Siasa kwenye viwanja vipya vya serikali, tunaelekea wapi?

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,459
498
Wanajamvi natoa dukuduku langu, najua siko peke yangu ila kwa niaba yao naomba kuwasilisha, kuna hivi viwanja vipya serikali imevipima hapa DSM nafikiri toka miaka ya 2000 mwanzoni, kuna baadhi ya matajiri wamejitwalia maeneo kinguvu tena yenye hati za wananchi na bado wakawa na jeuri kutisha watu na kuzungushia ukuta viwanja vya watu, Wizara ya ardhi inajua hizi taarifa lakini mpaka leo haijachukua hatua.

Mfano kuna eneo pale Kibada watu wamezuiwa kujenga, jamaa kaziba mpaka njia, taarifa zilifika kabla hata ya kujenga lakini kimyaaa, sasa kesho watu wakiuana kwa ajili ya hayo maeneo au mtu mmoja anapokuwa na ubavu wa kuziba njia ya jumuia (public pale kibada) na kudai yeye ni afisa wa Ikulu ndo nini hasa?

Ni maeneo mengi ninayosikia maamuzi madogo yafanywe lakini hayafanywi, hebu fanyeni kazi yenu bwana, watu tumekopa kwa ajili ya ujenzi ikabidi tununue vibajaj na sasa vimeshachakaa an hela hamna.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom