyo vifo vingi mnavyovitangaza!?

Corona kwa tz ilishafeli kitambo. Watanzania ni watu wakujuliana hari,kama kuna jirani anaumwa basi majirani karibia ya wote wanajua nini shida ya mgonjwa, inapotokea yule mgonjwa kafa wanajua kilichomuua ni nin...
Nakuhurumia sana mkuu.
 
Tatizo kubwa ni janga kufanyiwa siasa:

1. Nimeshuhudia uzinduzi wa chanjo kulipodaiwa bila aibu chanjo ni kwa hisani ya SSH na CCM.
2. Kwenye uzinduzi vibwagizo vya SSH na CCM hoyeee kuwa rasmi...
Kweli kabisa,Sasa jamii ifanye nini iliiokoke?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom