bambumbile
Senior Member
- Aug 30, 2009
- 109
- 0
Mutwa,labda nami niulize ni kibarua gani huyu tena kijana mdogo wa kyela anaweza kuwa na mwakili wake dar akawaambia waishtaki IPPMEDIA?au kuna mwakalinga mwingine yupo nyuma ya huyu mwakalinga kibarua?
vinginevyo naaza kuamini mwakyembe amefanya kazi ya ziada kuleta maendeleo mpaka vibarua wa jimbo lake wana wanasheria wao
big up sana mwakyembe kwa hilo.
asante engineer kwa ushauri wako,simpendi yeyote kati ya hao wagombea wenu watarajiwa kwakuwa ya kyela ikifika uchaguzi tutawaachia wenyewe,
lakini kwenye story yote iliyopo anaetajwa ni dan mwakalinga ambaye kwa mujibu wa mtanzania ni yule kibarua kwahiyo sijui wewe umetoa wapi uhakika kwamba alipomalizia kusema mwakalinga amewaambia wanasheria....... alimaanisha george na sio dan?labda you know them better ndio maana unaweza kusoma mawazo yao.
Sikonge,
Hii habari mimi niliituma moderators wa JF wakasema ni majungu.
Ni kwamba huyo kijana alikamatwa akiwa ana record mkutano wa mbunge kwa kutumia simu. Baada ya hapo wakamfungia kwenye gari, kisha wakampeleka nyumbani kwa mbunge Ikolo na kuanza kumpekua, wakamnyang'anya simu, wakasoma sms zote.
Walimkamata saa nane mchana lakini wakamfikisha polisi saa mbili usiku wakati huo tayari jeshi la polisi limeshaanza kumtafuta.
Walipoona balaa wakazua case ya kwamba alikuwa na mwenzake ambaye alikuwa na kisu na walitaka kumdhuru mbunge. Polisi hata wamejua kisu kilinunuliwa wapi mjini. Ni yale yale ya ajali ya Iringa na kusingizia kugongwa na lori kwa nyuma.
Kwa taarifa za chini chini, RCO na kundi lake wameshathibitisha kwamba ni uwongo mtupu na sasa wanaandaa taarifa ambayo kila mtu anaisubiri kwa hamu maana kuna mtu atafungwa safari hii.
Huwezi kumteka kijana na ukampeleka nyumbani kwako na kumtesa masaa sita wakati hiyo kazi ni ya polisi, tena polisi wenyewe wako sio mbali na hapo mkutano ulipokuwa unafanyika. Hayo yote yanafanywa mbunge anashiriki, mtu ambaye inatakiwa aongoze kwa kulinda sheria.
Nipashe hawataji muda kwasababu haiingii akilini umkamate mtu aliyetaka kumuua mbunge saa nane na umfikishe polisi saa tatu usiku.
Wengine hapa tumetulia na uwongo huu utaumbuliwa mno. Someni na nipashe ya leo muone waliyoyaandika. Ni magazeti ya Mengi yanatumiwa vibaya na watu ambao wanataka wabaki madarakani kwa njia zote. Kila mtu anasubiri RPC wa Mbeya anonge.
Sasa unataka tusome gazeti la mtanzania?? Lakini tusubiri tu mwisho wa haya yote ni 2010, tusiwe na haraka ya kuhukumiana. Swali hapa ni kwa nini alikuwa anarekodi mkutano??
kwasababu kwenye mikutano yake vijijini anatoa majungu kwamba mwakalinga kahongwa milioni 400 na akina lowassa. Huo ulikuwa ni ukusanyaji wa ushahidi wa hizo tuhuma.
Ku record mkutano wa hadhara sio kosa.
hivi una wasiwasi kuwa lowasa na rostam hawajahonga kumwondoa mwakyembe? Hivi lowasa kukumsikia pale bungeni alivyolalamika kuhusu ripoti ya mwakyembe, na je hukumwona mama regina lowasa akiangua kilio kule kwenye gallery ya nunge?
wewe umehongwa na nani mpaka unaandika haya hapa? Sisi tunakaa mbeya na tunaifahamu mbeya acha kujidanganya
Na wewe umehongwa na nani kuandika hapa? Acha upumbafu wako.
Kwahiyo kila anayegombea ubunge na Mwakyembe basi kahongwa na Lowassa?
Mwakalinga mwenyewe ana miradi yake ya kutosha wala hahitaji kuhongwa na mtu.
Mbona yeye Mwakyembe anapewa pesa na Mengi? Nani kalalamika kuhusu yeye kudhaminiwa na Mengi?
Mpambano utaamuliwa na wananchi kwa kupima maendeleo ya Kyela na wala sio pesa. Huyu jamaa yenu anagombana na kila mtu hapa wilayani, anafikiri watu ni wajinga? Mtashangazwa kweli 2010.
Sasa anaanza hata kuteka vijana, huyo ni mwanasiasa kweli?
Sikonge,
Habari nilizozinasa sasa hivi hapa ni kwamba Mheshimiwa mbunge ana haha kumtafuta IGP Mwema asaidie. Sijui atamsaidia nini wakati ukweli wote uko wazi.
Pia alikuwa anamgombeza mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Kyela na kudai kwanini amemtoa kijana Dan nje tena bila masharti yoyote. Akaambiwa hawaweki rumande watu ambao hawana makosa. Pia akamwambia case hii yote inasimamiwa na RCO na RPC na akitaka awaulize wao.
Police wanasema hawataki kukurupuka na kufanya makosa ya wale wenzao wa Iringa. Wanaenda taratibu na kila ushahidi kuuweka sawa. Mtu hawezi kutumia uongo ule ule mara mbili.
Nasikia RCO ni moto wa kuotea mbali, jamaa akaamua ampigie IGP ambaye naye kamkaushia, akaishia kuongea na wasaidizi.
Amelikoroga mwenye wacha alinywe, sisi watoto wa kijuweni tunasema amefulia.
Jumatatu kuna mkutano wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na huenda hili jambo likajadiliwa maana tayari viongozi kadhaa wa mkoa wametuhumiwa na mheshimiwa kwamba eti kuna sms zao. Watataka waonyeshwe hizo sms.
Kama kawaida mimi nitawaletea habari. Engineer kwa breaking news za Kyela ni hatari tupu, mwache Masanilo apasuke bichwa!
Niseme tu kwamba mtu yeyote anayebeza juhudi za akina mwakyembe et al. ana matatizo ya akili.
ebanae, wewe Mkama unatoka Mara? mbona watu wa huko hawana ukabila? duh! upo kikabila kinoma mzee. Mbona unaondoa muunganiko wa vita dhidi ya ufisadi? acha hizo bro.
MkamaP,mtu anayeongelea ukabila si mkabila ila anaye upractisi ndiye mkabila kama mbowe na genge lake.
Kwani wanaoongelea UKUMWI wote wana ukimwi .teh teh teh pole sana.
wewe fuatilia tu utaona 99% wanaosifiwa wanapigana na ufisadi kwa sababu moja ama nyingine wana connection na uchagani,kwanini kwa sababu wanaowasifia wengi wao wana connection hiyo hiyo.
Ndo maana utakuta majemadali wa kweli kama marehemu CHACHA,jemedali ZITTO,jemedali MAGUFULI wanaitwa MAFISADI.
Kwani wewe husituki hata yule jamaa aliyevamiwa na wanchi yule mbunge mchaga anayeitwa sijui KIMARO ,yule aliyevamiwa ktk shamba ETI naye ni MPIGANIA UFISADI lakini kwa viwango vyao kama vya Mbowe.
Ng'wanza Madaso;
Join Date: Mon Aug 2009
Posts: 11
Thanks: 0
Thanked 5 Times in 4 Posts
Rep Power: 0
MLIKUWA MKISOMA KAMA WAGENI SASA MMEJIUNGA
Mh Ng'wanza Madaso,
Uko sawa hapo juu kuwa mimi ni mugeni (mgeni) humu ndani mwa JF. Kwa kuwa wewe unahelekea(unaelekea) kuwa ni mwenyeji humu JF hebu nielimishe, sisi hambao tulikuwa tunasomaga (tunasoma) kama WAGENI kwani ni makosa kuhamua (kuamua)kujiunga na kuchangia? Au unanishambulia kwa kuwa nimesema kitu hambacho wewe hakikupendezea? Kama ni hivyo si ungeshambuliaga (ungeshambulia) tu pointi nilizotoa badala ya kunishambulie eti mimi nilikuwa nasoma na baadaye nikahamua (nikaamua) kujiunga. Usemi wa kizungu unaosemaga (unaosema) kuwa "attack the message not the messenger" nadhani inabidi kuutafakari kama unapenda kufanya hivyo kwa faida yako.
Wewe nafikiri ndiye una matatizo ya akili. Nani anabeza kazi ya Mwakyembe kwenye Richmond?
Kwasababu alifanya kazi nzuri Richmond basi ndio ajichukulie sheria mkononi mpaka kuanza kuteka vijana?
Soma hotuba zake, hata sehemu moja haongelei maendeleo ya Kyela. Kama anataka kuwa rais wa nchi si agombee urais?
Kyela watamwajibisha kwa kushinda kufanya kazi za kusukuma maendeleo wilayani kwake na badala yake ni migogoro tu.
Mbona Dr. Slaa anafanya kazi na RC wa CCM? Yeye kila siku ni malalamiko tu RC ananikwamisha. Hivi kazi za RC na mbunge mbona ni tofauti sana?
Tatizo lake ni kutokukaa Kyela; sasa baada ya kutokea Mwakalinga ndio anajifanya kukaa Kyela lakini badala ya kuunganisha watu analeta vituko vya kuteka vijana na uwongo eti simu ina sms za vigogo. Nimeongea na ofisi ya RCO wanasema ni usanii tu wa Kyela. Kweli Kyela inahitaji mbunge wa namna hiyo?