Siasa za CCM zinawavuruga CHADEMA

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Ni ukweli kuwa CCM ni magwiji katika kuzicheza siasa za kuwajaza matumaini hewa CHADEMA na hasa kundi la vijana wa CHADEMA.

CCM wanacheza na siasa za CHADEMA ambazo kwa kiasi kikubwa kwa sasa zimejikita katika UDAKU.

Mara nyingi Edward Lowassa amesikika akiwaasa viongozi wa CHADEMA waachane na siasa za UDAKU kwa sababu ni siasa ambazo sio endelevu hasa katika chama ambacho kinataka kuchukua dola.

CHADEMA walishangilia sana baada ya Wema Sepetu kuhamia CHADEMA huku wakidai ni shujaaa kwa sababu kitendo alichokifanya ni cha kishujaa.

Tulimuona Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe akiambatana na Wema Sepetu sehemu mbali mbali. Hata Godbless Lema na Halima Mdee hawakubaki nyuma katika safari hizo.

CHADEMA hawakujua walichokuwa wanakifanya hakina tofauti na kutengeneza silaha ambayo itawaua wao wenyewe.

CHADEMA ‘’waliwashadadia’’ na kuwasifia Nape Nnauye na Hussein Bashe lakini lilipofika suala la kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Madiwani, CHADEMA walipata jibu sahihi.

Kwa maelezo zaidi pitia hii thread;
Nape na Bashe wamewapa CHADEMA somo la siasa za CCM

CHADEMA hawakujua kuwa kuna Wahenga Walinena; Ndugu Wakigombana, Chukua Jembe Ukalime...!

CHADEMA hawakujua kuwa ugomvi wa Wema Sepetu na CCM ulikuwa ni sawa na ndugu wanaogombana.

Wema anawaumbua CHADEMA baada ya ugomvi wake na Paul Makonda kumalizika.

CHADEMA wamebaki kurusha matusi na kejeli bila kujua kuwa tatizo sio Wema Sepetu bali ni siasa wanazofanya za kushadadia UDAKU wa Instagram na majungu.

Leo Wema amerusha picha akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wanapata upepo mwanana wa Dar huku akimsifia Makonda.

CHADEMA wataendelea kuvurugwa na CCM mpaka pale watakapoachana na siasa za UDAKU kutoka Instagram.

Hatutashangaa kuona kuna mwingine tena waliyemsifia sana atatoka CHADEMA na kujiunga na CCM au yule waliomzodoa kuwa fisadi akiwa CCM atajiunga na CHADEMA.

Picha ya Paul Makonda akiwa pamoja na Wema Sepetu.
wema na makonda2.jpg
 
Huyo mgawa papuchi nae akija Na kuondoka anaumiza vichwa watu?
Alikuwa analia lia hovyo mpaka akaonewa huruma Na tundulissu Na kibatala kuhusu Huyo makonda leo ndo makonda amekuwa mzuri!!

Kweli mwanamke mzuri sehemu zake za siri ndio zitakazoumia!!
 
Kila kukicha wanacheza ngoma ya CCM bila kujua!

Msemajiukweli sikuwahi kutarajia kuwa una mitazamo myepesi hivi. Hapo cdm wamechezeshwa vipi na siasa za ccm? Huyo Wema sio ndio alituhumiwa na mambo ya dawa za kulevya na hata hivi tunavyoongea ana kesi ya bangi? Aliyekuwa akiendesha vita hiyo si huyohuyo Makonda? Sasa hapa utatupa ujumbe gani kwa wale mliotuaminisha kwamba Makonda anapambana na madawa ya kulevya?
 
Huyo mgawa papuchi nae akija Na kuondoka anaumiza vichwa watu?
Alikuwa analia lia hovyo mpaka akaonewa huruma Na tundulissu Na kibatala kuhusu Huyo makonda leo ndo makonda amekuwa mzuri!!

Kweli mwanamke mzuri sehemu zake za siri ndio zitakazoumia!!
Aya ni maneno ya mkosaji nenda kwenye hoja sio kufanya vioja,kwani mlipompoke hamkujua aya yote!Hii ni sawa na kusema sizitaki mbichi hizi
 
Back
Top Bottom