Siasa sio Uadui, Gambo na Lema wapiga picha pamoja

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
WAGOMBEA Ubunge Arusha Mjini, Mrisho Gambo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Godbless Lema wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekutana katika mgahawa wa Safari Bistro jijini humo.

Wawili hao ambao wamekuwa na mchuano mkali kuwani jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 wamekutana mgahawani hapo leo Jumanne 29 Septemba 2020.

Lema anatetea jimbo hilo ambalo ameliongoza kwa miaka kumi mfululizo huku Gambo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akijitosa kwa mara ya kwanza kutaka kurejesha jimbo hilo chini ya himaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wanasiasa hao, wamepiga picha kadhaa wakiwa kwenye mgahawa huo na kila mmoja ameiweka kwenye kuraza zake za mitandao ya kijamii na kuiandikia maelezo ya kufarijiana kwa kile kitakachotokea baada ya uchaguzi mkuu.

“Leo tumekutana mbunge ninaeingia madarakani na mbunge aliyemaliza muda wake! Ameniambia kuwa hajawahi kuwa na uchaguzi mgumu kama mwaka huu na amejiandaa kisaikolojia.”

“CCM ni chama kubwa hatuwezi kukosa kazi ya kumpa. Hakika nyumbani kumenoga!,” ameandika Gambo

Wakati Gambo akiandika hivyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, mshindani wake mkubwa Lema, ameweka picha Instagram na kuandika “nimekutana na huyu kijana hapa Safari Bistro cafe… akaomba picha, nikasema ni sawa tu, kwani akose Ubunge hata na picha na mimi wajameni…hali yake ni ya majonzi sana.”

1601392371652.png
 
Hongera kwao salam ziwafikie Magu na team yake. Natamani Magu kule Kigoma angemjengea mazingira Lissu, wafanye selfie, Ingempa faraja Lissu kupunguza sumu moyoni.
 
Hii picha pengine imechukua chini ya dakika mbili lakini amini kwamba imebandika mawazo mapya kwa wengi mojawapo ni "Kumbe tunaweza kuiva pamoja"
 
WAGOMBEA Ubunge Arusha Mjini, Mrisho Gambo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Godbless Lema wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekutana katika mgahawa wa Safari Bistro jijini humo.

Wawili hao ambao wamekuwa na mchuano mkali kuwani jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 wamekutana mgahawani hapo leo Jumanne 29 Septemba 2020.

Wanasiasa hao, wamepiga picha kadhaa wakiwa kwenye mgahawa huo na kila mmoja ameiweka kwenye kuraza zake za mitandao ya kijamii na kuiandikia maelezo ya kufarijiana kwa kile kitakachotokea baada ya uchaguzi mkuu.

“Leo tumekutana mbunge ninaeingia madarakani na mbunge aliyemaliza muda wake! Ameniambia kuwa hajawahi kuwa na uchaguzi mgumu kama mwaka huu na amejiandaa kisaikolojia.”

“CCM ni chama kubwa hatuwezi kukosa kazi ya kumpa. Hakika nyumbani kumenoga!,” ameandika Gambo

Wakati Gambo akiandika hivyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, mshindani wake mkubwa Lema, ameweka picha Instagram na kuandika “nimekutana na huyu kijana hapa Safari Bistro cafe… akaomba picha, nikasema ni sawa tu, kwani akose Ubunge hata na picha na mimi wajameni…hali yake ni ya majonzi sana.”

View attachment 1584659
Gambo akishindwa na Lema atafukuzwa kwenye chama kwa usaliti
 
Jambo jema sana, yule mwingine anayewatisha watu kua hataleta maendeleo sehemu ambayo watachagua upinzani anajiskiaje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom