Siasa kuchanganywa na soka

political monger senior

JF-Expert Member
Nov 26, 2020
1,801
5,788
Mwaka 2005, Didier Drogba alimaliza vita ya miaka 5 ya wenyewe kwa wenyewe kwao Ivory Coast alipofunga goli lililosaidia Ivory Coast kuifunga Madagascar.

Aliomba mchezo uchezwe Bouake eneo ambalo ni ngome ya waasi, akafunga halafu akawapigia magoti waasi waachane na vita na waasi walikubali vita ikaisha.

FUNZO
Michezo inaunganisha watu wenye itikadi tofauti na kuwa kitu kimoja, ndio maana mashirikisho ya Kidunia ya michezo mingi kama sio yote yamekataza wanachama wao na vilabu kuingiza mambo ya siasa kwenye michezo.

Mfano Didier Drogba timu yake ya Taifa ya Ivory Coast ingekuwa inajihusisha na siasa za nchini kwao namna yoyote manake waasi wangemchukulia yeye na timu ya Taifa kama “maadui” na wasingemsikiliza wala vita isingeisha kirahisi. Wote tunafahamu faida ya vita kuisha na hizo faida zililetwa na Drogba kupitia soka.

Hapa nchini kwetu pia nimeona tabia ya kutumia picha, mabango na majina ya wanasiasa kwenye mechi au shughuli za vilabu na timu za taifa imeanza kushamiri hasa wakati huu tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ambapo kutakuwa na uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Tanzania nzima.

Natoa rai kwa wahusika kuchukua hatua za haraka na mapema kuondokana na hiki kinachoendelea kwakuwa soka inatuunganisha watu wenye itikadi tofauti tofauti, kwahiyo sio wote watakaokuwa na mapenzi na hisia sawa. Tusifike kule ambako sanaa na wasanii nchini wamefika. Niko tayari kukosolewa... Ameandika JEMEDARI SAID BIN KAZUMARI..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom