Siasa na uraia nani alaumiwe?

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Tangu enzi za Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani, Mrema alitangaza kuwa Kambona hakuwa raia wa Tanzania na kuwa atakamatwa uwanja wa ndege akitokea uhamishoni. Salim Ahmed Salim naye alikuwa akipakaziwa katika kampeni za kuwania urais kwa tiketi ya CCM kuwa alikuwa ni raia wa Saud Arabia. Generali ulimwengu aliambiwa siyo raia wa Tanzania baada ya kumkosoa Mkapa. Mtikila naye akazusha ya kwake kuwa Nyerere hakuwa raia wa Tanzania na kuwa ni raia wa nchi jirani na Tanzania. Kuna makamu wa BMT aliwahi kufukuzwa nchini kuwa hakuwa raia wa Tanzania. Bashe na Mkullo nao wanasemekana siyo raia wa Tanzania. Pia Mkapa aliwahi kuandamwa na wanasiasa kuwa ni raia wa Msumbiji. Rostam Aziz naye anasemekana ni raia wa Iran. Unaweza kujaza kurasa kuelezea visa vya wanasiasa au nafasi za uongozi na uraia. Kwa nini idara ya uhamiaji isifanye kazi yake barabara kuanzia huko wanakoishi wananchi?. Hivi sasa inaonekana masuala ya uraia yanatiliwa mkazo kwenye suala la kugombea uongozi. Kinachotakiwa ni idara ya uhamiaji itoe elimu ya uraia ili raia wajue haki zao na kulinda usalama wa nchi kwa kuzuia wahamiaji haramu. Suala hili ni muhimu kwa haki na wajibu wa Watanzania, usalama wa Taifa na ulinzi wa mali za Watanzania. Uhamiaji na serikali tekelezeni sera na sheria za uhamiaji vema vinginevyo uraia unaonekana kutumika kama mtaji katika siasa.
 
Tangu enzi za Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani, Mrema alitangaza kuwa Kambona hakuwa raia wa Tanzania na kuwa atakamatwa uwanja wa ndege akitokea uhamishoni. Salim Ahmed Salim naye alikuwa akipakaziwa katika kampeni za kuwania urais kwa tiketi ya CCM kuwa alikuwa ni raia wa Saud Arabia. Generali ulimwengu aliambiwa siyo raia wa Tanzania baada ya kumkosoa Mkapa. Mtikila naye akazusha ya kwake kuwa Nyerere hakuwa raia wa Tanzania na kuwa ni raia wa nchi jirani na Tanzania. Kuna makamu wa BMT aliwahi kufukuzwa nchini kuwa hakuwa raia wa Tanzania. Bashe na Mkulo nao wanasemekana siyo raia wa Tanzania. Pia Mkapa aliwahi kuandamwa na wanasiasa kuwa ni rais wa Msumbiji. Rostam Aziz naye anasemekana ni raia wa Iran. Unaweza kujaza kurasa kuelezea visa vya wanasiasa au nafasi za uongozi na uraia. Kwa nini idara ya uhamiaji isifanye kazi yake barabara kuanzia huko wanakoishi wananchi. Hivi sasa inaonekana masuala ya uraia yanatiliwa mkazo kwenye suala la kugombea uongozi. Kinachotakiwa ni idara ya uhamiaji isitoe elimu ya uraia ili raia wajue haki zao na kulinda usalama wa nchi kwa kuzuia wahamiaji haramu. Suala hili ni muhimu kwa haki na wajibu wa Watanzania, usalama wa Taifa na ulinzi wa mali za Watanzania. Uhamiaji na serikali tekelezeni sera na sheria za uhamiaji vema vinginevyo uraia unaonekana kutumika kama mtaji katika siasa.

Mkuu unauliza swali hili kama vile wewe si mtanzania. Ni idara gani Tanzania inafanya kazi yake barabara, sasa hivi watu wako busy na kujichumia pesa, hakuna aliyeonesha uzalendo wa kutosha kwa Tanzania. Kama ingekuwa hivyo ujinga wote tunaousikia usingekuwepo. Nafahamu watu wengi tu wasio watanzania, lakini ukienda kusema uhamiaji unaweza kushangaa mwenyewe unaingia jela. Jaribu kusema Rostam Aziz si mtanzania uone kitakachokukuta.
 
Hapo ndipo shughuli ilipo, usalama wa nchi yetu upo mashakani. Kunatakiwa mabadiliko makubwa sana ili nchi yetu ibaki salama.
 
Mkuu kuna mambo ya ajabu sana yanatokea siku hizi. Huwezi kuamini, kuna watu wengi sana wanatanua na passport za Tanzania nje ya Tanzania, wahindi kibao wanakuja toka India wanakaa Tanzania mwaka tu wanafanya ujanja na kupata passports za Tanzania wanaenda kuishi Canada, hawajui kiswahili hata siku ya uhuru wa Tanganyika, ajabu wengine hata Nyerere hawamjui. Kuna wengine wengi tu wamesoma shule za serikali, wengine mpaka wanaomba hata mikopo bodi ya mikopo na wengine wengi wanaomba visa hapahapa Tanzania kwenda nchi za nje kwa kutumia passport za Tanzania, nobody cares.

Kuna mambo mengi ambayo miaka 10 iliyopita yalikuwa unthinkable lakini sasa ni common knowledge. Zamani haikuwa rahisi majambazi kwenda kufanya uhalifu at our city centre, lakini sasa wanaweza kufanya hivyo even 500 meters kutoka Ikulu. sasa hivi wezi wanaweza hata kuiibia benki kuu na kuendelea kutesa mjini huku wakiwa na ulinzi juu. Hii inaonesha kuwa sasa hivi watu hawana interest na usalama wa Tanzania na wa watanzania. wanaangalia hela zao tu.
 
Nani wa kulaumiwa? Sisi Watanzania, idara ya uhamiaji au Serikali? Watanzania tufanyeje sasa?. Tuache mambo yaendelee kama yalivyo? Tukiacha mambo yaendelee hivi wajukuu zetu wataishi mazingira gani?.
 
Mkuu we are playing our part. Kwanza wewe kuanzisha thread hii it is part of playing your part. Wako watu wengi tu wa idara ya uhamiaji, am very sure kuwa wanasoma lakini they are not going to do anything, simple because they do not care. No doubt what we are facing now it is a result of being mute, Someone was mute in early 80's na matokeo yake tunayaona sasa.

Kuna watu wanatumia status za hawa watu kujichumia pesa. wanajua kuwa si raia halali lakini wanapokea malipo kila baada ya muda na kuwatunzia siri zao. In other words ni kama wanatuuza. Uzalendo umepungua sana, we are not working and fighting for Tanzania. we take it for granted. Tunatakiwa tupige kelele zaidi.
 
Hii ni kufirisika kisiasa kwa viongozi walioko madarakani. Law enforcement Tanzania ndo tatizo namba moja. Hakuna sheria inayotekelezwa kwa sababu serikali ni kama haipo. Ndo maana unaona hata mauaji ya kulipizana visasi inaaanza kuwa common knowledge Tanzania. Kwa sababu mtu akikufanyia faulo huna mahali pa kwenda, labda upambane naye kibinafsi. Na solution za kibinafsi ndo hizo unazoziona. Ukisema uende kwenye vyombo vya sheria Tanzania, you are doomed. Hakuna kinachoendelea.

Sasa ukija kwenye masuala ya uraia, nasema huku ni kufirisika kisiasa kwani si utekelezaji wa sheria. Hii kete ya uraia imekuwa ikitumiwa na wenye nguvu waliofirisika kisiasa kama mtaji wa kuwamaliza wale wanaohisi ni maadui zao. Hasa wale wanaotofautiana nao katika mchezo wa kutafuta maguvu ya kudhibiti mfumo wa uchotaji wa fedha za walipa kodi. Ingekuwa ni suala la utekelezaji wa sheria, tungeona mambo haya siku zote si wakati wa uchaguzi tu tena kwa watu fulani fulani. Kama ni utekelezaji wa sheria zoezi hili lingekuwa endelevu. Watu wanaoajiriwa Tanzania hakuna anayehakiki uraia. Kuna maeneo ya ajira hasa kwenye mahoteli wameajiriwa wageni kibao, tena wengi hawana hata makaratasi ya kuwaruhusu kuwepo nchini achilia ukweli kuwa si raia na wanaruhusiwa kufanya kazi ambazo raia wanaweza kufanya.

Sheria zetu za uraia imebaki ni kete ya mufilisi wa kisiasa kwa ajiri ya kuwaangamiza wale wanaowaogopa. Sheria zetu zinachafuliwa na kunajisiwa kila siku na hao wanaotakiwa wazitetee kwa kula rushwa. Unafikiri kwa nini hawa wanaotamkwa kuwa si raia wanakuwa ni watu ambao wameshapitia michujo mbali mbali ambayo ilitakiwa iwathibitishe kuwa ni raia au si raia lakini michujo haikufanya hivyo? Hao wanaosimamia hizo sheria hawalazimiki kuzifuata kila wakati kwani hata ikigunduliwa hawakuzifuata hakuna anayefanya chochote.

Kwa mfano, kutamka kuwa Bashe si raia halafu ushindwe kuwachukulia hatua watu wote walioshiriki kumfikisha hapo alipofika bila kudhibitisha uraia wake, ni uzumbukuku. CCM katika hatua mbali mbali walitakiwa wawe walijiridhisha kuwa huyu ni raia au siyo. Asingeweza kuwa mwanachama kwani masharti ya kwanza ni kuwa raia wa Tanzania. Ni hatua gani waliochukuliwa waliomwandikisha uanachama bila kumhakiki?? Utaona kuwa hii yote ni Ghilba, ni Hila, ni Fitna, uongo na uzushi. Wanakubali kuwa vyombo vyote havifanyi kazi hadi pale wanapotaka vifanye kazi. Vyombo vyote imebakia ni magenge ya kujikusanyia rushwa.

Hata kama una vithibitisho vyote kuwa wewe ni raia wakati wowote wanaweza kutangaza kuwa wewe si raia kwa sababu hawaziheshimu taasisi zinazotoa hivyo vithibitisho kwani wanajua kuwa hizo taasisi ni magenge ya wala rushwa tu. Kwa ujumla hii inatuambia kuwa Tanzania hatuna sheria isipokuwa ni pale tu wenye nguvu wanapoamua kufanya watafanya.
 
ah suala la uraia inabidi tukajihakiki vinginevyo waweza zushiwa jambo...hili suala limekuwa kama filimee (sinema) manake mi bado nakumbuka Balali ilisemekana ni Mmarekani na akazikwa huko(marekani)...kweli vyombo vya usalama vifanye kazi zao vinginevyo haponi mtu tukianza kuulizana uraia huko mitaani.
 
kujihakiki hakutasaidia chochote, kwani siku ukikaa on the wrong hand ya watawala hawatazitambua hizo document za kujihakiki kwa sababu hivi vyombo utakapaenda kujihakiki havina credibility yoyote mbele ya watawala, hasa pale vitakaposema tofauti na wanavyotaka.
 
Na sheria inaweza kuwa interpreted vyovyote na watawala kwani mahakama haitapewa nafasi. Kumbuka hizi ni tambo tu zitakazotumiwa kukuzuia kufanya kitu ambacho wenyewe hawataki ufanye.
 
tatizo pia ni mfumo mbovu wa kutunza kumbukumbu. rai hawana kitambulisho chochote kuutambua utaifa wao unategemea nini. nenda kenya au hata rwanda uone jinsi wanavyofanya kutambuana.eo ukiambiwa sio raia huna kitambulisho wala baba hana wala babu tabu tupu.
ndio maana watu wanatumia mwanya huo kuharibiana
 
Suala la uraia ni suala la msingi na nyeti sana kwa nchi yoyote. Sisi tunaitwa Watanzania kwa sababu ya uraia wetu. Ni suala la msingi la kujitawala na linahusiana na uhuru wa nchi yetu. Kama mfumo ulikuwa unafanya kazi kabla ya miaka ya 80 kwa nini isiwe sasa?. Lililo wazi ni kuwa watawala wa sasa si viongozi. Hawana la kujifunza kutoka serikali ya awamu ya kwanza kuhusu utaifa na utanzania wetu. Pia hawana cha kujifunza kutoka nchi zingine ambapo mifumo ya uraia inafanya kazi vizuri. Sasa tunahitaji kuweka uongozi mpya nje ya chama tawala cha sasa, uongozi utakaojali maslahi na usalama wa watanzania. Uongozi utakao tenganisha masula ya msingi ya nchi na siasa za vyama. Dr. Slaa kaonyesha njia, atarudisha utaifa wetu, uchungu kwa nchi yetu na atahakikisha usalama wa nchi yetu.
 
kujihakiki hakutasaidia chochote, kwani siku ukikaa on the wrong hand ya watawala hawatazitambua hizo document za kujihakiki kwa sababu hivi vyombo utakapaenda kujihakiki havina credibility yoyote mbele ya watawala, hasa pale vitakaposema tofauti na wanavyotaka.

Mkuu this is very interesting. Kuna watanzania wengi tu wana uraia wa nchi mbili lakini kwa kuwa wako upande wa serikali serikali iko kimya kabisa. Kuna wengine wengi tu huwa wanatangazwa na wanasemwa kuwa ni raia wa nchi nyingine, na hata uthibitisho unawekwa hapa lakini hakuna linalofanyika. Kuna wageni mpaka wamekuwa magavana wa Benki Kuu, wengine mpaka wakuu wa wilaya, walipojifanya kusimamia utaratibu wakatimuliwa na kuitwa wageni.

You can ask yourself kwanini mtu kama kinana is always low key, although yeye ni mmoja kati ya outstanding Tanzanians. Ametegeshewa bomu la uraia.

Kwa nakubaliana na unachosema kuna wakati ukiidifu CCM na serikali, au ukikaa kimywa wanapofanya madudu yao basi you are good. Hii ni TZ.
 
Unanikumbusha kauli ya Sumaye, ukitaka mambo yako yakunyokee jiunge CCM. Lakini ni mambo gani yanawanyokea watanzania. Maisha ya watanzania yanazidi kudorora sababu ya ndiyo kwa chama tawala. Tupige hatua watu wajue kuwa tafsiri ya Mtanzania ni zaidi ya wanachama wa chama tawala na hatuwezi kuendelea kuishi maisha ya ''uwana mtandao'' Huu ni ubinafsi ambao hauisadii nchi yetu.
 
Mkuu unauliza swali hili kama vile wewe si mtanzania. Ni idara gani Tanzania inafanya kazi yake barabara, sasa hivi watu wako busy na kujichumia pesa, hakuna aliyeonesha uzalendo wa kutosha kwa Tanzania. Kama ingekuwa hivyo ujinga wote tunaousikia usingekuwepo. Nafahamu watu wengi tu wasio watanzania, lakini ukienda kusema uhamiaji unaweza kushangaa mwenyewe unaingia jela. Jaribu kusema Rostam Aziz si mtanzania uone kitakachokukuta.
Bongolander, kumbe unaelewa system iliyopo Tanzania....kwa upuuzi kama huu ambao umetawala katika serekali ndio maana nashindwa kufahamu hawa watu wanao itawala Tanzania wana imani kweli na nchi yao? Mimi nimepata bahati ya kuishi nje ya Tanzania kwa miaki mingi sana ,sijawahi kuona mambo kama haya popote pale. wenzetu kila raia anjua haki yake na kila raia anajua umuhimu wa kuilinda nchi yake. Sisi bongo tunaishi kama wadudu tu, viongozi na raia wa kawaida wote tuko kundi moja. Ndio maana naona wanzanzibar wanafanya cha maana kutaka kuwa kivyao... kwasababu huu utawala mbovu unarudisha watu nyuma ...kama wazanzibari watakua na nchi yao basi naamini watapiga hatua haraka sana...na hii labda inaweza kutuokoa sisi... kwasababu hawa viongozi wetu hawatakua na visingizio tena.
 
ndio maana wanachelewesha kutoa National Identity Cards, kumbe
hawamjui nani ni raia na nani si raia.
 
Bongolander, kumbe unaelewa system iliyopo Tanzania....kwa upuuzi kama huu ambao umetawala katika serekali ndio maana nashindwa kufahamu hawa watu wanao itawala Tanzania wana imani kweli na nchi yao? Mimi nimepata bahati ya kuishi nje ya Tanzania kwa miaki mingi sana ,sijawahi kuona mambo kama haya popote pale. wenzetu kila raia anjua haki yake na kila raia anajua umuhimu wa kuilinda nchi yake. Sisi bongo tunaishi kama wadudu tu, viongozi na raia wa kawaida wote tuko kundi moja. Ndio maana naona wanzanzibar wanafanya cha maana kutaka kuwa kivyao... kwasababu huu utawala mbovu unarudisha watu nyuma ...kama wazanzibari watakua na nchi yao basi naamini watapiga hatua haraka sana...na hii labda inaweza kutuokoa sisi... kwasababu hawa viongozi wetu hawatakua na visingizio tena.

Wazanzibari tena? Umeoa huko Mkuu? umesahau nao hivi karibuni walitaka kuwatolea nje wangazinja kwa sababu zile zile zinazotumiwa na wenzao wa bara?

Amandla.....
 
Mkuu kuna mambo ya ajabu sana yanatokea siku hizi. Huwezi kuamini, kuna watu wengi sana wanatanua na passport za Tanzania nje ya Tanzania, wahindi kibao wanakuja toka India wanakaa Tanzania mwaka tu wanafanya ujanja na kupata passports za Tanzania wanaenda kuishi Canada, hawajui kiswahili hata siku ya uhuru wa Tanganyika, ajabu wengine hata Nyerere hawamjui. Kuna wengine wengi tu wamesoma shule za serikali, wengine mpaka wanaomba hata mikopo bodi ya mikopo na wengine wengi wanaomba visa hapahapa Tanzania kwenda nchi za nje kwa kutumia passport za Tanzania, nobody cares.

Kuna mambo mengi ambayo miaka 10 iliyopita yalikuwa unthinkable lakini sasa ni common knowledge. Zamani haikuwa rahisi majambazi kwenda kufanya uhalifu at our city centre, lakini sasa wanaweza kufanya hivyo even 500 meters kutoka Ikulu. sasa hivi wezi wanaweza hata kuiibia benki kuu na kuendelea kutesa mjini huku wakiwa na ulinzi juu. Hii inaonesha kuwa sasa hivi watu hawana interest na usalama wa Tanzania na wa watanzania. wanaangalia hela zao tu.

Mkuu heshima mbele.

Mambo yalianza kubadilika mwishoni mwa miaka ya tisini ambapo kulianza kuwepo ufisadi katika kutoa passport za Tanzania kiholela ambapo "middlemen" walikuwa wengi.

Ilikuwa ukitaka passport kwa ajili ya kusafiri unamwona "middleman" ambae anakuhakikishia kuwa ndani ya masaa 24 utakuwa umepata passport hiyo bila matatizo yoyote yale.

Mimi nakumbuka nilipata passport yangu kwa muda wa wiki kama mbili hivi kwa kufuata utaratibu wa kujaza fomu na kuipeleka pale "home affairs" na pia baada ya kuzaja affidavit pale mahakama ya mwanzo kisutu na kulipa ada inayotakiwa.

Lakini kwa muda mrefu nikiwa ughaibuni ambako pia nilikuja kwa kufuata utaratibu nikiwa mtoto wa maskini, nimeshuhudia baadhi ya wasafiri wenzangu katika viwanja mbalimbali vya ndege wenye asili ya Asia au Somalia na hata baadhi ya nchi za Afrika magharibi, wakiwa wamebeba passport za Tanzania lakini kila nilipojaribu kuongea nao kiswahili wanashindwa kujibu hata neno jambo na habari tu.

Hali hii inatatiza sana na huko tunakoelekea tutakuwa na "very- very uncertain future".
 
Mkuu kuna mambo ya ajabu sana yanatokea siku hizi. Huwezi kuamini, kuna watu wengi sana wanatanua na passport za Tanzania nje ya Tanzania, wahindi kibao wanakuja toka India wanakaa Tanzania mwaka tu wanafanya ujanja na kupata passports za Tanzania wanaenda kuishi Canada, hawajui kiswahili hata siku ya uhuru wa Tanganyika, ajabu wengine hata Nyerere hawamjui. Kuna wengine wengi tu wamesoma shule za serikali, wengine mpaka wanaomba hata mikopo bodi ya mikopo na wengine wengi wanaomba visa hapahapa Tanzania kwenda nchi za nje kwa kutumia passport za Tanzania, nobody cares.

Kuna mambo mengi ambayo miaka 10 iliyopita yalikuwa unthinkable lakini sasa ni common knowledge. Zamani haikuwa rahisi majambazi kwenda kufanya uhalifu at our city centre, lakini sasa wanaweza kufanya hivyo even 500 meters kutoka Ikulu. sasa hivi wezi wanaweza hata kuiibia benki kuu na kuendelea kutesa mjini huku wakiwa na ulinzi juu. Hii inaonesha kuwa sasa hivi watu hawana interest na usalama wa Tanzania na wa watanzania. wanaangalia hela zao tu.
Duh, Tanzania hii inatisha!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom