Siasa za Kisasa au Kupoteza Dira kwa Vyama vya Siasa Tanzania? CCM, CUF na CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za Kisasa au Kupoteza Dira kwa Vyama vya Siasa Tanzania? CCM, CUF na CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Sep 9, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  CCM - Wanaiogopa CHADEMA na kutumia nguvu kupita kiasi kukidhibiti: Wamesahau/wameifunika itikadi yao imara ya 'Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea'

  Je ni kwasababu wametekwa na woga wa kivuli chao kinacho sababishwa na mwanga wa CHADEMA? Au ni makusudi kwakuwa viongozi wake wamekiuka miiiko ya chama na wanahangaikia mapenzi yao binafsi? Je vingozi hawa wanaopotosha misingi imara ya Chama cha Mapinduzi wanahofia kuadhbiwa ndo maana wanapambana chama kubaki madarakani au wana nia ya kweli ya nchi hii? chama hiki kitapona na shutuma za undugu?

  CHADEMA- Wanadai mabadiliko, yapi? Sikumbuki kuona orodha! Na wanaletaje mabadiliko hayo wanayodai? Wamefanikiwa kuwatisha viongozi wa CCM, kwakuwa wako gizani wamewamulika na tochi ya ghafla, Mwanga wa CHADEMA unatokana na kurunzi yenye tochi imara au za muda tu ambazo zinaweza kufifia kutokana na jazba badala ya sera? Chama hiki kitapona na shutuma za ukabila?

  CUF- Walilewa mapenzi ya CCM huko Zanzibar, wanaibuka na kukumbuka wakati wa uchumba, mambo yalikuwa machungu, lakini wakakubali ndoa, sasa wanashtuka kuwa ndoa yenyewe inaweza kuwa chungu kama ile ya uchumbani? Je wameanzisha itikadi ileile ya misingi ya "Kufa baadhi ili wengine waishi milele"? Hawa waliozinduka ni watoto wa kambo wa bara? Wa Zanzibar wana hisia zile zile bado? Je wamegundua kuwa kuna Mke mpya anakutarajiwa kuolewa na CCM? Na wivu umewajaa wanaanzisha kampeni za kumchukia mume wao ili hata huyo mrembo mpya asiingie? Safari Hii CUF itapona na shutuma za udini?

  Nia yao ya kugombania kushika madaraka ya nchi hii ni dhati na ya kweli? Au tutaona ya nchi jirani za Zambia na Malawi ambapo waliogombania madaraka kutoka upinzani walifanya madudu zaidi ya yale tuliyoyaona?

  Nani kati ya hawa watatu ambao bila ubishi wanashikilia hatamu ya siasa za Tanzania, atatupeleka kwenye nchi yenye neema na amani kwa watu wote bila kujali itikadi, hali yao kiuchumi, kisasa, kidini au kiasili? unahitaji nini kati yao, moja wapo ya chama hiki au Kiongozi kati yao atakaebadilisha upepo na kutuepusha na mgao unaofanywa na vyama vyote hivi (kwa manufaa ya hao wanaoongoza vyama hivi kwa kuwa wanataka kuendelea kuwepo madarakani?) Huko madarakani kuna nini?

  Nani atatuambia tutatokaje na siku moja itakayolengwa kwa sisi kuwa sehemu ya taifa Afrika, au Duniani imara kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimaendelo kwa ujumla (sayansi, usalama wa chakula, nafasi sawa ya elimu kwa wote, huduma za afya wote, maji safi kwa wote, ziada ya fedha, dhahabu na mafuta ambavyo tunavyo na kila mtu akimvumilia mwenzake na kumheshimu).

  Kama ungependa kunukuu makala hii kwenye gazeti, wasiliana nami kwa kuni PM.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Profesa,
  Hii kitu imesimama. yaani umenipeleka mbali sana kuanza kuchambua vyama hivi na nasikitika kusema kwamba NCHI imepoteza dira na sasa hivi Vyama vya Siasa navyo vimepoteza DIRA. Hivyo sio swala la Katika, sera wala Ilani za vyama isipokuwa tatizo letu ni WATU.. Sisi wenyewe ndio WAJINGA wanaofikiria wameelimika wakati hawajaelelimka, wanaofikiria wanajua kumbe hawajui maana ujinga (kutoelimika) upo wa aina nyingi sana.

  Kuelimika ni pamoja na kujua kwa undani matatizo na mahitaji yetu yanatokana na nini na tutaweza vipi kuyaondoa. Hivyo tunaposhindwa hata kuyakabiri isipokuwa kwa maneno matupu yenye kutafuta mchawi mara zote huwa ni ukosefu wa ELIMU..Siasa zetu zimejaa majungu, chuki na imani za Uchawi hivyo Ujinga ni sehemu ya utamaduni wa siasa za Tanzania and for that I hate politics..
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  CCM waliingia katika mfumo wa vyama vingi kwa shingo upande. Waliona kuwepo kwa utitiri wa vyama kuwa ni mtaji kwao kwa sababu ya umri wao na kwa sababu ya kazi aliyoifanya Mwalimu Nyerere kujenga chama cha watu Tanzania. Lakini kadri walivyozidi kutupilia mbali kanuni zilizojenga chama, ndivyo kilivyozidi kutengana na watu wa Tanzania. CCM kingependelea kuona vyama dhaifu vya upinzani ili kuuonyesha ulimwengu kwamba wanakubali multipartyism. Lakini kufikia mwaka 2005 ilikuwa ni wazi kabisa kuwa CCM imeshindwa kutoa uongozi bora. Na kama alivyosema Mwalimu, Watanzania watautafuta nje ya CCM.

  Umesema Chadema hawajaonyesha sera. Inaonekana wewe ndiye hujafuatilia kwa ukaribu matamshi ya viongozi wa Chadema. Wakati CCM imepuuza elimu Chadema wamesema watawekeza kwenye elimu. Wakati CCM imeshindwa kudhibiti ufisadi, kwa sababu ndiyo kula yao, Chadema wameshasema ni hatua gani watakazochukua kupambana na ufisadi. Kwa mtanzania wa kawaida hizi ni ahadi tosha za kuwafanya waipe Chadema nafasi.

  Pia umezungumzia suala la ukabila. Nadhani hii ni single ambayo inakufa polepole kwa kuzingatia umaarufu wa Chadema katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Sidhani mtu mwenye akili timamu anaweza kusimama leo na kusema Chadema ni chama cha ukabila kwa sababu tu kwamba Freeman Mbowe ni mchagga na Dr. Slaa ni mbulu. Utamweka wapi John Mnyika? Utamweka wapi Sugu? utamweka wapi Tundu Lissu na Wenje? Watanzania wamechoshwa na ulaghai wa CCM.

  Kuiondoa tu CCM mamlakani itakuwa hatua kubwa mbele kuelekea Tanzania ambayo lazima iwe.
   
 4. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Jasusi, sipingani na wewe, na labda nijikosoe kuwa sikumaanisha CHADEMA hakina sera, ila kuna hatari ya kuzidiwa na mapambano ya kisiasa na kuacha kuzungumzia sera za chama na 'itikadi' na kujikita kwenye kurushiana makombora na shutuma ili kuwafanya wananchi wa kichukie chama mnachokilenga.

  CHADEMA bado nahitaji kuelewa ni itikadi gani wanayotaka kuisimamia, Uchumi unaojengwa na Jamii kubwa kwa upana au Uwekezaji wa wenye uwezo wa chache ambao wanawea kuota ajira kwa wengi? Siasa ya Mabadiliko, yapi hasa, maana usiniambie kuondoa ufisadi ni sera au itikadi, ni neno tunaloliita 'Moto' kwenye kampeni au ujumbe na husimamia mambo fulani ambayo yanatakiwa yatokee. CHADEMA inataka kuleta mfumo gani kama wanaamini mfumo wa Kijamaa (na kujitegemea) wanaamini umeshindwa?

  Tangu mmeanza siasa, mapambano makubwa yalilenga chama kilichopo madarakani, lakini ninahofia sasa mapambano yatajuisha CUF kwa kuwa wamewashambulia jana, maana hizi ndio siasa zilizotawala.

  Natamani kuona CHADEMA wakielezea kasoro zilizopo kwenye mfumo wa sasa wa kiuchumi, kisasa na kiutawala. Usiniambie ufisadi, wizi au elimu duni au kutokuweo kwa umeme ni kasoro za mfumo la hasha, hayo ni matatizo yanayotokana na udhaifu wa mfumo wa kusimamia uchumi, siasa na utawala.

  Uongozi ni uwezo wa kuota dira na kuhamasisha maono na matarajio yaliyoko mbele na kuwafanya watu kusimamia na kuuboresha mfumo kwa moyo wao wote huku wakiamini na kushiriki kuyafikia matumaini yao ya kufikia maono yanayotolewa na uongozi kupitia mfumo uliowekwa. Je tuna uongozi au ni utawala tu? Je nikipi tunahitaji kwa sasa utawala au uongozi? Au tunahitaji vyote? Kwanini?

  Kila chama kina utamaduni, na utamaduni si sera wala itikadi ni utamaduni wa chama. Kwa hiyo utamaduni ukiwa ni "Takriama" kama ilivyokuwa kwa CCM miaka ya hivi karibuni, basi wengi nwanafuata humo na huwa tamaduni hizi si lazima ziwe kwenye mfumo au sera yoyote ya chama. Utamaduni ukiwa ni kutumia kauli kali za vitisho na kujiona mnaonewa kama ilivyo CUF basi inakuwa hivyo, CHADEMA utamaduni wenu unadhani unaweza kuwa nini?

  Hata neno ufisadi ni kujaribu kuutokomeza utamaduni wa rushwa na kujilimbikizia mali ambao umeota mizizi ndani ya CCM (ingawa siamini sana hilo, kwani inaweza kuwa kiini macho cha kufunika kombe mwana haramu apite kwani ilifika wakati ukizungumzia matatizo ya ndani ya chama kama rushwa na upendeleo wa kindugu ndani ya CCM wewe unabadilika kuwa adui). Na kila mtu iwe kwenye kikao au kwenye kampeni anafikiri atatajirika vipi harakaharaka ili ajenge, anunue gari, au afanye kitu kingine kama waliofanya walivyoweza. Tamaduni hizi kama chama kinatawala basi huingia moja kwa moja kwenye mfumo wa utawala yaani serikali.

  So mnieleze mabadiliko gani mnataka kuyaleta, msiniambie mnataka kuondoa ufisadi, siamini kwenye hilo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. m

  mharakati JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Profesa unaamini wapinzani siyo mbadala wa CCM...wenyewe wakiingia watafanya more or less kama CCM.. Watakuwa mabawana wakubwa, motorcade ndefu, suti kubwa, excuses nyingi za serikali haina uwezo, wanasafiri na kucheka cheka na mabepari wa kimataifa katika miji mikuu kama London, Paris, na Washington DC, huku miundo mbinu ikikua kwa kasi ndogo, afya na elimu vikiwa bado taabani au kuonyesha unafuu mdogo, tofauti ya vipato ikiendelea kukua kwa kasi huku umaskini ukizidi, kilimo kikiendelea kuwa chini, wakiwa wenyewe na rungu la dola sasa watakua wakinyanyasa wenzao walio nje ya serikali kwa kutumia polisi na usalama huku mipaka ya nchi ikiendelea kuvuja na raia haramu wakiendela kuingia na kuzagaa nchini......etc etc
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo Profesa, unachotaka kujua wewe ni priorities za Chadema na si sera, au? Mimi si msemaji wa chama, ni mfuasi tu, tena bado niko mbali na nchi, lakini katika uwekezaji, tofauti kubwa kati ya Chadema na hii CCM ya Kikwete ni kwamba CCM wameachia usukani wa uwekezaji mikononi mwa wageni.

  Chadema tunaamini kuwa sisi wenyewe ndiuo tunaopaswa kushika usukani wa kuwekeza na wageni wakikaribishwa kama washirika na sio waendeshaji, kama ilivyo hivi sasa. Umesema huamini kauli ya Chadema ya kuondoa ufisadi. You are entitled to your opinion. Lakini bila kuondoa ufisadi tuatendelea kupoteza 30% ya mapato yetu na fedha za maendeleo katika mifuko ya wajanja wachache, kama alivyokiri, Kikwete, bila kuchukua hatua zozote kupambana na hali hiyo.

  Tutaimarisha utawala wa kisheria na kuhakikisha takukuru ina meno ya kuwafikisha hatiani wote wanaotuhumiwa kulihujumu taifa kwa ufisadi. Inavyoonekana ni kwamba viongozi wa Chadema wanapozungumzia mabadiliko waliyodhamiria kuyaleta baadhi yenu mnaweka pamba masikioni na mnachoona na kukisikia ni mashambulizi tu dhidi ya CCM.

  Unapoilaumu Chadema, hakikisha, umesoma malengo yao na umesikia kwa kiasi kikubwa wanayosema viongozi wa chama.
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Jasusi,

  CHADEMA started as the center right political party. This platform didn't take them anywhere because there is no audience for that. So you can't convince me that CHADEMA have policies when they can't articulate what they stand for.

  Currently CHADEMA are playing populist politics. They tell us they will do exactly what CCM have failed to deliver. This kind of politics is very easy when you are in opposition. But it doesn't work well when you are in charge of running the country.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Zakumi,

  Chadema is still a center right party. Nothing is wrong with that. But what has happened is that since Nyerere's death CCM has ditched even the best ideas that he had. So let us say there is a void today in terms of ideas and policy within CCM. Chadema is the only altenative. I like Chadema's stand on "foreignization".

  I like Chadema's idea on empowering Tanzanians in investing in their own country instead of relying on foreigners. Umeona wale wachina waliokamatwa wakichimba madini kwenye mbuga za wanyama? Hii si ajabu chini ya CCM. Isingeweza kutokea chini ya Chadema. Kuna kitu kinaitwa "resource nationalism," ambayo leo CCM hawana.

  In the absence of any party articulating Nyerere's ideas I feel comfortable supporting Chadema. At least wao wana uzalendo. CCM wamebaki na unyama tu, kujipendekeza kwa wazungu na kujaza matumbo yao.
   
 9. m

  mharakati JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  this is what ive been saying here for long now, CDM just ride on the back of people resignation with CCM's incompetence on economy, and political leadership.

  CDM dont offer clear alternatives to CCM's problems. Removing change excitement, and CDM looks naked without clear and precise strategies on how to let say increase national income, tackle corruption. You corner them in this, they tell you the new constitution will take care of corruption, well the current constitution is very clear on corruption and its punishable by law, and yet we havent seen any corruption culprit put behind bar "seriously"". You go ahead and say what enforcement strategy they will use because a constitution however good without implementation is still a piece of paper, they dont have an answer for that. And this for a sober mind its not real change, its not the change this country wants especially now in this juncture of our history. Its like moving rooms in the same house while the kitchen, the garden, and the neighborhood is still the same. CDM needs to move Tanzania to a new house and not a different room in the same house.
   
 10. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Mharakati, tunataka kiongozi mwenye uwezo wa kutawala sio mtawala mwenye uwezo wa kuongoza, kwa kuwa ya kwanza huongozwa na maono ya pale tunapotaka kwenda na ya pili huongozwa na kusimamia ili vitu visiende hovyo aidha against or in support of those in power na si lazima kuwepo na maono ya kitaifa ya wapi tunataka kuwepo. Kwa sasa tuna mtawala na anahakikisha miaka yake mitano, kama si kumi inatulia ili imalizike salama, na si lazima asimamie maono yeyote yale yaliyowekwa aidha na watu au viongozi waliopita, bali amalize apumzike bila shari.

  Kiongozi tunaemtaka tunataka asimamie maono ya kule tunakotaka kwenda na hata kama ana maono yake basi kwa kipindi tunachompa dhamana awe na uwezo wa kuweka misingi ya kufuatilia maono ya kule tunakotaka kwenda.

  Hayo unayoyasema hapo si mageni kwa nchi karibu zote za Afrika! Waliokufa juzi mgodini Afrika ya Kusini hawakuffa kwa sababu ya kudai mshahara kama wengi tunavyoona, kiundani watu hawa wanapigania tofauti ya vipato inayoendelea kukua kwa kasi huku umaskini ukizidi. Na bado sijashaiwshika kama tuna kiongozi yeyote kwa sasa anaezungumzia kwa ufasaha atatutoa vipi kwenye haya! Ninawasikia viongozi wa kisiasa wanaopelekwa na mada za wenzao wakisubiri kutafuta maneno makali ya kujibu au kumdhalilisha au kuhakikisha mwingine anadhalilika. Na wootte kwa kweli wamenasa kwenye mtego huu wa siasa za aina hizi, wakiwana hofu ya mwenzake kuchukua madaraka au kuzuiwa kuwa madarakani, na wanasahau kuwa wanawajibikwa kwa wananchi na asilimia zaidi ya 80 ambao wana kipato duni wanataka kuona nani atakaetutoa huku tuliko.

  Je viongozi wa sasa wana mbinu gani za kutuponya na ukoloni mambo leo? Kujenga uchumi wa ndani, kukuza kipato cha watu wa hali ya chini na kuhakiksha huduma zote muhimu ni bure? na asituambie tu atatupa huduma hizi atushawishi pia kuwa anawezaje kuweka mazingira yatakayowezesha hili (Kama tunavyosikia kwa wenzetu wanaongelea mfumo wa kodi, mfumo wa biashara, mfumo wa elimu na wa afya kuhakiksha watu wote wanapata huduma bila kujali anatoka wapi)? Je wanawezaje kusimamia miundo ya kiuchumi inayotoa mbadala na kutuponya bila kuharibu uhusiano na watawala wa magharibi ambao hawakwepeki na kuingia gharama kubwa ya kushughulika na adhabu zao ambazo tunaona wanazitoa kwa nchi nyingi tu? na wasipotoa adhabu wanakungóa madarakani. Je atafanya biashara na Mashariki bila kugongana na Magharibi? kwakuwa Mashariki biashara ni nzuri magharibi biashara si nzuri sana ila kila upande una faida katika kufanya nao biashra.

  Ni nani huyu katika chama gani anaeweza kusimamia nchi bila kuingia katika hayo ulliyoyataja hapo juu mharakati? Angalau kupunguza kwa kiasi kikubwa na kutufanya tu-apreciate hilo na kulichukua kama mfano. ninani atakaetawala nchi hii bila kujali itikadi, wala hulka ya mtu nani? nnani ambaye atatawala nchi na sio chama na kuwafanya upinzani kuwa watu wengine na kusahau kuwa ni raia wake pia? Nani na tutaamnije kuwa atatekeleza hayo. Nani anaeipenda nchi yake kwa ukweli ambaye si mbinafsi akiguswa na kwa uchungu moyoni mwake (bila kuigiza kwa kuvaa matamabara eti anajali masikini)
   
 11. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  kwenye red hapo naafikiana na wewe kabisa, ila si rahisi kama unavyofikiri jasusi, tuna wakati mgumu sana, labda tuwe tayari kuingia gharama za kipindi cha mpito na kipindi hicho lazima kiwe na kiongozi anaekubalika na wengi hata kama huduma nyingi zitadidimia na hali kuyumba kutokana na subortage ya hali ya juu inayoweza kufanywa na hao wanaotamani rasilimali zetu basi watu wawe tayari wasianze kutaka kumng'oa. Unaona yanayotokea Zimbabwe? Tanzania tuliwasupport lakini unajua nini, ilikuwa kisiasa sisi wenyewe hatukuwa na hatu akama zao, sawa tulirekebisha sheria ya ardhi ambayo ni nzuri kwakweli kimsingi (inategemea na mtizamowako katika usimamizi wa ardhi, maana ninashida pale tu inapopelekea watu kuondolewa kwenye maeneo yao ya asili, au Wamasai wanapozuiwa kundeleza tamaduni zao za ufugaji huria, na fidia zinapokuwa hazileti mabadiliko yeyote kwa yule aliyekuwepo pale akiwa anaishi kimaskini juu ya utajiri wa ajabu na kundelea kuachwa fukara).

  Jasusi nimesoma katiba ya CHADEMA, ninafuatilia mikutano yao na hata ya vyama vingine, nina hamu ya kuiona ilani ya CHADEMA ya uchaguzi ujao. Msifanye kosa 2015 bado kuna muda wa kutosha CCM hawajalala, na kama kuna kitakachotokea basi kitakuwa pale juu kwenye uongozi, nadhani wote tuna ushahidi wa mikikimikiki ambay ninawapongeza mmejitahidi kuidhibiti. Ila pakipanguka hapo kuu, dah siombei yale ya NCCR-Mageuzi na vyama vingine maana baadhi yao wamo humo tena kwenye nafasi za juu tu.

  CCM kweli kuna tatizo kubwa sana sana tu, labda itakuwa vema kuwaweka penmbeni wajipange upya, nadhani labda itakuwa dawa ili kupunguza kiburi walichonacho. Ila ninapenda kushawishika kuwa huyu ambaye tutamuwek madarakani basi apangue kikwelikweli Dira tunayoitaka si kutumia udhaifu wa CCM kumng'oa, kwakuwa kuchukua madaraka ni moja, kutupeleka tunakotaka ni jambo lingine. Ninafurahishwa na baadhi ya halmashauri mlizozishikilia, lakini mnajua CCM wanachojaribu kuwafanyia kila wakati, watakapokuwa upinzani vurugu hizo hazitakoma maana nao watakuwa wanatafuta kuingia madarakani.
   
 12. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  I do agree without reservations to all these situations, and CHADEMA nyinyi kama wanachama hameni kwenye ushabiki na musimamie miakakati na kushawishi utekelezaji wake utatupeleka wapi, otherwise sitashangaa mkiingia mkawa even worse than the CCM, ni kwa nia njema kabisa maana huko CHADEMA ki=una wadogo zangu na wajomba zangu
   
 13. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2013
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Sisi kama wachambuzi na wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa na uongozi kwa ujumla wake ndani ya Taifa letu hili, tuna kila sababu ya kurejea kwenye madai ya chama cha Chadema kuwa CCM ipo ipo tu! Haijijui wapi inatoka na wapi inakwenda japo ipo kwenya mamlaka!


  Nasema hivyo kutokana na ukweli wa hili tamko la Serikali la kufuta matokeo ya mutihani wa kidato cha Nne. Chedema wamekuwa wakilalamika kwa nguvu zote kuwa utawala uliopo madarakani unatuvurugia nchi na kuwageuza watoto wetu kuwa vipofu kutokana na kutokuwa na mfumo wa elimu unaoeleweka, lakini wamekuwa wakibezwa.

  Sasa maamzi haya ya kufuta matokeo yanamaanisha nini??

  TAFAKARI.
   
 14. O

  OSHABU Senior Member

  #14
  May 3, 2013
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Pamola na hayo yote mi binafsi ninapongeza hatua za kufutwa kwa matokeo hayo, kwasababu yalishaanza kuniathiri.Ninawadogo zangu wanee wamwmalioza na wote wamepata div 4 karb na zero, kwa matokeo yale hata ualimu wasingeenda,kwasasa nashusha pressure. Kwa hili mi napongeza,japo wangeweza kuzuia toka zamani.
   
 15. F

  FUSO JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  CDM inarudia rudia tu kutukumbusha sisi watanzania kwamba CCM haina Dira wala mwelekeo, kauli hii iliyowahi kutolewa kwa mara ya kwanza na kiongozi wa juu kabisa wa chama cha mapinduzi miaka ya 1990.

  Toka wakati huo CCM imekuwa ikibisha tu bila kuwahakikishia watanzania kwamba hawana mwelekeo, lakini ki uhalisia ndugu zangu kauli ile inalenga ukweli mtupu na itabakia kuwa HAI. (R.I.P H.Kolimba)
   
 16. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,096
  Likes Received: 1,708
  Trophy Points: 280
  Umeanzisha ujinga halafu unauchangia mwenyewe kwa multiple id zako
   
 17. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,096
  Likes Received: 1,708
  Trophy Points: 280
  Mleta mada nakushauri uwasiliane na dr kigwangalla anatibu ugonjwa wako a hana gharama kubwa
   
 18. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,096
  Likes Received: 1,708
  Trophy Points: 280
  Kwa mtu mwenye akili zake timamu hawezi kufanya siasa uchwara kama hizi za kwako
   
 19. Kennedy Daima Mmari

  Kennedy Daima Mmari Verified User

  #19
  May 3, 2013
  Joined: Dec 12, 2012
  Messages: 981
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  nyie magamba mbona mnawashwa namna hiyo?kama vile mnatarajia kujifungua...hebu tulieni,mdeal na content ya mtoa mada na sio kumfanyia personal attacks
   
 20. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2013
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Mwathirika sio wewe tu na hata suala la kurudiwa mitihani hiyo hakuna anayelipinga kwani watoto wetu walidhurumiwa haki zao. Lakini bado tujiulize,
  1. ni nani wa kubeba gharama za upuuzi huo kama sio mimi na wewe?!

  2. Kwanini watanzania tusifike mahala tukaanza kutambua kuwa kila senti ya serikali inayotumika inachomolewa kutoka mifukoni mwetu! Hivi ni wangapi wanaojiuliza hilo?

  3. Na wale watoto wetu waliopoteza maisha kutoka na kupata mshituko uliotokana na matokeo hayo machafu, nani atarudhia uhai wao?

  4. Je, tuna hakika gani kwamba ile spirit ya masomo waliyokuwa nayo mwanzo bado wanayo, tutashangaa kama wakifanya vibaya zaidi kuliko hata mwanzo?

  5. Maswali ni mengi jiongeze>>...........................................................
   
Loading...