siasa ndo biashara inayolipa fasta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

siasa ndo biashara inayolipa fasta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Oct 27, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  si jambo la ajabu kwa wasomi, wanataaluma na wataalamu wa fani mbalimbali kujitumbikiza kwenye siasa. mfano raisi obama na aliyekuwa wazri mkuu wa Uingereza tony blair na rais Eisenhower alikua jenerali. Pengine cha ajabu kwa hapa kwetu ni jinsi ambavyo kumekuwa na mkusanyiko mkubwa wa kundi hili la wasomi wanataaluma na wataalamu mbalimbali kukimbilia siasa hadi kufika mahala bunge letu lina madaktari mabigwa wa tiba mfano sarugi, chiduo na kadhalika hadi sasa tunae mwakyusa.

  Wapo madaktari wa falsafa na wataalum wa fani zao kama profesa mwandosya na wapo mainjinia. orodhani ndefu mno. je nini kinawapeleka wote hawa kukimbilia bungeni? ni wito wa kuwatumikia wananchi au sisa imekua kimbilio lao katika muda huu wa lala salama?

  Pengine swali kubwa la kujiuliza: jamii inafaidika nini kwa kundi hili kuacha taaluma zao na kwenda kwenye siasa? daktari bigwa anapohitajika zaidi kwenye wito wake wa udaktari na kwenda kwenye siasa anawatendea haki wananchi? pamoja na kua na katiba ya nchi inampa haki hiyo? faida na hasara ni zipi kwenya jamii? mfano profesa sarugi alihitajika zaidi akiwa bingwa wa tiba ya mifupa kuliko kama yeye kuwa mbunge.

  Daktari bingwa unafuata nini kwenye siasa? unataka upate nini zaidi ya ubigwa na sifa inayotokana na ubigwa wako? kama ni tamaa ya kuwa waziri huo ni ubinafsi ambao tayari tunauona na kuushudia kwa wanasiasa wetu. malalamiko ya wanaokosa uwaziri ni mengi. tunaona zaidi ya yote ni ubinafsi unaowasukuma baadhi ya wanatalaaluma kijitumbukiza kwenye siasa.

  Tumefika mahali mwanataaluma akishaingia kwenye siasa, basi hata fani yake anaisahau kabisa. kama ni daktari anausahau kabisa udaktari wake. kama ni profesa basi uprofesa wake haupo tena! anabaki kua profesa jina tu lakini, taaluma keshaitupa mkono na sio profesa wa usomi hapa ndipo tulipofika.
   
Loading...