Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Aliyekuwa diwani wa kata ya kaloleni kupitia CHADEMA inasemekana anatafutwa na Polisi kwa tuhumu za kumtapeli mwekezaji mwenza kwenye biashara yao ya utalii. Charles David Mpanda (Rasta) anadaiwa kumtapeli Margaret Lema kiasi cha Dola 16,400 kutoka kwenye akaunti yao ya pamoja.
Hili jambo limenifanya nifikirie upya siasa za bongo. Margaret ni Mdogo wake God bless Lema Mbunge wa Arusha Mjini kwa maana nyingine yale yanayotokea CCM kwa watu wa ukoo mmoja kumiliki chama yanatokea na CHADEMA pia. Mbowe kaoa mtoto wa Edwin Mtei Muasisi wa CHADEMA, Lucy Owenya mbunge wa viti maalum ni mtoto wa Philimon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini.
Ukikutana na Rose Kamili Mbunge wa viti maalum ujue ni mzazi mwenzie Dr. Wilbroad Slaa pia ujue kwamba ukikutana na Christina LIssu ni Mdogo wake na Tundu Lissu, na Moulida au Anna Komu Mbunge Viti maalum ni Mke wa mkuu wa Idara ya fedha Makao Makuu CHADEMA, Anthony Komu. Hawa ni wale wanaohusiana kimapenzi na kiukoo hatujui wale wanaohusiana kimaslahi kama vile kibiashara wako wangapi na kwenye ngazi zipi. Lakini jambo hili kwa sababu limetokea CDM basi litatetewa weeee hadi mijasho itukauke.
Aliyekuwa mkuu wa upelelezi Kanda Maalum ya Dar es salaam Abdalah Zombe alidai kwamba Godbless Lema alikuwa ni mwizi wa magari. Sijaona mcharuko mkubwa angalau wa kumshinikiza Zombe aseme anavyojua wizi wa magari wa Lema wala wa kumshinikiza Lema kueleza historia yake ya nyuma kabla hajawa Mbunge inahusiana vipi na wizi wa magari. Wote tuko kimyaa kwa sababu ni mtoto wa nyumbani. Rage kuonyesha Bastola ilikuwa nongwa lakini la Lema ni "Uzushi' wa magamba.