Ni juzi tu moto uloposhika jengo la Kimathi katikati ya jiji la Nairobi. Ilikuwa ni usiku na baadhi ya local tv walionyesha hili tukio moja kwa moja.
Wengi wetu (nadhani) hatumfahamu Bw. Mwampembwa aka GADO kuwa ni 'mwanaharakati' mwenzetu, kwa wasiolijua hilo ni kuwa huyu ni Mtanzania aliyepiga hatua kubwa sana kimatifa katika nyanja ya utoaji maoni kupitia kazi za katuni.
katuni zake pamoja na kazi zake nyingine zinakuwa na upeo wa hali ya juu sana, japo zinatoka Nation media lakini hata media house nyinginge wanazitumia kudhihirisha kuwa huyu bwana ni mweleawa.
Nasikia alisomea UCLAS mambo ya architecture na ndio kazi yake kabla hajaamua kujikita zaidi kwenye cartoon.