Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 42
Tangu enzi za Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani, Mrema alitangaza kuwa Kambona hakuwa raia wa Tanzania na kuwa atakamatwa uwanja wa ndege akitokea uhamishoni. Salim Ahmed Salim naye alikuwa akipakaziwa katika kampeni za kuwania urais kwa tiketi ya CCM kuwa alikuwa ni raia wa Saud Arabia. Generali ulimwengu aliambiwa siyo raia wa Tanzania baada ya kumkosoa Mkapa. Mtikila naye akazusha ya kwake kuwa Nyerere hakuwa raia wa Tanzania na kuwa ni raia wa nchi jirani na Tanzania. Kuna makamu wa BMT aliwahi kufukuzwa nchini kuwa hakuwa raia wa Tanzania. Bashe na Mkullo nao wanasemekana siyo raia wa Tanzania. Pia Mkapa aliwahi kuandamwa na wanasiasa kuwa ni raia wa Msumbiji. Rostam Aziz naye anasemekana ni raia wa Iran. Unaweza kujaza kurasa kuelezea visa vya wanasiasa au nafasi za uongozi na uraia. Kwa nini idara ya uhamiaji isifanye kazi yake barabara kuanzia huko wanakoishi wananchi?. Hivi sasa inaonekana masuala ya uraia yanatiliwa mkazo kwenye suala la kugombea uongozi. Kinachotakiwa ni idara ya uhamiaji itoe elimu ya uraia ili raia wajue haki zao na kulinda usalama wa nchi kwa kuzuia wahamiaji haramu. Suala hili ni muhimu kwa haki na wajibu wa Watanzania, usalama wa Taifa na ulinzi wa mali za Watanzania. Uhamiaji na serikali tekelezeni sera na sheria za uhamiaji vema vinginevyo uraia unaonekana kutumika kama mtaji katika siasa.