marcus rojo
JF-Expert Member
- Mar 19, 2017
- 1,496
- 5,320
WANYAMA APEWA MTAA DAR
Anaandika Ezekiel Kamwaga
_________________________________________
Mwacheni Victor Wanyama apewe MTAA!
Sisi Watanzania ni watu wa ajabu kidogo. Leo Wanyama kapewa Mtaa hapa Dar es Salaam ba watu wameanza kulalamika tayari. Kwanini tunapenda kulaumu wanaotbubutu?
Hivi, kumpq mtaa Victor Wanyama kunazuia nini kumpa mtaa Mbwana Samatta, Filbert Bayi au Juma Ikhangaa? Kuna mitaa mingapi haina hata majina Dar, Mwanza, Arusha, Mbeya na kwingineko?
Wanyama anacheza UK. Kaja TZ. Akina David Beckham wamekuja TZ Na hawakutaka hata wajulikane kama wako hapa. Christian Eriksen yuko hapa hataki ajulikane. Everton wanakuja na kuna washabiki wao tayari wanalalamika kuwa wachezaji wao wataambukizwa Ukimwi kwa kuja kwao TZ.
Victor kaja kwetu. Kaenda Clouds, kala Triple 777, kaenda East Africa Radio. Leo mimi mwenyewe nimemuona pale Azam TV. Anaongea KISWAHILI kama sisi wote.
Kwanini tumeamia kuwa na mtizamo finyu sana kuhusu Tanzania na UTANZANIA? MTANZANIA anatakiwa kuwa yoyote mwenye.mapenzi na nchi yetu na si lazima azaliwe hapa.
C'mmon, huyu Wanyama hadi kakutana na Saida Karoli na kuchukua kazi zake. Ni supastaa gani wa Tanzania ambaye ameonyesha hadharani kukubali kazi za Saida Karoli? Wanyama amezungumza na kuonyesha vitendo.
Kama Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, ameamua kumpa mtaa katika Manispaa yake, anatakiwa kupongezwa kwa ubunifu na UTHUBUTU wake.
Inawezekana Kenya hawajampa Wanyama heshima hiyo na Ubungo wamemuwahi. Jambo hili litabaki kwenye kumbukumbu ya Victor kwa muda mrefu na Mungu anajua ni namna gani atalipa fadhila hii.
Watanzania wenzangu, ifike wakati tuwe tunapongeza mema yanayofanywa. Kwenye macho yangu, VICTOR WANYAMA ni Mtanzania kuliko wengi ambao UTANZANIA wao ni kuzaliwa hapa tu.
Hongera Meya Boniface Jacob kwa UTHUBUTU na UBUNIFU!!!!
Eze
________________
[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]: Kamwaga ameeleza yote niliyotaka kueleza. Thanks bro. Kuna watu tangu jana naona wanahemka na kuhusu Wanyama kupewa mtaa. Wanahoji mbona Samatta hajapewa. Jibu ameeleza Ezekiel hapo juu. Ni kwamba Wanyama kupewa mtaa haizuii Samatta kupewa. Tanzania haina mtaa mmoja tu usio na jina. Ipo mingi. Tuchukue mmoja tumpe Samatta. Hakuna sababu ya kulalamika.
Angalau Boniface Jacob ameonesha ubunifu wa hali ya juu. Mameya wengine wanashindwa nini? Badala ya kumlaumu Bonny aliyethubutu, kwanini msiwalaumu hao mameya wengine ambao hawajathubutu kabisa?
Wakenya wamekuwa wakitu-outsmart kwenye vitu vingi tunaishia kulalamika tu. Waliwahi kusema mlima Kilimanjaro upo kwao, tukalialia. Majuzi wakaiambia dunia kuwa Olduvai ipo kwao, tukaendelea kulia. Tukajilaumu kuwa hatuna ubunifu ndio maana Wakenya wanatuwahi. Sasa leo tumewawahi Wakenya. Tumewapiga counter attack. Tumewaoutsmart. Tunaanza tena kulaumiana??
Wakenya kabla hawajafikiria kumpa Wanyama mtaa huko kwao sisi tumeitangazia dunia kwamba Wanyama ana mtaa Tanzania. Katika historia ya maisha ya Wanyama atakumbuka kuwa mtaa wa kwanza kupewa upo Tanzania, manispaa ya Ubungo. Hii ni habari njema sana kwetu kimataifa na ni habari mbaya sana kwa wakenya. Kwa mara ya kwanza tumewa-outsmart Wakenya katika jambo kubwa lenye msisimko kimataifa. Halafu eti bado kuna watu wanalalamika? Wendawazimu.!!
Kukasirika eti Kwanini Wanyama kapewa mtaa na sio Samatta haikufanyi kuwa mzalendo bali inakufanya kuwa Zwazwa. Kama Bonny amempa mtaa Wanyama apongezwe kwa ubunifu huo, halafu Mameya wengine washauriwe kwamba nao waamke watoe majina ya mitaa kwa mashujaa wetu kina Samatta, Filbert Bayi, Diamond, Remmy Ongala etc.
Yani mlitaka Samatta, Faru John, Sokoine, Ali Kiba, Marijani Rajab, Juma Pondamali etc wote wapewe mitaa manispaa ya Ubungo kisa Wanyama amepewa?? Acheni uzwazwa. Hii nchi ina manispaa ngapi? Ina mitaa mingapi isiyo na majina? Kwani wote lazima wapewe Ubungo? Kwanini wakati Bonny anampa Wanyama mtaa Ubungo, mameya wengine wasichangamke kuwapa mashujaa wetu wengine mitaa kwenye manispaa zao??
Mtu akifanya jambo zuri anastahili kupongezwa na wengine washauriwe waige. Hongera Mstahiki Meya Bonny. Hongera Wanyama. Wewe ni mfano wa kuigwa. Unacheza ligi kuu ya Uingereza lakini umekuja kushuhudia "Ndondo cup" Tanzania. Kenya kuna ligi za mchangani kama ndondo lakini hukwenda, umekuja hapa.
Umekutana na Saida Karoli umenunua kazi zake. Kenya kuna akina "Saida Karoli" wengi lakini umeamua kuanza na huyu wa kwetu. Wale wa Kenya wasubiri kwanza. Umetangaza mbuga zetu za wanyama. Kenya zipo mbuga nyingi lakini umeamua kuanza na za kwetu, za Kenya zisubiri kwanza. Umetembelea media house za Bongo kama Clouds, Azam etc. Kenya kuna media house nyingi lakini umeanza na za Kwetu. Za Kenya zisubiri kwanza.
Wewe si Mtanzania lakini umefanya zaidi ya Watanzania wengi. Ni ajabu "mazwazwa" yanaojiita watanzania wameshindwa kuona yote hayo wamebaki kulaumu kwanini umepewa mtaa. Wewe ulitakiwa upewe hata wilaya sio mtaa tu. Tungekua na mamlaka tungebadilisha hata ile "Chato" iwe Halmashauri ya wilaya ya Wanyama. Kwani nini? Jambo zuri lipongezwe na litutie hamasa.
Hawa wanaolialia kwanini Wanyama kapewa mtaa na ni Mkenya niwaulize imekuaje I dira Ghandi, Sam Nujoma, Kwame Nkurumah, Keneth Kaunda etc wamepewa mitas Tanzania. Hivi hawa wanatoka wilaya zipi za Tz? Vitu vingine ni kujichosha akili tu.
Narudia kusema kwamba Wanyama kupewa mtaa haizuii Samatta kupewa mtaa. Haizuii Diamond na Ali Kiba kupewa mitaa. Haizuii Faru Filbert Bayi na Bi Kidude kupewa mitaa. Hawa wote ni mashujaa wetu.
Tumeanza na Wanyama kwa kuapply ile theory ya uchumi ya "Opportunity cost" kwamba "do the fast thing first." Bonny kaanza na Wanyama, apongezwe then Mameya wengine washauriwe kuiga mfano wake. Watoe majina ya mitaa kwa mashujaa wetu wa ndani, sio kulaumiana.
Malisa GJ