Siasa na uraia nani alaumiwe?

Makamba: Bashe si raia
Bashe: Mimi ni raia
Uhamiaji: Nakuhakikisheni Bashe ni raia
Makamba: Hata Uhamiaji waseme nini mimi najua Bashe si raia
Waziri Masha: Ninavyojua uraia wa Bashe hauna utata.
Waandishi wa habari: Je kama hauna utata, Bashe ni raia au vipi
Waziri Masha: Nimesema uraia wake hauna utata, mkitaka kujua zaidi subirini mgombea Uraisi JK atajafafanua kwenye kampeni.
Mag3: Nipeni aspirin.

Maisha yanaendelea ! Hii bongo ati !
 
Mag3: Nipeni aspirin.

Hii kali! naona umeona hawa mbona wanakupasua kichwa? Ukaomba asprin hapo hapo
 
Mkuu heshima mbele.

Mambo yalianza kubadilika mwishoni mwa miaka ya tisini ambapo kulianza kuwepo ufisadi katika kutoa passport za Tanzania kiholela ambapo "middlemen" walikuwa wengi.

Ilikuwa ukitaka passport kwa ajili ya kusafiri unamwona "middleman" ambae anakuhakikishia kuwa ndani ya masaa 24 utakuwa umepata passport hiyo bila matatizo yoyote yale.

Mimi nakumbuka nilipata passport yangu kwa muda wa wiki kama mbili hivi kwa kufuata utaratibu wa kujaza fomu na kuipeleka pale "home affairs" na pia baada ya kuzaja affidavit pale mahakama ya mwanzo kisutu na kulipa ada inayotakiwa.

Lakini kwa muda mrefu nikiwa ughaibuni ambako pia nilikuja kwa kufuata utaratibu nikiwa mtoto wa maskini, nimeshuhudia baadhi ya wasafiri wenzangu katika viwanja mbalimbali vya ndege wenye asili ya Asia au Somalia na hata baadhi ya nchi za Afrika magharibi, wakiwa wamebeba passport za Tanzania lakini kila nilipojaribu kuongea nao kiswahili wanashindwa kujibu hata neno jambo na habari tu.

Hali hii inatatiza sana na huko tunakoelekea tutakuwa na "very- very uncertain future".

Mkuu tayari tmuefika huko. Sasa hivi kuna sehemu moja tu iliyobaki ambayo tunaweza kwenda bila visa, soon tutaanza kudaiwa visa. Walioko madarakani hawajali kwa kuwa wao ni rahisi sana kuomba visa. Lakini kibaya zaidi sasa hivi visa ya Tanzania inahusishwa na dawa za kulevya, kuna watu wengi wanakamatwa na dawa za kulevya wakiwa na passport za Tanzania lakini si watanzania. Pamoja na kuwa kuna watanzania, lakini ukweli ni kwamba kuna ujanja ujanja unatumika pale uhamiaji kuwapa passport ili kwenda kuichafua Tanzania.

Kama Slaa akiingia madarakani moja la muhimu ni kumwambia aangalie utaratibu wa kutoa passport, na kuhakiki zile ambazo tayari zimetolewa. Lazima turudishe heshima ya passport ya Tanzania na heshima ya mtanzania.
 
Makamba: Bashe si raia
Bashe: Mimi ni raia
Uhamiaji: Nakuhakikisheni Bashe ni raia
Makamba: Hata Uhamiaji waseme nini mimi najua Bashe si raia
Waziri Masha: Ninavyojua uraia wa Bashe hauna utata.
Waandishi wa habari: Je kama hauna utata, Bashe ni raia au vipi
Waziri Masha: Nimesema uraia wake hauna utata, mkitaka kujua zaidi subirini mgombea Uraisi JK atajafafanua kwenye kampeni.
Mag3: Nipeni aspirin.

Maisha yanaendelea ! Hii bongo ati !

Baada ya Mag3 kupata aspirin: Vipi kuna maendeleo yoyote kuhusu uraia wa bashe?
Masanja: Tulikuwa tunatania tu, kwa uraia wake ulikuwa na matatizo?
Makamba: Subiri uchaguzi uishe uraia wake utakuwa wa kawaida tu.
Mag3: Naomba panadol naona aspirin haifanyi kazi
 
Hili suala la uraia isije ndio njia ya kuhalalisha ile kampuni ile ya kuchapisha vitambulisho
 
Walioko madarakani wanajua kuwa kuvunja sheria ni jambo la kawaida kwani wao wanafanya hivyo kila siku. Hawana moral authority ya kumkemea yeyote kuwa anavunja sheria kwani wao wenyewe wanazivunja kila siku na hakuna tatizo. Suala ni pale unapokuwa tishio kwa wao kuendelea kuwepo pale walipo. Hata kama hujavunja sheria yoyote utabambikiwa kosa. Jamani haya mambo yapo clear. Polisi akukamate kwa sababu yoyote ile, anataka umpe rushwa akuachie, ukatae kumpa rushwa; nini kinatokea? Anakupeleka ndani, na kesho utabebeshwa misokoto ya bangi (kama unafanana na wavuta bangi) au kete za madawa ya kulevya (kama unaonekana una ukwasi).

Haya mambo yanawapata watu kila siku na tunadhani yako mbali na sisi kwa sababu hayajatukuta. Lakini this is how our government works, kutoka chini kabisa hadi juu. Ukitaka kulijua hilo, we tofautiana na kiongozi yeyote mkubwa, you will prove what I have written here!! Na hiki ndo kinachowakumba hao wanaobambikiwa kuwa si raia. Kwa sababu haya ni madai ambayo kila mtu yanamgusa, wakishasema huyu si raia, basi watu wanaanza kushangaa tu; kumbe fulani si raia?? Wanajua hii ni hot button kwa walio wengi, kama ambavyo yule polisi anavyokusingizia madawa ya kulevya. Majirani zako watasema, aaah ndo maana anaonekana kuwa nazo sana eeh!! Hakuna atakayejiuliza mara mbili.
 
Back
Top Bottom